Sunday, October 25, 2020

WAAMUZI WASIMAMIE SHERIA 17 MZUNGUKO WA PILI VPL

Must Read

Fati aweka rekodi Barcelona

CATALUNYA, Hispania ANSU Fati ameweka rekodi ya mchezaji kinda wa kwanza kufunga mabao...

Lampard amshika mkono Silva

MANCHESTER, England KOCHA wa Chelsea, Frank Lampard, amesema atamtumia, Thiago Silva, katika mechi nyingi msimu huu licha ya...

Tuchel awatolea uvivu Mbappe, Neymar

PARIS, Ufaransa KOCHA wa PSG, Thomas Tuchel, amechukizwa na kiwango kibovu walichoonyesha mastaa wa timu hiyo, Kylian...

BODI ya Ligi (TPLB) imewatoa kwenye ratiba ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL) waamuzi kadhaa ambao walichezesha chini ya kiwango baadhi ya mechi za mzunguko wa kwanza wa ligi na zile za Ligi Daraja la Kwanza Tanzania Bara (FDL).

Uamuzi huo umetolewa baada ya kikao cha Kamati ya Usimamizi na Uendeshaji wa Bodi ya Ligi kilichofanyika karibuni kujiridhisha kuwa waamuzi hao walishindwa kusimamia sheria 17 za mchezo wa soka katika baadhi ya mechi walizochezesha.

Waamuzi walioondolewa kwenye ratiba hiyo ni pamoja na Martin Saanya na mshika kibendera Samweli Mpenzu, waliochezesha pambano la Simba na Yanga, Mwamuzi Rajabu Mrope aliyechezesha pambano la Mbeya City na Yanga na mwamuzi Thomas Mkombozi aliyechezesha mechi ya FDL kati ya Coastal Union na KMC.

Mbali na kuwaondoa kwenye ratiba waamuzi hao, suala lao limerudishwa kwenye Kamati ya Waamuzi kwa ajili ya kushughulikiwa kitaalamu na ikibidi kuwachukulia hatua zaidi au kuwasafisha kwa jinsi kamati hiyo itaona inafaa.

Kufuatia hatua hizo zilizochukuliwa na Bodi ya Ligi, kupitia Kamati yake ya Usimamizi na Uendeshaji, BINGWA tunaamini uamuzi huu umetoka kwa kuzingatia weledi na si presha ya baadhi ya watu.

Tunatoa wito kwa waamuzi wengine wa VPL na FDL kuitazama hatua hii ya Bodi ya Ligi dhidi ya akina Saanya kama mfano na kujidhatiti katika kusimamia sheria 17 za soka kila watakapopata nafasi ya kuamua mechi.

Tunaamini kama waamuzi wakisimamia sheria 17 za soka basi watakuwa salama na watajiepusha na rungu kama hili lililowashukia wenzao ambao walishindwa kusimamia dhamana waliyopewa uwanjani.

Mbali na kutoa wito kwa waamuzi kusimamia sheria 17 za soka, kuelekea mzunguko wa pili wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, BINGWA tunaitaka Bodi ya Ligi na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kuwaadhibu wale wote watakaotoa maneno au lugha za kuudhi dhidi ya waamuzi.

Tunasema hivi kwa sababu tunafahamu kuna Kamati na vyombo vilivyowekwa kwa ajili ya kushughulikia waamuzi pindi wanapoboronga, hivyo tunawataka wachezaji na viongozi wa vilabu kufikisha malalamiko yao kwenye vyombo hivyo na si kupiga kelele kwenye vyombo vya habari pindi wakiona hawajatendewa haki.

Tunaamini ni jukumu la TPLB na TFF kulinda waamuzi dhidi ya mashabiki, wachezaji, makocha na viongozi wa timu pale inapotokea wanashambuliwa kwa maneno au hata kutaka kudhuliwa kama ilivyokuwa kwa Mkombozi mkoani Tanga kwenye mechi ya Coastal Union na KMC.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Fati aweka rekodi Barcelona

CATALUNYA, Hispania ANSU Fati ameweka rekodi ya mchezaji kinda wa kwanza kufunga mabao...

Lampard amshika mkono Silva

MANCHESTER, England KOCHA wa Chelsea, Frank Lampard, amesema atamtumia, Thiago Silva, katika mechi nyingi msimu huu licha ya kuwa na umri wa miaka...

Tuchel awatolea uvivu Mbappe, Neymar

PARIS, Ufaransa KOCHA wa PSG, Thomas Tuchel, amechukizwa na kiwango kibovu walichoonyesha mastaa wa timu hiyo, Kylian Mbappe na Neymar, kwenye mechi...

IBRA:Kifaa kipya Konde Gang aliyetembea kwa mguu kumwinda Harmonize

NA BRIGHITER MASAKI UKITAJA vijana wanaofanya vizuri katika mziki wa bongo fleva, huwezi kukosa kumtaja msanii chipukizi anayefahamika zaidi...

Jay-Z: Mama aliingilia bifu langu na Nas

-Z: Mama aliingilia bifu langu na Nas New York, Marekani HAKUNA shabiki wa Hip hop asiyelifahamu...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -