Thursday, December 3, 2020

Waziri amrudisha Pluijm Yanga

Must Read

HUJUMA NZITO YANGA

NA WINFRIDA MTOI UONGOZI wa Yanga upo katika harakati za kuhamishia mechi zao zilizobaki...

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

NA ZAITUNI KIBWANA

WAZIRI wa Mambo ya Ndani, Mwigulu Nchemba, amemrejesha aliyekuwa Kocha wa Yanga, Hans van der Pluijm ambaye alijiuzulu kuinoa timu hiyo mapema wiki hii.

Pluijm alijiuzulu baada ya Yanga kumleta Mzambia, George Lwandamina, aliyeingia mkataba wa miaka miwili kukinoa kikosi hicho mara baada ya kumaliza mkataba wake na Zesco.

Kufuatia kujiuzulu kwa Pluijm, Nchemba aliamua kuingilia kati suala hilo na kufanya mazungumzo na kocha huyo takribani siku tatu ambapo sasa amekubali kuendelea kukinoa kikosi hicho cha Wanajangwani.

Awali, Mwigulu ambaye ni mpenzi na mwanachama wa Yanga, alianza mazungumzo na wachezaji wa timu hiyo na baadaye kuwashauri viongozi kumrudisha Pluijm.

Kwenye taarifa iliyotumwa kwenye vyombo vya habari iliyosainiwa na Katibu Mkuu wa Yanga, Baraka Deusdedit jana imasema hawaoni sababu ya kuachana na Mholanzi huyo baada ya mafanikio waliyoyapata.

“Toka amejiunga na Yanga Desemba 2014, umeisaidia timu kutwaa taji la Ligi Kuu Tanzania Bara mara mbili Kombe la FA, hivyo hatuoni sababu ya kuachana na wewe,” aliandika Baraka kwenye barua hiyo.

Pluijm alijiuzulu mapema wiki hii baada ya kukerwa na uongozi wa klabu kuleta kocha mpya kutoka Zambia, George Lwandamina, bila kumtaarifu.

Mholanzi huyo tayari alishawaaga wachezaji wa timu hiyo na kukosekana kwenye mechi dhidi ya JKT Ruvu iliyosimamiwa na msaidizi wake, Juma Mwambusi, huku ikishinda 4-0.

Uongozi wa Yanga ulitaka kumwondoa Pluijm na wasaidizi wake wote, Juma Mwambusi, kocha wa makipa, Juma Pondamali na meneja Hafidh Saleh na kuwaleta Mzambia Lwandamina atakayekuwa kocha mkuu, akisaidiwa na Charles Mkwasa, kocha wa makipa Manyika Peter na meneja ni Sekilojo Chambua.

Pluijm, aliyezaliwa Januari 3, mwaka 1949, alikuwa anaifundisha Yanga katika awamu ya pili baada ya awali kufundisha kwa nusu msimu mwaka 2014, akimpokea Mholanzi mwenzake, Ernie Brandts.

Pluijm alitaka kuondoka Jangwani baada ya kuiongoza Yanga katika jumla ya mechi 124, akishinda 77, sare 25 na kufungwa 22.

Katika mechi 19 za nusu msimu mwaka 2014, alishinda 11, sare sita na kufungwa mbili, wakati katika mechi 106 za tangu mwaka jana, alishinda 66, sare 19 na kufungwa 20.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

HUJUMA NZITO YANGA

NA WINFRIDA MTOI UONGOZI wa Yanga upo katika harakati za kuhamishia mechi zao zilizobaki...

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul 'Ben Pol' ameshukuru mashabiki kwa...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -