Wednesday, November 25, 2020

Wenger azungumza jinsi Ozil alivyoianza kazi mpya

Must Read

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali...

LONDON, England

KIUNGO mbunifu wa klabu ya Arsenal, Mesut Ozil, usiku wa kuamkia jana aliufanya mchezo wa hatua ya makundi Ligi ya Mabingwa Ulaya kuwa mwepesi huku akifunga ‘hat-trick’ yake ya kwanza tangu atue kwenye klabu hiyo na kuisaidia inyakue ushindi wa mabao 6-0 dhidi ya Ludogorets.

Mfalme huyo wa ‘asisti’ ndani ya Arsenal, alibadilika kutoka kuwa mpishi wa mabao hadi mpachikaji akifunga mabao hayo safi yaliyofanikisha kuwamaliza mabingwa hao wa Bulgaria.

Kocha wa ‘The Gunners’ hao, Arsene Wenger, ambaye alimwambia fundi huyo wa Kijerumani kujitahidi katika suala la ufungaji, alisema: “Inaonekana ameanza kuipata ladha ya kufunga mabao kwani ameshatengeneza mabao mengi.

“Kabla ya hapo, alikuwa ni mtu wa kutengeneza nafasi. Nataka awe mtoa pasi na mfungaji na taratibu anaanza kufanya vizuri,” alisema.

Lakini Wenger pia alimmwagia sifa mlinda mlango wake, David Ospina kwa kuiokoa timu yake ilipokuwa ikishambuliwa mara baada ya Alexis Sanchez kufungua akaunti ya mabao.

Ludogorets walilisakama lango la Arsenal kwa kutumia uwezo wao wote kabla ya mabao kutoka kwa Theo Walcott na Alex Oxlade-Chamberlain, katika vipindi vyote vya mchezo huo kuituliza presha yao.

Wenger, ambaye vijana wake wamefanikiwa kushinda michezo saba mfululizo katika michuano yote, alisema: “Katika kipindi cha kwanza, mchezo ulionekana kuwa tofauti kwani walionekana kuwa hatari kila waliposogea kwetu.

“Tulifunga haraka na labda tuliumaliza mchezo mapema kidogo.

“Ningependa kumpongeza Ospina aliyetuokoa mara mbili kutoka kwenye hatari.

“Ni ngumu kuelezea lakini muhimu ni kuwa tunafunga mabao mengi. Tuna michezo migumu kwahiyo lazima tutumie nafasi tuzipatazo,” alisema.

Kutokana na matokeo hayo, Arsenal inaongoza kundi A lakini wakilingana na Paris Saint-Germain, ambao walikutana kwenye mchezo wao wa kundi hilo mapema mwezi wa tisa.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...

Sarpong ‘aua’ shabiki Simba

Na MWANDISHI WETU, MWANZA BAO la dakika ya 29 lililofungwa na Michael Sarpong wa Yanga juzi, limesababisha kifo cha...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -