Tuesday, November 24, 2020

WAZIRI MWAKYEMBE KUNA VIPORO VYA BAJETI JITAHIDI VIISHE

Must Read

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali...

NA IRENE MPATWA, OUT

HIVI Karibuni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Pombe Magufuli, alifanya mabadiliko kidogo ya Baraza lake la Mawaziri, ambayo yalishuhudia aliyekuwa Waziri wa Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo, Nape Nnauye, akiondoka na nafasi yake kuchukuliwa na Dk. Harrison Mwakyembe.

Ni kawaida kwenye shughuli za kisiasa mambo kama hayo kutokea, tunampongeza sana Nape kwa kazi nzuri aliyoifanya katika Wizara hiyo hasa katika kujenga misingi mizuri ya setka zote nne zilizopo kwenye wizara yake.

Katika kipindi hiki licha ya kwamba bajeti ya Wizara hiyo ni ndogo, lakini Serikali ilijitahidi kutoa kiasi fulani cha fedha katika taasisi zake ambazo nyingine hazikuwa zimepata mgawo wa fedha za maendeleo kwa kipindi kirefu kutoka serikalini.

Wadau wa sekta ya Sanaa, Utamaduni na Michezo, wataendelea kukumbuka mchango japo mdogo wa Nape katika uongozi wake. Lakini wakati hayo yametokea, hatuna budi kumkaribisha kwa moyo mkunjufu Waziri mpya Mwakyembe ambaye anapokea kijiti cha Nape katika harakati za kuendeleza gurudumu la maendeleo kwenye wizara hiyo yenye sekta nne.

Karibu sana Waziri Mwakyembe, lakini wakati unaingia ni vyema ukafahamu kwamba hadi sasa baadhi ya taasisi zilizopo kwenye Wizara yako hazijakamilishiwa bajeti yake kama ambavyo ilitengwa na Bunge na hivyo kushindwa kukamilisha miradi yake ya maendeleo katika kipindi cha mwaka huu.

Moja ya taasisi ambazo zinahitaji sana kukamilishiwa bajeti yake ni Taasisi ya Sanaa na Utamaduni ya Bagamoyo (TaSUBa), ambayo ilitengezewa shilingi milioni 300 na hadi sasa imepatiwa milioni 100 tu ambazo hazitoshi kukamilisha mradi wa maendeleo uliokusudiwa.

Hivyo basi, tunaamini wewe Mwakyembe ni moja ya watu makini ambao hawahitaji muda mrefu kujifunza mambo, kwa kazi uliyoifanya wakati ukiwa Waziri wa Uchukuzi na kutuachia treni ya Mwakyembe jijini Dar es Salaam, basi ni matumaini yangu kwamba utahakikisha viporo vya bajeti katika taasisi zilizo chini ya Wizara yako mpya vinakamilika kabla ya mwaka wa bajeti kuisha.

Pamoja na viporo vya bajeti, lakini ni vyema ukafahamu kwamba kuna changamoto nyingi sana kwenye taasisi zilizo chini ya Wizara yako, vilio vya wasanii juu ya wizi na uharamia wa kazi zao bado vipo kwa sauti ya juu, vilio vya wadau wa michezo juu ya mafanikio kwenye mashindano ya kimataifa bado vipo kwa sauti ya juu na kwenye sekta ya habari ndiyo kama ambavyo unasikia changamoto ni nyingi licha ya kwamba umepewa maagizo makali na Rais juu ya sekta ya habari hasa vyombo binafsi, lakini ninaamini utajiongeza  kutokana na hali halisi iliyopo.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...

Sarpong ‘aua’ shabiki Simba

Na MWANDISHI WETU, MWANZA BAO la dakika ya 29 lililofungwa na Michael Sarpong wa Yanga juzi, limesababisha kifo cha...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -