Saturday, January 16, 2021

WENGER AMEINGIA ‘CHAKA’ KUTOA PAUNI MIL 34?

Must Read

Usiyoyajua sare ya Leicester, United

NI katika mechi ya Ligi Kuu ya England iliyomalizika kwa sare ya mabaon 2-2.-Man United wamemiliki mpira...

Eti Zidane anapangiwa kikosi!

IMEFICHUKA kuwa wachezaji waandamizi wa Real Madrid walikaa kikao na Zinedine Zidane kumwambia wachezaji anaopaswa kuwapanga na...

DIDA ASAINI IHEFU FC

Golikipa wa zamani wa Yanga na Simba, Deogratius Munishi ‘Dida’ amejiunga na Timu ya Ihefu inayoshiliki Ligi...

LONDON, England


WAKATI wa dirisha la usajili la majira ya kiangazi, Arsenal waliweka kando utamaduni wao wa ubahili na kumsajili kiungo Granit Xhaka.

Arsenal walitoa pauni milioni 34 kuinasa saini ya Granit Xhaka. Kabla ya hapo, Xhaka alikuwa akiitoa udenda Arsenal kwa muda mrefu na kocha Arsene Wenger alikuwa akijitaja kuwa shabiki mkubwa wa kiungo huyo.

Licha ya uhamisho wake kugharimu kiasi hicho cha fedha, Mswis huyo ameshindwa kufanya kile kilichoitoa Arsenal udenda wakati alipokuwa akikipiga Borussia Monchengladbach.

Xhaka alikuwa sehemu muhimu ya kikosi cha Gladbach kilichomaliza mbio za ubingwa wa Bundesliga kikiwa nafasi ya nne.

Mashabiki wa Arsenal waliamini wamepata jembe hasa kutokana na kiwango alichokionesha kwenye michuano ya Euro 2016 akiwa na Uswisi.

Kinyume na matarajio hayo, Xhaka ameshindwa kujihakikishia namba kwenye kikosi cha kwanza cha kocha Arsenal Wenger.

Xhaka mwenye umri wa miaka 24, ameingia kwenye kikosi cha kwanza mara nane pekee kati ya 19.

Kwa upande mwingine, hata nidhamu yake imekuwa ikimuogopesha mzee Wenger. Bado Wenger anaikumbuka kadi nyekundu aliyopewa mchezaji wake huyo katika mchezo dhidi ya Swansea mwezi uliopita.

Ilikuwa ni mara yake ya nane kukumbana na adhabu hiyo katika kipindi cha miaka mitatu.

“Ni kijana mpole, lakini kuna kipindi huwa maamuzi yake ni makali kidogo. Anatakiwa kulifanyia kazi hilo na kuzuia hasira zake,” alisema Wenger.

Walau Xhaka alionesha uwezo mkubwa katika mchezo wa London derby dhidi ya Tottenham. Katika mtanange huo, nyota huyo hakucheza hata rafu moja.

Xhaka alicheza ‘tackles’ nyingi (tano) na kuliko mchezaji yeyote katika mtanange huo.

“Nilijua ni mchezo ambao ungehusisha nguvu, hivyo nilichagua wachezaji wenye uzoefu na wanaoweza kupambana,” alisema Wenger akimzungumzia Xhaka.

Katika mchezo huo wa Ligi Kuu England uliomalizika kwa sare ya bao 1-1, Xhaka aliwafunika Mousa Dembele na Victor Wanyama waliokuwa kwenye eneo la kiungo.

Katika mchezo dhidi ya Manchester United, licha ya Santi Cazorla kuwa majeruhi, Wenger alimpotezea staa huyo na nafasi hiyo ilichukuliwa na Mohamed Elneny aliyecheza vema na Mfaransa Francis Coquelin.

Arsenal walipokuwa wakicheza na Paris Saint-German juzi katika mtanange wa Ligi ya Mabingwa Ulaya, Wenger alianza na Ramsey na Coquelin katika eneo la kiungo, hivyo bado Xhaka hajaihakikishia nafasi pale Emirates.

Ramsey na Coquelin walionekana kulimiliki vema eneo la kiungo la PSG.

Wachambuzi wa soka wanaamini kuwa mchango wa Xhaka kikosini ni mdogo ukilinganishwa na gharama iliyotumika kumnunua.

Wachezaji wengine ghali pale Emitrates wamekuwa wakionesha makali yao na mfano mzuri ni Mesut Ozil na Alexis Sanchez.

Tofauti na Xhaka, nyota hao wamekuwa moto wa kuotea mbali na wamejihakikishia namba kwenye kikosi cha kwanza cha Gunners.

Mbali na hao, hata beki wa kimataifa wa Ujerumani, Shkodran Mustafi, amekuwa nguzo imara kwenye safu ya ulinzi licha ya ugeni wake kwenye soka la England.

Beki huyo wa kati alinunuliwa kwa ada ya pauni milioni 35 na amecheza michezo yote ya Ligi Kuu England na ile ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Mchezo wake wa kwanza akiwa na Arsenal ulikuwa ni ule waliocheza na Southampton ambapo waliibuka na ushindi wa mabao 2-1.

Kutokana na uwezo wake dimbani, ni ngumu kutabiri kuwa majeruhi Per Mertesacker ataweza kumpokonya namba.

Mwanzoni wengi walitabiri kuwa Xhaka angejituma na kutumia vizuri majeraha ya Cazorla kujihakikishia namba kikosini lakini mpaka sasa hajaonekana kufanya hivyo.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Usiyoyajua sare ya Leicester, United

NI katika mechi ya Ligi Kuu ya England iliyomalizika kwa sare ya mabaon 2-2.-Man United wamemiliki mpira...

Eti Zidane anapangiwa kikosi!

IMEFICHUKA kuwa wachezaji waandamizi wa Real Madrid walikaa kikao na Zinedine Zidane kumwambia wachezaji anaopaswa kuwapanga na ndiyo maana timu hiyo imeshinda...

DIDA ASAINI IHEFU FC

Golikipa wa zamani wa Yanga na Simba, Deogratius Munishi ‘Dida’ amejiunga na Timu ya Ihefu inayoshiliki Ligi Kuu Tanzania Bara katika kipindi...

JDart Nation wapanga kutawala Africa

CHRISTOPHER MSEKENA MWANAMUZIKI na bosi wa JDart Nation, JDart, amesema miongoni mwa mipango yake kwa mwaka 2021 ni kuhakikisha...

HUJUMA NZITO YANGA

NA WINFRIDA MTOI UONGOZI wa Yanga upo katika harakati za kuhamishia mechi zao zilizobaki za Ligi Kuu Tanzania Bara...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -