Wednesday, October 21, 2020

Dili la England lampa Wenger kigugumizi

Must Read

Director Kenny: Harmonize alinipeleka WCB nikafanya video ya Lavalava

MWONGOZAJI bora wa video nchini, Kenned Sanga a.k.a Derector Kenny kutoka Zoom Extra, ametua   hapa Jiachie na...

Rogers mwanamuziki anayevutiwa na Marijani

NA JEREMIA ERNEST BONGO Star Search (BSS), ni shindano lililofanikiwa kuibua vipaji vingi vya...

Ihefu, Azam patachimbika Sokoine, Katwila ndani

NA ASHA KIGUNDULATIMU ya Ihefu inatarajia kushuka uwanjani kucheza na Azam ukiwa ni mchezo wa Ligi Kuu...

LONDON, England

ARSENE Wenger yuko tayari kukubali kukinoa kikosi cha timu ya Taifa ya England majira yajayo ya kiangazi.

Mtandao wa Starsport umesema kocha huyo wa Arsenal anavutiwa na kibarua hicho cha kuinoa klabu hiyo kwa ajili ya kujiandaa na fainali za Kombe la Dunia mwaka 2018 nchini Urusi.

Wenger aliweka wazi kwamba anaweza kuwa kocha wa England, baada ya kusema: “Nina mkataba na Arsenal hadi mwakani na siku zote naheshimu mkataba wangu, lakini sijui nitakachofanya baadaye.”

Hivyo ilikuwa wazi kwamba, Wenger hatavunja mkataba wake na Arsenal hadi majira ya kiangazi, hivyo England watasubiri na Gareth Southgate atabakia na kikosi hicho mechi moja zaidi ya nne kama ilivyodaiwa mwanzoni ambapo mechi yake ya mwisho huenda ikawa Machi 26 mwakani dhidi ya Lithuania.

Wakati Chama cha Soka cha England (FA) kinamsubiria Wenger mpaka majira ya kiangazi, kimempa kocha wa timu ya vijana chini ya umri wa miaka 21, Southgate wakimsubiria kocha huyo wa Ufaransa kurithi mikoba ya Roy Hodgson.

Southgate hakuwa kwenye hesabu za kupewa timu hiyo, lakini kocha huyo wa zamani wa Middlesbrough, amekabidhiwa kikosi hicho baada ya Sam Allardyce kuachia nafasi hiyo.

Tayari ameshamchukua kocha msaidizi wa Chelsea, Steve Holland, kwenye benchi la ufundi la kikosi hicho cha England, wakati Sammy Lee na kocha wa makipa, Martyn Margetson, wataendelea na kazi zao.

Lakini hakuna maamuzi yaliyofanywa kwa Craig Shakespeare, kocha aliyechukuliwa kutoka Leicester na Allardyce.

Mtandao huo wa Starsport umesema kwamba kocha huyo mwenye umri wa miaka 66, Wenger, ambaye anasherehekea miaka 20, anamaliza mkataba wake na Gunners mwakani.

Kocha wa Bournemouth, Eddie Howe, amekuwa akipewa nafasi kubwa ya kumrithi Wenger kwenye klabu hiyo ya Gunners.

Klabu hiyo ya Emirates wana mashaka kwamba huenda Wenger akaondoka majira ya kiangazi wakati mkataba wake wa sasa utakapomalizika, hasa kama nafasi ya kuinoa England haitakuwa na mtu.

Inaamini kwamba, England hawataki kumchukua Howe kwa kuwa wanamuona kama kocha ambaye atabeba mikoba ya Wenger kwenye klabu hiyo ya Arsenal.

Kama Wenger atakichukua kikosi hicho kama mmoja wa makocha hodari, kazi yake ya kwanza itakuwa mchezo wa kufuzu Kombe la Dunia dhidi ya Scotland kwenye Uwanja wa Hampden Park, Juni 10 mwakani, kisha atacheza mechi ya pili ya kirafiki dhidi ya nchi yake mwenyewe (Ufaransa) mjini Paris siku tatu baadaye.

Itafuata mechi nyingine ya kufuzu ugenini dhidi ya Malta, kisha nyumbani wakiikaribisha Slovakia na kusafiri hadi Slovenia na Lithuania.

Lakini mwenyekiti wa zamani wa Gunners, Peter Hill-Wood, amesema juzi usiku: “Wazo la Arsene kuwa kocha wa England ni la kipuuzi, kwasababu hatavunja mkataba wake.”

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Director Kenny: Harmonize alinipeleka WCB nikafanya video ya Lavalava

MWONGOZAJI bora wa video nchini, Kenned Sanga a.k.a Derector Kenny kutoka Zoom Extra, ametua   hapa Jiachie na...

Rogers mwanamuziki anayevutiwa na Marijani

NA JEREMIA ERNEST BONGO Star Search (BSS), ni shindano lililofanikiwa kuibua vipaji vingi vya wanamuziki wa Tanzania ambao miongoni...

Ihefu, Azam patachimbika Sokoine, Katwila ndani

NA ASHA KIGUNDULATIMU ya Ihefu inatarajia kushuka uwanjani kucheza na Azam ukiwa ni mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara  (VPL), utakaochezwa leo...

Mugalu atema cheche Simba

NA ASHA KIGUNDULA MSHAMBULIAJI wa Simba, Chris Mugalu, amesema wanakwenda mkoani Rukwa kupambana na kupata ushindi katika mchezo wao...

Malale aitisha Yanga

NA ZAINAB IDDY KOCHA Mkuu wa timu ya Polisi Tanzania, Malale Hamsini, amezisikia sifa za kocha mpya wa Yanga,...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -