Tuesday, October 27, 2020

WENGER ADAI MABAO YA MAN CITY HAYAKUWA HALALI

Must Read

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya...

LONDON, England

KWA kile unachoweza kusema kuwa anadai Man City walibebwa, kocha Arsene Wenger, amedai kuwa mabao waliyofungwa Arsenal juzi kwenye Uwanja wa Etihad, yote yalikuwa ni ya kuotea.

Juzi washika mtutu hao kutoka Kaskazini mwa Jiji la London, walichezea kichapo cha 2-1 yaliyowekwa kimiani na mastaa,  Leroy Sane na Raheem Sterling kipindi cha pili, baada ya Theo Walcott kuipatia Arsenal bao la  mapema kipindi cha kwanza.

Akizungumza na Kituo cha Sky Sport, Wenger alisema hawakuwa na nguvu kipindi cha pili kama walivyokuwa cha kwanza.

“Nadhani hatukuwa na nguvu kipindi cha pili. Kipindi cha kwanza tulikuwa hatari muda wote na wenye kasi, lakini pamoja na yote mwamuzi hakuwa upande wetu,” alisema Mfaransa huyo.

“Mabao yote mawili yalikuwa ya kuotea  na katika mechi ya namna ile, nadhani ilitosha kwa upande wetu. Tumekutana na maamuzi mabaya msimu wote na hasa leo (juzi) nimeyaangalia magoli yote, waliotea,” aliongeza Wenger.

“Goli la pili wamezidi kwa yadi tano. Na la kwanza hali kadhalika. Lakini nini naweza kufanya? Inabidi tukubali matokeo. Tunahitaji kujitathmini wenyewe na kujua ni kwanini tumepoteza mchezo,” aliongeza tena Mfaransa huyo.

Matokeo hayo yanamaanisha Arsenal wanashuka hadi nafasi ya nne kwenye msimamo wa ligi, pointi tisa nyuma ya vinara Chelsea.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika ujumbe kupitia ukurasa wake wa...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya kinda wa zamani wa timu...

Afua Suleiman afunguka ‘Utalijua Jiji’ ilivyompa ustaa mjini

NA JEREMIA ERNEST JINA alilopewa na wazazi wake ni Afua Suleiman na hata alipojitupa kwenye ulimwengu wa muziki wa...

Keche: Kundi maarufu Ghana linalowatamani Diamond, Kiba, Harmonize

JIACHIE na Staa Wako, wiki hii tumetua mpaka Accra, Ghana kwa kundi maarufu la muziki nchini humo, Keche linofanya vizuri na ngoma...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -