Sunday, January 17, 2021

MO AWAOKOA MASHABIKI SIMBA

Must Read

Usiyoyajua sare ya Leicester, United

NI katika mechi ya Ligi Kuu ya England iliyomalizika kwa sare ya mabaon 2-2.-Man United wamemiliki mpira...

Eti Zidane anapangiwa kikosi!

IMEFICHUKA kuwa wachezaji waandamizi wa Real Madrid walikaa kikao na Zinedine Zidane kumwambia wachezaji anaopaswa kuwapanga na...

DIDA ASAINI IHEFU FC

Golikipa wa zamani wa Yanga na Simba, Deogratius Munishi ‘Dida’ amejiunga na Timu ya Ihefu inayoshiliki Ligi...

NA ZAITUNI KIBWANA

MASHABIKI wa klabu ya Simba sasa watakuwa na ahueni, baada ya wanachama waliokuwa wakipinga Mohamed Dewji ‘Mo’ kupewa timu kuamua kusalimu amri na sasa watakabana na mahasimu wao katika mbio za ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara.

Kitendo hicho cha Katibu wa Baraza la Wadhamini, Hamis Kilomoni, kuamua kuungana na wenzake na kumpisha Mo kuendesha klabu hiyo, kitakuwa kama kimewaokoa mashabiki wa Simba ambao walikuwa hawajui hatima ya timu yao.

Awali Simba ilikuwa haipo sawa na Baraza la Wadhamini chini ya Kilomoni mpaka kufikia kwenda mahakamani kupinga mkutano mkuu wa dharura.

Lakini akizungumza kwenye mkutano wa waandishi wa habari jana, Rais wa Simba, Evans Aveva, alisema wamefikia azimio la kuungana baada ya kukaa kwa pamoja na baraza hilo chini ya Mwenyekiti wake Ramesh Patel.

“Tumekuwa na vikao mara kwa mara na baadhi ya wajumbe wa kamati ya wadhamini kujaribu kuangalia tufanye nini ndani ya klabu yetu ya Simba, baada ya kutokea sintofahamu baina ya uongozi na wenye mali na klabu ya Simba,” alisema.

Alisema mbali na kuungana na baraza hilo la wadhamini pia wanachama 71 waliofukuzwa uanachama baada ya kukiuka katiba ya Simba wanapaswa kufuta shauri lao mahakamani ili kuweza kusamehewa.

Wanachama hao 71 walisimamishwa uanachama kwa mujibu wa katiba ya mwaka 2014, baada yakukiuka katiba ya Simba, Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) na Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa), ambayo inasema masuala ya soka hayapaswi kupelekwa mahakamani.

“Tumetafakari kwa kina suala la wanachama hao, hivyo tunawataka waende mahakamani wakafute ile kesi waje sisi kama viongozi wa Simba tutatoa ridhaa ya kushirikiana nao, ili tuweze kusukuma gurudumu hili mbele.

“Tuna imani kabisa walikosea kwa mujibu wa katiba yetu, lakini kibinadamu kuna makosa ya hapa na pale hivyo wakafute ile kesi ili warudi tushirikiane kama zamani,” alisema.

Naye katibu wa baraza hilo la wadhamini, Kilomoni, alisema wamemaliza tofauti zao na uongozi na kukubaliana kuungana.

“Tulikubaliana hili jambo lifikie mwisho, hakuna asiyekosea kwenye dunia hii, kila mtu anakosea na anapokosea kuna msamaha, kwenye maisha lazima mtu uupate, viongozi wametutafuta japo walitusahau kidogo kwa miaka mitatu,” alisema.

Akizungumzia sakata la Mo kupewa timu, alisema walichokubaliana na uongozi ni kutengeneza mustakabali ili kuweza kutambua mabadiliko hayo yatakuwa na faida gani na hasara gani.

“Tumewaambia watuletee maelezo na tukae na wanasheria ili tuangalie hayo mabadiliko, hakuna anayekataa mabadiliko duniani, lakini tuyaangalie yana faida gani na hasara gani,” alisema.

Kilomoni alimaliza kwa kutoa rai kwa viongozi hao kuwa mtu yeyote atakayemilika klabu hiyo, hataruhusiwa kugusa mali za klabu hiyo kama uwanja, jengo na mambo mengine.

“Mali za Simba zimeanza zamani sana, hivyo mtu yeyote anayetaka kumiliki klabu hii basi asiziguse rasilimali hizo kwani mali za klabu ni mali za klabu na uongozi ni uongozi,” alisema.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Usiyoyajua sare ya Leicester, United

NI katika mechi ya Ligi Kuu ya England iliyomalizika kwa sare ya mabaon 2-2.-Man United wamemiliki mpira...

Eti Zidane anapangiwa kikosi!

IMEFICHUKA kuwa wachezaji waandamizi wa Real Madrid walikaa kikao na Zinedine Zidane kumwambia wachezaji anaopaswa kuwapanga na ndiyo maana timu hiyo imeshinda...

DIDA ASAINI IHEFU FC

Golikipa wa zamani wa Yanga na Simba, Deogratius Munishi ‘Dida’ amejiunga na Timu ya Ihefu inayoshiliki Ligi Kuu Tanzania Bara katika kipindi...

JDart Nation wapanga kutawala Africa

CHRISTOPHER MSEKENA MWANAMUZIKI na bosi wa JDart Nation, JDart, amesema miongoni mwa mipango yake kwa mwaka 2021 ni kuhakikisha...

HUJUMA NZITO YANGA

NA WINFRIDA MTOI UONGOZI wa Yanga upo katika harakati za kuhamishia mechi zao zilizobaki za Ligi Kuu Tanzania Bara...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -