Sunday, November 29, 2020

WATAONEKANA TENA LIGI KUU BARA

Must Read

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali...

NA ZAINAB IDDY

SINGIDA United na Lipuli zimekuwa za kwanza kurejea katika msimu ujao wa Ligi Kuu Tanzania Bara, zikitokea Ligi Daraja la Kwanza baada ya kuongoza kwa pointi ambazo hazitafikiwa na timu nyingine.

Lipuli ilijihakikishia kurejea ligi kuu  baada ya kushuka daraja kwa zaidi ya miaka 10, kufuatia ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Polisi ya Dar es Salaam.

Kwa matokeo hayo, Lipuli iliweza kufikisha pointi 29 kutoka Kundi A, ambazo hazitafikiwa na timu nyingine kwenye kundi hilo, wakati Singida United ikiongoza Kundi C kutokana na pointi 30.

Singida United licha ya kusaliwa na mchezo mmoja mkononi, walijihakikishia kurejea ligi kuu kufuatia ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Alliance, uliochezwa hivi karibuni kwenye Uwanja wa Namfua mkoani Singida.

Kurejea kwa timu hizo kongwe kutaleta ushindani katika msimu ujao wa ligi kuu, lakini kutatoa fursa kwa mashabiki wa mikoa ya Singida na Iringa kuziona timu zenye mashabiki wengi za Simba na Yanga.

Lakini kubwa zaidi mashabiki wa soka watapata fursa ya kuwaona baadhi ya wachezaji waliopoteza katika ligi kuu na kwenda kuzisaidia timu hizo kupanda au kujerea katika msimu ujao wa ligi hiyo.

Mbali na wachezaji hao ambao waling’ara wakiwa na timu kongwe kama Simba na Yanga, lakini kuna makocha waliowahi kuzifundisha timu za ligi kuu na baadaye kujikuta wakitimuliwa na kwenda kuzinoa timu za daraja la kwanza na kuzipa mafanikio.

Felix Minziro

Ni kocha mwenye uzoefu mkubwa na mikikimikiki ya ligi kuu, licha ya kuifundisha JKT Ruvu, kocha msaidizi wa Yanga na timu nyingine ndiye aliyeiwezesha kuirejesha Singida.

Katika misimu takribani miwili ya ligi kuu, Minziro alipoteza baada ya kuachia ngazi kuifundisha JKT Ruvu kufuatia kufanya vibaya katika mechi za mwanzo za msimu uliopita.

Minziro anatarajiwa katika benchi la Singida United katika msimu ujao wa ligi baada ya kufanikiwa kuirejesha.

 Richard Amatre 

Kocha raia wa Uganda aliyeirudisha Lipuli na aliyewahi kuwa kocha msaidizi wa Simba ikiwa chini ya kocha mkuu mganda mwenzake, Moses Basena.

Nizar Khalfani

KIUNGO wa zamani wa kimataifa wa Tanzania wa klabu ya Vancouver Whitecaps ya Canada, aliyewahi kuzichezea timu za Moro United iliyoshuka daraja ligi kuu, Yanga na Mwadui.

Baada ya kutemwa na Mwadui, sasa Nizar anatarajia kuonekana ligi kuu msimu ujao wakiwa na kikosi kipya cha Singida United.

 

Said Lubawa

Unapolitaja jina la Lubawa katika miaka ya hivi karibuni, unawakumbusha wadau wa soka la Tanzania katika mchezo wa Simba dhidi ya Mgambo Shooting iliyoshuka daraja msimu uliopita wa ligi kuu.

Katika mchezo huo wa mzunguko wa kwanza, Lubawa anayecheza nafasi ya kipa, aliweza kufanya kazi kubwa ya kuokoa hatari nyingi langoni mwake, licha ya Simba kuondoka na ushindi wa mabao 2-0 uliochezwa kwenye Uwanja wa Mkwakwani, jijini Tanga.

Baada ya kushuka daraja msimu uliopita, kipa huyo chipukizi alitimkia katika kikosi cha Singida United aliyoipigania hadi kuweza kufanikiwa kurejea ligi kuu.

Salum Machaku

Ni mshambuliaji mwenye historia ndefu katika Ligi Kuu Bara, akiwa amecheza katika klabu mbalimbali kongwe hapa nchini ikiwamo Simba.

Kabla ya kutua Simba waliwahi kuichezea Mtibwa Sugar na baadaye kurejea tena kwenye kikosi hicho na baadaye Polisi Moro ambayo kwa sasa inashiriki Ligi Daraja la Kwanza baada ya kushuka.

 

Machaku tunarajia kumwona tena katika kikosi cha Lipuli kitakachoandaliwa kwa ajili ya msimu mpya wa ligi kuu kutokana na mchango wake mkubwa ya kuirejesha ligi kuu timu hiyo.

Ally Mohamed

Kipa kinda aliyeiwezesha Lipuli kurejea ligi kuu, lakini akiwa na uzoefu wa kutosha aliyetumikia Tanzania Prisons.

Wengine wanaotarajia kuonekana kwenye ligi hiyo ni Salum Kipaga na Salum Mlima (Singida United ambao walikuwa wakikipiga Mgambo Shooting, Rashid Gumbo, Mtibwa, African Lyon, Simba na Yanga.

Lakini Hamis Sengo aliyewahi kuichezea  JKT Ruvu na Mohamed Titi  Coastal union iliyoshuka daraja.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...

Sarpong ‘aua’ shabiki Simba

Na MWANDISHI WETU, MWANZA BAO la dakika ya 29 lililofungwa na Michael Sarpong wa Yanga juzi, limesababisha kifo cha...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -