Thursday, December 3, 2020

WENGER AMEAMUA KUONDOKA MWENYEWE

Must Read

HUJUMA NZITO YANGA

NA WINFRIDA MTOI UONGOZI wa Yanga upo katika harakati za kuhamishia mechi zao zilizobaki...

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

LONDON, England

Kocha wa Arsenal, Arsene Wenger, amethibitisha kwamba, amekwisha kufanya maamuzi juu ya hatima yake na atatangaza hivi karibuni.

Baada ya kikosi chake kuchapwa mabao 3-1 dhidi ya West Brom katika mchezo wa Ligi Kuu England, ikiwa ni kipigo cha tano, wakiwa na pengo la pointi sita nje ya ‘top four’, huku zikiwa zimebaki mechi 11 kabla ya ligi kumalizika, Wenger amesema kikosi chake kiko kwenye wakati mbaya.

“Msiwe na wasiwasi, najua cha kufanya kuhusu hatima yangu, hivyo nitatangaza mapema,” alisema Wenger, baada ya kichapo hicho kwenye Uwanja wa Hawthorns.

“Utaona. Leo (juzi) kwasasa sina hofu kuhusiana na hilo. Tuko kwenye hali mbaya ambayo hatukuwahi kuwapo kwa miaka 20. Tunapoteza mechi mfululizo, hilo ndilo jambo muhimu zaidi kuliko hatima yangu.

“Tunapigana vita kubwa na tuko kwenye hali ngumu sana, hakuna namna nyingine zaidi ya kuendelea kupambana na tunapaswa kufanya hivyo hadi mwisho wa msimu.”

Hatima ya Wenger imesababisha mtafaruku na mabango kurushwa angani kwenye Uwanja wa Hawthorns kabla ya mechi kuanza na wakati mechi inaendelea, huku bango la kwanza likimpinga kisha likapita jingine linalomuunga mkono.

Lile la kwanza liliandikwa ‘Hakuna mkataba’ na kumalizia ‘Wenger aondoke’ (No Contract #WengerOut) na la pili liliandikwa ‘Tunamwamini Arsene’ na kumalizia ‘Mheshimu Arsene Wenger’ (In Arsene We Trust #RespectAW).

Kuhusu mabango hayo, Wenger alisema: “Nilikuwa naangalia mechi. Sikuangalia jukwaani. Unatakiwa uangalie kazi yako bila kujali watu wanafikiria nini.”

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

HUJUMA NZITO YANGA

NA WINFRIDA MTOI UONGOZI wa Yanga upo katika harakati za kuhamishia mechi zao zilizobaki...

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul 'Ben Pol' ameshukuru mashabiki kwa...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -