LONDON, England
KOCHA Arsene Wenger amewangukia mashabiki wa Arsenal akiwaomba kuwa na umoja, bada ya kufanikiwa kuondoka tena kifua mbele kwenye Uwanja wa Wembley kwa kuwalaza mabingwa wa Ligi Kuu, Chelsea katika mchezo wa Ngao ya Jamii uliopigwa juzi.
Kwa kupata ushindi huo, Gunners watakuwa wamemuonesha kocha Antonio Conte kwamba hana ubavu kwaoa katika michezo ya nyumbani baada ya mchezo wa fainali wa Kombe la FA uliopigwa Mei mwaka huu kumchapa kwa mabao 2-1 na kisha juzi wakamnyuka kwa mikwaju ya penalti 4-1, baada ya muda wa kawaida miamba hao kutoshana nguvu kwa kufungana bao 1-1 ikiwa ni baada ya staa Sead Kolasinac kutokea benchi na kuzawasha lilifungwa na Victor Moses mapema kipindi cha pili.
“Kwa ujumla nafikiri tuna kiwango ambacho ni mwendelezo wa kile tulichokuwa nacho mwishoni mwa msimu uliopita na hicho ndicho natakiwa kukifanyia kazi,” alisema kocha huyo mwenye umri wa miaka 67.
“Kwenye michuano ya Ligi Kuu kila mechi nivita kama yah ii ya leo (juzi), unatakiwa kuwa makini katika hilo kwani unaweza kushinda na hata usipocheza vizuri,”aliongeza Mfaransa huyo.
Alisema kwamba hata hivyo huwa inakuwa vigumu kuwafanya mashabiki wafurahi muda wote, lakini akaahidi kuwa watajituma na kwamba angependa kuona wapo nyuma yao.