Friday, December 4, 2020

WENGER AAMUA KUBAKI ARSENAL

Must Read

HUJUMA NZITO YANGA

NA WINFRIDA MTOI UONGOZI wa Yanga upo katika harakati za kuhamishia mechi zao zilizobaki...

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

LONDON, England

 KWA lugha nyepesi unaweza kusema amewaambia wanaompinga kwamba, wavimbe  hadi wapasuke, baada ya Kocha wa Arsenal, Arsene Wenger, kutangaza dhamira yake ya kuendelea kuinoa klabu hiyo ya Emirates hadi msimu ujao.

Kwa mujibu wa gazeti la Express, Wenger alitangaza dhamira hiyo juzi, ikiwa ni baada ya Jumamosi timu yake kupata  kipigo cha mabao 3-1 dhidi ya West Brom, kwa kusema kuwa  tayari ameshafanya uamuzi juu ya mustakabali wake.

Kocha huyo wa Gunners mkataba wake unafika ukomo mwisho wa msimu huu na presha kubwa imekuwa juu yake, mashabiki wakimtaka kuachia timu.

Mwendo wa vipigo sita katika mechi tisa umeifanya Arsenal kupata anguko kubwa katika historia, huku mashabiki wakipaza sauti na mabango kumtaka Wenger kuachia ngazi.

Upinzani huo dhidi ya Wenger umefanyika kwenye mechi mbili za nyumbani na ugenini ambapo Jumamosi wakati wa mechi dhidi ya West Brom, ndege iliruka juu ya uwanja ikiwa na bango la kumkataa Wenger ang’atuke.

Hata hivyo, gazeti hilo la  Express linaeleza kuwa, mashabiki hao watavunjika moyo kwa sababu inaaminika Wenger ameshakubali kusaini mkataba mpya wa mwaka mmoja kubaki Emirates.

Ripoti inasema kwamba, Wenger amefikia makubaliano na bodi ya Arsenal, ambao awali walimpa mkataba wa miaka miwili.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

HUJUMA NZITO YANGA

NA WINFRIDA MTOI UONGOZI wa Yanga upo katika harakati za kuhamishia mechi zao zilizobaki...

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul 'Ben Pol' ameshukuru mashabiki kwa...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -