Sunday, January 17, 2021

‘WE RONALDO NAKUCHUKIA’

Must Read

Usiyoyajua sare ya Leicester, United

NI katika mechi ya Ligi Kuu ya England iliyomalizika kwa sare ya mabaon 2-2.-Man United wamemiliki mpira...

Eti Zidane anapangiwa kikosi!

IMEFICHUKA kuwa wachezaji waandamizi wa Real Madrid walikaa kikao na Zinedine Zidane kumwambia wachezaji anaopaswa kuwapanga na...

DIDA ASAINI IHEFU FC

Golikipa wa zamani wa Yanga na Simba, Deogratius Munishi ‘Dida’ amejiunga na Timu ya Ihefu inayoshiliki Ligi...

MADRID, Hispania

Antoine Griezmann amemchana ‘live’ Cristiano Ronaldo kwamba anamchukia, baada ya Ureno kuifunga Ufaransa kwenye fainali ya michuano ya Euro 2016.

Les Bleus walikuwa wakipewa nafasi kubwa ya kuibuka na taji la ubingwa huo wa Mataifa ya Ulaya Julai mwaka huu, lakini bao lililofungwa dakika 30 za nyongeza na mshambuliaji wa zamani wa Swansea, Eder, liliipa Ureno taji hilo.

Hiyo ilikuwa ni kwa mara ya pili Ronaldo kuzima ndoto za mafanikio ya Griezmann barani Ulaya, baada ya kufunga penalti ya ushindi na kuisaidia Real Madrid kunyakua taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Atletico Madrid katika fainali iliyofanyika msimu uliopita.

Ronaldo ambaye alitolewa kipindi cha kwanza kwa machela kwenye mchezo wa fainali hiyo ya Euro 2016, baada ya kupata majeraha kwa kukanyangwa na Griezmann, alifunguka kwamba mshambuliaji huyo wa Ufaransa na Atletico alimwambia anamchukia baada ya kukutana wakati wa mapumziko ya msimu uliopita.

“Inachekesha, kwa sababu muda mfupi baada ya fainali wakati tuko kwenye mapumziko mjini Miami (Marekani), nilikutana na Antoine Griezmann kwenye mgahawa mmoja ambapo alikuwa anakula chakula cha jioni na mchumba wake. Alikuja kwenye meza yangu kuniona akiwa na tabasamu la dharau na kuniambia ‘Cristiano, nakuchukia,” anasema Ronaldo alipozungumza na mtandao wa Sport.

Ronaldo alimfunika Griezmann tena mwishoni mwa wiki iliyopita alipopiga ‘hat-trick’ wakati Madrid wakishinda mabao 3-0 katika mchezo wa La Liga dhidi ya Atletico kwenye Uwanja wa Vicente Calderon.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Usiyoyajua sare ya Leicester, United

NI katika mechi ya Ligi Kuu ya England iliyomalizika kwa sare ya mabaon 2-2.-Man United wamemiliki mpira...

Eti Zidane anapangiwa kikosi!

IMEFICHUKA kuwa wachezaji waandamizi wa Real Madrid walikaa kikao na Zinedine Zidane kumwambia wachezaji anaopaswa kuwapanga na ndiyo maana timu hiyo imeshinda...

DIDA ASAINI IHEFU FC

Golikipa wa zamani wa Yanga na Simba, Deogratius Munishi ‘Dida’ amejiunga na Timu ya Ihefu inayoshiliki Ligi Kuu Tanzania Bara katika kipindi...

JDart Nation wapanga kutawala Africa

CHRISTOPHER MSEKENA MWANAMUZIKI na bosi wa JDart Nation, JDart, amesema miongoni mwa mipango yake kwa mwaka 2021 ni kuhakikisha...

HUJUMA NZITO YANGA

NA WINFRIDA MTOI UONGOZI wa Yanga upo katika harakati za kuhamishia mechi zao zilizobaki za Ligi Kuu Tanzania Bara...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -