Sunday, November 29, 2020

WASTANI WA VIGOGO KUZICHANA NYAVU NJE YA ENEO LA HATARI EPL

Must Read

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali...

LONDON, England

MICHUANO ya Ligi Kuu England ni miongoni mwa mechi zenye wachezaji wenye ushindani mkubwa katika kuziona nyavu.

Hali hiyo ndiyo imekuwa ikiwafanya kuhaha kwa kila njia ili kuhakikisha wanazipa ushindi timu zao.

Katika kuhaha huko, wengine wamekuwa wakijaribu kupiga mashuti ya mbali na kufanikiwa kuzitikisa nyavu.

Katika makala haya BINGWA imejaribu kuangalia wastani wa kila timu wachezaji wao kufunga mabao wakiwa nje ya eneo la hatari.

 

 1. Swansea City

Msimu huu umekuwa mbaya kwa klabu hiyo ya Kusini mwa Wales, licha ya kufanya vibaya katika michezo yake, vilevile imeambulia patupu katika ufungaji wa mabao ya mbali, ambapo kwa sasa wastani wake kwa wachezaji wake kuziona nyavu wakiwa nje ya eneo la hatari ni pointi   10.52.

 

 1. Arsenal

Arsenal nayo ni miongoni mwa timu ambazo zinaonekana kuwa na tatizo kwa wachezaji wake kushindwa kuziona nyavu wakiwa umbali mrefu, ambapo hadi sasa wastani wa klabu hiyo ya Kaskazini mwa jiji la London ni pointi 10.79

 

 1. Manchester City

Ikiwa na idadi ya mabao 53, ambayo ni matano chini ya timu inayoongoza kuziona nyavu, Liverpool, inavyoonekana Kocha  Pep Guardiola hawezi kumtaka straika wake,  Sergio Agüero, mwenye mabao 12 kumpiku mwenzake, Kevin De Bruyne, ambaye ameziona nyavu mara tatu akiwa nje ya eneo la hatari.

Wastani ufungaji mabao ni pointi 10.84

 

 1. Stoke City

Xherdan Shaqiri amefanikiwa kufunga mabao matatu akiwa nje ya eneo la hatari, sawa na wenzake Philippe Coutinho, Zlatan Ibrahimovic, Harry Kane na Gylfi Sigurdsson, ambao ndio wanaongoza kwa ufungaji mabao wakiwa nje ya eneo la hatari kwa Stoke City.

Wastani wa timu hiyo ni pointi 11.03.

 

 

 1. Crystal Palace

Katika orodha hii timu ya Cristal Palace inafanya vizuri kuliko kwenye michuano ya Ligi Kuu ambapo inashika nafasi ya 17 kutokana na kwamba ina wastani wa pointi  11.49.

 1. Middlesbrough

Licha ya Boro kuwa ni moja ya timu ambazo hazipendezi kuziangalia kwenye michuano ya Ligi Kuu, lakini walau katika eneo hili inaonekana kufanya vizuri, ambapo ina wastani wa pointi 11.58

 

 1. West Ham United

Hadi sasa West Ham imefunga takribani mabao 36 katika michuano ya Ligi Kuu na huku ikiwa na wastani wa pointi 11.68 kwa wachezaji wake kuziona nyavu wakiwa nje ya eneo la hatari.

 

 1. West Bromwich Albion

Licha ya kuwa pia na timu hii inashika nafasi za katikati mwa msimamo wa ligi, ikiwa nafasi ya 13, West Brom nayo inaonekana kufanya vizuri katika ufungaji wa mabao ya mbali ambapo wastani wake ni pointi 12.10.

 

 1. Bournemouth

Kama ilivyo West Brom, timu hii nayo inazidiwa kidogo kwa upande wake ikiwa na wastani wa pointi 12.13.

 

 1. Tottenham Hotspur

Harry Kane ndiye anayeibeba timu hiyo kwa upachikaji mabao, akiwa na 19 ambapo matatu kati ya hayo ameyafunga akiwa nje ya eneo la hatari na kuifanya timu hiyo kuwa na wastani wa pointi 12.20.

 1. Everton

Licha ya kuwa katikati mwa msimamo wa ligi, Everton inaonekana pia kufanya vyema katika kuziona nyavu wakiwa nje ya eneo la hatari ambapo wastani wao ni pointi 12.26.

 

 1. Hull City

Licha ya kushika nafasi ya tatu kutoka mwisho kwenye msimamo wa ligi, Hull City nao wanaonekana kuwa wabaya katika kuziona nyavu wakiwa nje ya eneo la hatari ambapo wastani wao ni pointi 12.42.

 

 

 1. Watford

Licha ya kuwa katikati mwa msimamo wa ligi katikati mwa msimu, lakini Watford wanaonekana wana cha kujivunia katika eneo hili kutokana na kuwa wana wastani wa pointi 12.70 kwa kuziona nyavu wakiwa nje ya eneo la hatari.

 

 

 1. Southampton

Kila bao ililolifunga Southampton limepatikana wakati wachezaji wake wakiwa umbali wa yadi 21.71 kutoka langoni, jambo ambalo linawafanya kuwa na wastani wa pointi 12.71.

 

 1. Liverpool

Straika Jordan Henderson alifunga bao akiwa nje ya eneo la hatari dhidi ya  Chelsea  mwanzoni mwa msimu na mengine machache yaliyofungwa na  Coutinho ndiyo yaliyowafanya  Liverpool kushika nafasi ya sita wakiwa na wastani wa pointi  12.74

 

 1. Leicester City

Kiwango cha mabingwa hao watetezi wa Ligi Kuu hakitabiriki kutokana na kwamba siku 14 zilizopita ilikuwa katika ukanda wa kushuka daraja. Lakini kwenye orodha hii wanaonekana kuwa wazuri, wakiwa nafasi ya tano na pointi zao 12.87

 

 1. Sunderland

Licha ya kuwa ndio wanaoburuza mkia kwenye msimamo wa ligi, lakini ni wazuri kwa kufunga mabao ya mbali, wakiwa na wastani wa pointi 13.50.

 1. Manchester United

Baada ya kuanza kwa kusuasua wakiwa chini ya kocha wao mpya, Joe Mourinho, Man United wanaonekana kuzinduka na kufanikiwa kushika nafasi ya tatu kwenye orodha hii, wakiwa na wastani wa pointi  13.53.

 1. Chelsea

Licha ya kuwa ndio wanaoongoza kwenye msimamo wa ligi, wakiwa mbele kwa pointi  10, lakini Chelsea wapo nyuma kwa nafasi moja kwa wachezaji wake kufunga mabao wakiwa nje ya eneo la hatari, baada ya kujikusanyia wastani wa pointi 13.84.

 

 1. Burnley

Wakiwa katikati mwa msimamo wa ligi,  Burnley inashangaza kuongoza msimamo huu wakiwa na wastani wa pointi 14.29.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...

Sarpong ‘aua’ shabiki Simba

Na MWANDISHI WETU, MWANZA BAO la dakika ya 29 lililofungwa na Michael Sarpong wa Yanga juzi, limesababisha kifo cha...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -