Thursday, December 3, 2020

WENGER ANAMTAFUTA NINI SANCHEZ?

Must Read

HUJUMA NZITO YANGA

NA WINFRIDA MTOI UONGOZI wa Yanga upo katika harakati za kuhamishia mechi zao zilizobaki...

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

Ana dalili za kumuudhi wikiendi hii

LONDON, England

USIJE ukashangaa kesho Arsene Wenger akamuudhi mshambuliaji wake, Alexis Sanchez.

Tatizo hilo halitakuwa kwenye upande wa mkataba. Hakutakuwa na tatizo la masuala ya nidhamu ndani na nje ya uwanja.

Bali kocha huyo wa Arsenal atamwambia nyota huyo wa Chile kwamba ataachwa kwenye kikosi kitakachocheza Kombe la FA dhidi ya Southampton kesho. Hilo ni jambo la wazi kwamba Sanchez hatalifurahia.

Sanchez anapenda soka na Wenger atakuwa na sababu za msingi kwa uamuzi wake, lakini zitakuwa kama zinaingia masikioni mwa kiziwi.

Ikiwa Sanchez alichukia kwa kutolewa dakika 10 za mwisho mchezo wa Ligi Kuu England, ambao walikuwa wamekwishashinda mabao 4-0 dhidi ya Swansea, sidhani kama atafurahishwa endapo ataambiwa kwamba kesho hatacheza Kombe la FA.

Wenger ataeleza kwamba, ana washambuliaji wawili ambao wanahitaji muda wa kucheza ambao ni Danny Welbeck anayereja kutoka majeruhi baada ya kuumia wakati Lucas Perez anaendelea kuzoea soka la England baada ya kutua kwenye klabu hiyo ya London akitokea Deportivo La Coruna, aliponunuliwa kwa dau la pauni milioni 17 majira ya kiangazi.

Pia kutakuwa na uwezekano wa winga, Theo Walcott, kuwa tayari kucheza, hivyo basi atakuwepo benchi kusubiria nafasi baada ya kupona majeraha yake ya kigimbi cha mguu.

Hizo ni sababu za maana kweli kweli. Sababu ambazo kwenye soka zinakubalika, lakini sababu hata ziwe na mantiki kiasi gani hazina nafasi kwenye akili ya Sanchez.

Hakufurahishwa kukosa mechi ya robo fainali michuano ya EFL ambayo walifungwa na Southampton, Novemba mwaka jana na alichukia pia kuachwa kwenye kikosi kilichocheza mchezo wa Kombe la FA, Januari 7 mwaka huu.

Wenger ana sababu ambazo zinakubalika. Lakini Sanchez huwa hazielewi. Anataka kuhusishwa kwenye timu wakati wote.

Anawaza soka na anataka kucheza, kama Arsenal walivyoamua kumsajili.

Wakati Sanchez anakwenda kupigwa picha za utambulisho wa kutua Arsenal, waliingia kwenye uwanja wa mazoezi London Colney. Wakiwa kwenye uwanja wa ndani eneo hilo la London Colney na shughuli za kupiga picha zikiendelea, Sanchez akiwa na wakala wake na wasaidizi, aliona mpira.

Baada ya kuona mpira alianza kuupiga na kuuchezea, akijaribu staili mbalimbali za kuchezea mpira huo, kitendo ambacho kilichukua dakika 10 akiwa kimya bila ya kuzungumza wala mtu wa kumzungumzisha, huku wafanyakazi wa uwanja wa London Colney wakibakia wameshangaa kwa vitu anavyofanya. Baada ya hapo wakala wake akasema: “Hakuna matata. Pindi Alexis anapoona mpira, hawezi kujizuia.”

Hivyo ndiyo maana anachukia kutolewa uwanjani wakati anataka kucheza na ndio maana atachukia atakapoambiwa kwamba hatacheza mechi ya kesho dhidi ya Southampton. Hamu yake ya kucheza mpira ndiyo sababu inayomfanya Wenger atake kumbakisha Emirates miaka mingi.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

HUJUMA NZITO YANGA

NA WINFRIDA MTOI UONGOZI wa Yanga upo katika harakati za kuhamishia mechi zao zilizobaki...

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul 'Ben Pol' ameshukuru mashabiki kwa...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -