Sunday, January 17, 2021

WAWA: NAKUJA YANGA

Must Read

Usiyoyajua sare ya Leicester, United

NI katika mechi ya Ligi Kuu ya England iliyomalizika kwa sare ya mabaon 2-2.-Man United wamemiliki mpira...

Eti Zidane anapangiwa kikosi!

IMEFICHUKA kuwa wachezaji waandamizi wa Real Madrid walikaa kikao na Zinedine Zidane kumwambia wachezaji anaopaswa kuwapanga na...

DIDA ASAINI IHEFU FC

Golikipa wa zamani wa Yanga na Simba, Deogratius Munishi ‘Dida’ amejiunga na Timu ya Ihefu inayoshiliki Ligi...

 

WAWA

NA THERESIA GASPER

BEKI wa zamani wa Azam FC, Pascal Wawa, ameibuka na kufichua kwamba ameshafanya mazungumzo na Yanga na kuweka wazi kwamba yuko tayari kuja kujiunga na mabingwa hao wa Ligi Kuu Tanzania Bara.

Wawa ambaye kwa sasa ni mchezaji huru baada ya kumaliza mkataba wake na timu ya El Merreikh ya Sudan, alisema kwamba anachosubiri ni kuwekewa ‘mpunga’ mezani atue Yanga.

Beki huyo anapewa nafasi kubwa ya kuziba pengo la Vincent Bossou aliyeondoka Yanga, baada ya timu hiyo kushindwa kumpa kiasi cha fedha alichohitaji baada ya kumaliza mkataba.

Akizungumza na BINGWA jana, Wawa alisema yuko tayari kutua Jangwani na kuahidi kupiga kazi kama atawekewa ofa ya kuridhisha.

“Kuna kiongozi wa Yanga alimpigia simu wakala wangu na kusema wananihitaji nije kucheza Tanzania, wameambiwa wamtumie ofa kwenye barua pepe (email) kwa hiyo kwa sasa tuwawasubiri,” alisema Wawa.

“Kimsingi mimi ni mchezaji huru, kama tutaafikiana sitakuwa na pingamizi kuja kucheza Yanga, nina uhakika nitafanya kazi vizuri na uwezo kwa kuwa hakuna asiyeujua uwezo wangu,” alisema beki huyo.

Beki huyo aliyeichezea Azam FC misimu miwili, alitengeneza ukuta mgumu kwa kushirikiana na Agrey Morris na kuifanya klabu hiyo ya Chamazi kuwa na safu nzuri ya ulinzi.

Yanga inahitaji kuongeza beki mwingine baada ya kuondka kwa Bosou, huku Kelvin Yondani na Nadir Haroub ‘Cannavaro’ ikionekana kuwa umri umeshaanza kuwatupa mkono na Vincent Andrew ‘Dante’ na Abdallah Shaibu ‘Ninja kutokuwa na uzoefu wa kutosha kwenye kikosi hicho.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Usiyoyajua sare ya Leicester, United

NI katika mechi ya Ligi Kuu ya England iliyomalizika kwa sare ya mabaon 2-2.-Man United wamemiliki mpira...

Eti Zidane anapangiwa kikosi!

IMEFICHUKA kuwa wachezaji waandamizi wa Real Madrid walikaa kikao na Zinedine Zidane kumwambia wachezaji anaopaswa kuwapanga na ndiyo maana timu hiyo imeshinda...

DIDA ASAINI IHEFU FC

Golikipa wa zamani wa Yanga na Simba, Deogratius Munishi ‘Dida’ amejiunga na Timu ya Ihefu inayoshiliki Ligi Kuu Tanzania Bara katika kipindi...

JDart Nation wapanga kutawala Africa

CHRISTOPHER MSEKENA MWANAMUZIKI na bosi wa JDart Nation, JDart, amesema miongoni mwa mipango yake kwa mwaka 2021 ni kuhakikisha...

HUJUMA NZITO YANGA

NA WINFRIDA MTOI UONGOZI wa Yanga upo katika harakati za kuhamishia mechi zao zilizobaki za Ligi Kuu Tanzania Bara...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -