Friday, October 30, 2020

Watajwa vipigo Simba

Must Read

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya...

NA MWANDISHI WETU

SIKU chache baada ya Wekundu wa Msimbazi, Simba kukubali kichapo cha mabao 2-1 dhidi ya Mbeya City jijini Mbeya, mapya yameibuka baada ya nyota kadhaa kutajwa kuchangia matokeo mabaya ya timu hiyo.

Simba, ambayo inaongoza ligi kwa pointi 15, imecheza mechi 15, huku ikitoka sare michezo miwili na miwili kufungwa na Tanzania Prisons na African Lyon.

Kufuatia matokeo ya jana, mengi yametajwa kuchangia kwenye kipigo hicho, lakini majina ya nyota kama Awadh Juma, Said Ndemla na Abdi Banda pia yamekuwa yakitajwa kuwa ndiyo chanzo cha kupoteza mchezo huo.

Nyota hao wanatajwa kutokana na kushindwa kupata nafasi kwenye kikosi hicho, kinachonolewa na Joseph Omong, huku wengi wakiamini bado wana uwezo wa kucheza ndani ya timu hiyo.

Awadh, ambaye ana historia ya kubadilisha matokeo, hasa timu hiyo inapozidiwa, hajacheza hata mechi moja ndani ya kikosi hicho, sawa na Banda, huku Ndemla amekuwa akiingizwa kwenye dakika za majeruhi.

Viwango vyao na msaada wao waliowahi kuutoa kwenye kikosi hicho cha Simba umewafanya mashabiki kuwakumbuka na kumtaka kocha huyo mzunguko wa pili kuwapa nafasi kwenye kikosi hicho.

Shabiki kutoka tawi la Temeke, Isihaka Peter, aliliambia BINGWA kuwa kwenye mchezo wao wa juzi dhidi ya Prisons, Ndemla, Awadh na Banda walipaswa kuanza.

“Sitaki kuwataja wachezaji, ila tuweke uongo pembeni juzi wengi walizidiwa, ila mfano angekuwa Banda anajulikana amezoeleka kucheza undava au Awadh hakuna asiyejua amekuwa mtu wa kubadili matokeo mara kadhaa,” alisema.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika ujumbe kupitia ukurasa wake wa...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya kinda wa zamani wa timu...

Afua Suleiman afunguka ‘Utalijua Jiji’ ilivyompa ustaa mjini

NA JEREMIA ERNEST JINA alilopewa na wazazi wake ni Afua Suleiman na hata alipojitupa kwenye ulimwengu wa muziki wa...

Keche: Kundi maarufu Ghana linalowatamani Diamond, Kiba, Harmonize

JIACHIE na Staa Wako, wiki hii tumetua mpaka Accra, Ghana kwa kundi maarufu la muziki nchini humo, Keche linofanya vizuri na ngoma...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -