Tuesday, October 27, 2020

Wawa anukia Yanga

Must Read

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya...

NA SALMA MPELI

MKATABA wa beki wa Azam, Pascal Serge Wawa, na klabu yake unakaribia kumalizika na kuna tetesi kuwa staa huyo wa kimataifa wa Ivory Coast, ananukia kwenye kikosi cha mabingwa watetezi wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, Yanga.

Hivi karibuni, Wawa aliwahi kunukuliwa na mtandao mmoja wa michezo nchini akisema kuwa,licha ya mkataba wake Azam kubakisha miezi miwili, hafahamu juu ya mustakabali wake ndani ya timu hiyo.

Wawa alisemabado hajaanza mazungumzo yoyote ya kuongeza mkataba nauongozi wa klabu yake hiyo na kufunguka kuwa kwa sasa kuna klabu tatu zinaitaka saini yake, ambapo alidai kuwa mbili ni kutoka Uarabuni huku moja ikiwa ni ya hapahapa nchini.

Licha ya kutoweka wazi ni timu gani ya hapa iliyopeleka ofa kwake, BINGWA linataarifa kuwa ofa hiyo inatoka Yanga kwa sababu miamba hiyo ya Jangwani ndiyo klabu pekee nchini ambayo inaweza kuwa na nguvu ya fedha ya kupambana na Azam.

Mchezaji huyo ambaye kwa sasa anasugua benchi kwa muda mrefu sasa kutokana na majeraha ya goti aliyopata Aprili 10, mwaka huu wakati timu hiyo ikiichapa Esperance ya Tunisia kwa mabao 2-1 kwenye mchezo wa raundi ya pili ya Kombe la Shirikisho Afrika.

BINGWA lilizungumza na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Azam, Saad Kawemba,kufahamu kama klabu hiyo ina mpango wa kumbakisha beki huyo au la, kitu ambacho bosi huyo hakutaka kukiweka wazi.

Kawemba alisema suala la mazungumzo ya kuongeza mkataba lipo kati ya klabu ya mchezaji husika na si lazima kutangaza kuwa ni lini watakaa na kuzungumza.

“Mbali na Wawa, wapo wachezaji takribani sita ambao mikataba yao imemalizika na wote hao wapo kwenye kikosi cha kwanza, hivyo lini uongozi utafanya mazungumzo nao kwa ajili ya mkataba mpya ni siri yetu na si lazima tuweke wazi,” alisema Kawemba.

Wakati Azam wakiendelea kujivuta kukaa mezani na Wawa, Yanga imekuwa ikifuatilia mchakato mzima na kuna uwezekano beki huyo akatua Jangwani kiulaini tofauti na matarajio ya wengi.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika ujumbe kupitia ukurasa wake wa...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya kinda wa zamani wa timu...

Afua Suleiman afunguka ‘Utalijua Jiji’ ilivyompa ustaa mjini

NA JEREMIA ERNEST JINA alilopewa na wazazi wake ni Afua Suleiman na hata alipojitupa kwenye ulimwengu wa muziki wa...

Keche: Kundi maarufu Ghana linalowatamani Diamond, Kiba, Harmonize

JIACHIE na Staa Wako, wiki hii tumetua mpaka Accra, Ghana kwa kundi maarufu la muziki nchini humo, Keche linofanya vizuri na ngoma...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -