Friday, October 23, 2020

WEMA ASOTA MAHABUSU

Must Read

Fati aweka rekodi Barcelona

CATALUNYA, Hispania ANSU Fati ameweka rekodi ya mchezaji kinda wa kwanza kufunga mabao...

Lampard amshika mkono Silva

MANCHESTER, England KOCHA wa Chelsea, Frank Lampard, amesema atamtumia, Thiago Silva, katika mechi nyingi msimu huu licha ya...

Tuchel awatolea uvivu Mbappe, Neymar

PARIS, Ufaransa KOCHA wa PSG, Thomas Tuchel, amechukizwa na kiwango kibovu walichoonyesha mastaa wa timu hiyo, Kylian...

Na HERIETH FAUSTINE

JESHI la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, limeendelea kumshikilia  mwigizaji wa filamu ambaye alikuwa Miss Tanzania mwaka 2006, Wema Sepetu na wenzake saba kwa madai ya kusubiria upelelezi ukamilike.

Wema ameendelea kusota rumande tangu alipokamatwa Februari 3, mwaka huu, kabla ya polisi kukagua nyumbani kwake na kukuta misokoto ya bangi na karatasi za kusokotea.

Akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam, Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu, Kamishna Simon Sirro, alisema wanasubiria majalada yao yafikishwe kwa wakili wa Serikali ili aweze kuyapitia na kuona ushahidi uliopo kisha kupelekwa kwa Mkemia Mkuu.

“Mtuhumiwa Wema Sepetu na wenzake saba ambao walikamatwa na vielelezo vya dawa za kulevya bado wapo ndani wakisubiria upelelezi ukamilike na  majalada yao tumeyapeleka kwa wakili wa Serikali ili ayapitie na kuona ushahidi uliopo pamoja na kupata majibu kutoka kwa Mkemia Mkuu wa Serikali, kwahiyo naamini upelelezi ukikamilika  watapelekwa mahakamani,” alisema.

Wema ni miongoni mwa wasanii 13 waliotajwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda ambao walitakiwa kukutana naye Kituo Kikuu cha Polisi Kati kwa mahojiano kutokana na tuhuma za utumiaji wa dawa za kulevya.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Fati aweka rekodi Barcelona

CATALUNYA, Hispania ANSU Fati ameweka rekodi ya mchezaji kinda wa kwanza kufunga mabao...

Lampard amshika mkono Silva

MANCHESTER, England KOCHA wa Chelsea, Frank Lampard, amesema atamtumia, Thiago Silva, katika mechi nyingi msimu huu licha ya kuwa na umri wa miaka...

Tuchel awatolea uvivu Mbappe, Neymar

PARIS, Ufaransa KOCHA wa PSG, Thomas Tuchel, amechukizwa na kiwango kibovu walichoonyesha mastaa wa timu hiyo, Kylian Mbappe na Neymar, kwenye mechi...

IBRA:Kifaa kipya Konde Gang aliyetembea kwa mguu kumwinda Harmonize

NA BRIGHITER MASAKI UKITAJA vijana wanaofanya vizuri katika mziki wa bongo fleva, huwezi kukosa kumtaja msanii chipukizi anayefahamika zaidi...

Jay-Z: Mama aliingilia bifu langu na Nas

-Z: Mama aliingilia bifu langu na Nas New York, Marekani HAKUNA shabiki wa Hip hop asiyelifahamu...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -