Tuesday, January 19, 2021

WENGER AGOMA KUSAJILI TENA

Must Read

Usiyoyajua sare ya Leicester, United

NI katika mechi ya Ligi Kuu ya England iliyomalizika kwa sare ya mabaon 2-2.-Man United wamemiliki mpira...

Eti Zidane anapangiwa kikosi!

IMEFICHUKA kuwa wachezaji waandamizi wa Real Madrid walikaa kikao na Zinedine Zidane kumwambia wachezaji anaopaswa kuwapanga na...

DIDA ASAINI IHEFU FC

Golikipa wa zamani wa Yanga na Simba, Deogratius Munishi ‘Dida’ amejiunga na Timu ya Ihefu inayoshiliki Ligi...

LONDON, England

KWA kile ambacho unaweza kusema ni kama jeuri ama kiburi, Kocha Arsene Wenger ameweka ngumu akisema hana mpango wa kuingia sokoni kusajili wachezaji wengine wakati dirisha dogo la usajili litakapofunguliwa mapema mwezi ujao.

Kauli ya Mfaransa huyo imekuja baada ya taarifa za hivi karibuni kudai kuwa Gunners wataongeza wachezaji wengine ili kukiongezea nguvu kikosi chao, baada ya kupata vipigo viwili mfululizo dhidi ya Everton na Manchester City.

Hata hivyo, pamoja na vipigo hivyo, Wenger anasema kwamba, wala haihitaji damu mpya kutokana na kwamba ana idadi kubwa ya wachezaji ambao wanakaribia kupona majeraha yanayowakabili.

Jeuri hiyo ya Wenger inaonekana kuwa na nguvu zaidi baada ya nyota wake, Danny Welbeck na Aaron Ramsey mwishoni mwa wiki kurejea mazoezini na huku wengine, Alex Oxlade-Chamberlain, Shkodran Mustafi na Per Mertesacker nao wakiwa njiani kurejea mazoezini.

“Ni sawa kurejea kwa wachezaji majeruhi kunaniathiri mimi jinsi ya kuingia katika soko la usajili,” Wenger aliwaambia waandishi wa habari.

“Kwa sababu tuna Lucas Perez, tuna Olivier  Giroud, tuna Alexis Sanchez, tuna Welbeck, Theo Walcott, Oxlade-Chamberlain, nani ambaye anawafikia washambuliaji hawa?” alihoji Mfaransa huyo.

Alisema kwamba, kwa sasa wana uwezo wa kuchagua mchezaji yeyote katika safu ya ushambuliaji, ulinzi na hivyo kwa sasa hawana  haja ya mchezaji yeyote.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Usiyoyajua sare ya Leicester, United

NI katika mechi ya Ligi Kuu ya England iliyomalizika kwa sare ya mabaon 2-2.-Man United wamemiliki mpira...

Eti Zidane anapangiwa kikosi!

IMEFICHUKA kuwa wachezaji waandamizi wa Real Madrid walikaa kikao na Zinedine Zidane kumwambia wachezaji anaopaswa kuwapanga na ndiyo maana timu hiyo imeshinda...

DIDA ASAINI IHEFU FC

Golikipa wa zamani wa Yanga na Simba, Deogratius Munishi ‘Dida’ amejiunga na Timu ya Ihefu inayoshiliki Ligi Kuu Tanzania Bara katika kipindi...

JDart Nation wapanga kutawala Africa

CHRISTOPHER MSEKENA MWANAMUZIKI na bosi wa JDart Nation, JDart, amesema miongoni mwa mipango yake kwa mwaka 2021 ni kuhakikisha...

HUJUMA NZITO YANGA

NA WINFRIDA MTOI UONGOZI wa Yanga upo katika harakati za kuhamishia mechi zao zilizobaki za Ligi Kuu Tanzania Bara...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -