Sunday, November 1, 2020

WAZAZI BADO HAWAJUI UMUHIMU WA MICHEZO KWA WATOTO

Must Read

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya...

NA WINFRIDA MTOI

LICHA ya kuwa michezo imekuwa ni ajira kubwa ulimwenguni kote, bado wazazi wameonekana kukosa uelewa juu ya umuhimu wa kumjenga mtoto katika michezo angali akiwa na umri mdogo.

Wazazi wengi wamekuwa wakichukulia michezo ni kitu cha mwisho katika mambo mengi wanayofikiria kuhusu  maisha ya watoto wao na kuwafanya washindwe kugundua vipaji vyao na matokeo yake vinapotea.

Ifahamike kuwa ili kumjenga mtoto katika misingi bora ya maisha yake ya baadaye, lazima kuanzia chini wakati akiwa na umri mdogo. Katika umri huu ndipo unapobaini mtoto wako ana kipaji gani  ili  kuweza kumwendeleza na kile kitu anachokimudu na kukipenda.

Wapo watoto wengi wenye vipaji vya michezo lakini wazazi ndio wamekuwa wagumu kutoa nafasi kwao. Wenzetu katika nchi zilizoendelea wamekuwa wakihusudu zaidi kipaji cha mtoto hasa katika michezo na ndio sababu wameweza kupatikana kina Ronaldo na Messi na wengine wanaowika duniani.

Huku kwetu jambo hilo limekuwa ni gumu kwa wazazi wengi na matokeo yake wanaangalia kile wanachokiona wao kimewafanikisha.

Hilo ni kosa, kwani kila mwanadamu anazaliwa na kipaji chake na wachache ndio wanaweza kuwa na vipaji sawa na wazazi au wengine hurithi kulingana na  yale wanayokuta wazazi wakifanya na kupendezewa kuwa kama walivyo.

Nimekuwa nikitembelea mara nyingi katika kituo cha michezo kwa vijana cha Jakaya Mrisho Kikwete (JMK Youth Sports Centre), Kidongo Chekundu, jijini Dar es Salaam na kubaini jambo hili kuwa wazazi hawatoi kipaumbele wa watoto wao juu ya kujifunza michezo.

Katika kituo hiki kuna programu za michezo mbalimbali zinaendeshwa kwa watoto, lakini imekuwa ngumu kwa wazazi wa Kitanzania kuhamasisha watoto wao kwenda sehemu hiyo.

Kituo hicho hakina masharti makubwa ya mtoto kuingia maeneo hayo na kucheza na kujifunza michezo zaidi ya kusajiliwa na kufuata taratibu, huku programu nyingi zikiwa zinaendeshwa jioni baada ya masomo.

Mara nyingi ninapokuwa maeneo hayo, wazazi ninaoona wameongozana na watoto wao kuwapeleka eneo hilo ni wale wa kigeni wanaoishi nchini.

Isitoshe programu zinaendeshwa bila malipo yoyote labda kwa wale wanaoishi hapo hapo wana taratibu zao nyingine wanazopewa na uongozi.

Hapo mtoto anapata vifaa vyote vya kujifunzia mchezo anaopenda na walimu wenye taaluma hiyo, lakini cha ajabu imekuwa ngumu kwa wazazi kuunga mkono jitihada hizo.

Ukweli ni kwamba, wapo watoto wengi wenye vipaji na wanaopenda kucheza michezo tofauti, mfano mzuri ukiwa nje ya kituo hicho utaona watoto wengi wakichungulia na kufurahia kinachoendelea humo lakini wamekosa mwongozo wa wazazi au kuhofia kwenda kuadhibiwa nyumbani wanaporudi wamechelewa.

Zipo shule zenye utaratibu wa kupeleka wanafunzi wao katika kituo hicho na kushiriki mashindano yanayoandaliwa kituoni hapo, lakini hiyo haiwezi kumsadia mtoto kama atakuwa anakosa sapoti ya mzazi wake.

Wazazi wanatakiwa kutambua kwamba, michezo hivi sasa ni ajira na haichezwi kwa kujifurahisha kama zamani na ndio sababu katika nchi nyingi duniani wawekezaji na kampuni nyingi wameamua kuwekeza zaidi katika michezo.

Hiyo ni moja ya fursa wazazi wanayotakiwa kutumia hasa wale waliopo maeneo ya karibu na kituo hicho kutoa nafasi kwa watoto wao kucheza, kwani kumjenga mtoto wako katika michezo na kuondokana na ile dhana ya kuona michezo itampotezea muda wa kusoma mtoto wako.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika ujumbe kupitia ukurasa wake wa...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya kinda wa zamani wa timu...

Afua Suleiman afunguka ‘Utalijua Jiji’ ilivyompa ustaa mjini

NA JEREMIA ERNEST JINA alilopewa na wazazi wake ni Afua Suleiman na hata alipojitupa kwenye ulimwengu wa muziki wa...

Keche: Kundi maarufu Ghana linalowatamani Diamond, Kiba, Harmonize

JIACHIE na Staa Wako, wiki hii tumetua mpaka Accra, Ghana kwa kundi maarufu la muziki nchini humo, Keche linofanya vizuri na ngoma...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -