Saturday, November 28, 2020

WENGER, SANCHEZ AU OZIL NANI MUHIMU KUBAKI ARSENAL?

Must Read

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali...

London, England

Kumekuwa na utata mkubwa kwa mashabiki wa Arsenal juu ya nani abaki kwenye kikosi hicho, kati ya kocha Arsene Wenger na nyota wawili, Alexis Sanchez au Mesut Ozil ambao wanataka kuongezewa mkataba mpya na mshahara mnono.

Hiyo inatokana na mwenendo mbaya wa klabu hiyo kwa kipindi hiki, pamoja na sakata hilo la kuongezwa mikataba mipya kwa wachezaji hao.

Lakini mkongwe wa Arsenal, Robert Pires, amemaliza utata wa nani muhimu kwenye kikosi hicho cha Gunners.

Pires amesema, Arsene Wenger kusaini mkataba mpya ni muhimu sana kuliko Sanchez au Ozil kuongeza mikataba yao kwenye klabu hiyo ya Emirates.

Mpaka sasa kuna tetesi kwamba Wenger amesaini mkataba mpya, lakini hakuna taarifa rasmi za kwamba tayari amesaini mkataba huo ingawa tetesi hizo zilidai klabu inasubiri kupata muda mzuri wa kutangaza.

Lakini kabla ya kuibuka kwa tetesi hizo za Wenger kudaiwa kusaini mkataba mpya kwenye klabu hiyo ya Emirates, aliwahi kuweka wazi kwamba hataachana na soka.

Ingawa bado mashabiki wanaendelea kumpinga na mabango ya kumtaka kocha huyo mwenye umri wa miaka 67 aondoke (Wenger Out), wakitumia ndege iliyorushwa kwenye Uwanja wa Hawthorns, kabla ya kikosi hicho kuchapwa mabao 3-1 katika mechi ya Ligi Kuu England wiki iliyopita.

Hata hivyo, Pires ambaye alikuwa mchezaji muhimu kwenye kikosi kilichomaliza msimu bila ya kufungwa (Invincibles) msimu wa 2003/04, anafikiri kwamba kuna umuhimu mkubwa zaidi kwa Arsenal kumpa mkataba mpya Wenger kuliko Sanchez au Ozil.

“Nafikiri kwa Sanchez na Ozil wataongeza mkataba mipya. Makubaliano ya masuala ya mkataba si mambo rahisi, yanachanganya,” alisema Pires.

“Lakini jambo muhimu ni kumwona Arsene Wenger akiongeza mkataba mpya. Arsene Wenger ni muhimu, muhimu sana kwa Arsenal kwa sasa na msimu ujao.

“Namwamini Arsene Wenger. Kwangu mimi kilikuwa kitu cha kipekee kufanya naye kazi kwa misimu sita. Hakuwa mkamilifu lakini alikuwa mzuri, tulinyakua mataji.”

Pires si mchezaji pekee wa kikosi hicho cha ‘Invincibles’ kumtaka Wenger kubaki.

Aliyekuwa mlinda mlango wa kikosi hicho, Jens Lehman, alitoa mawazo yake akizungumza na talkSPORT, akisema: “Ni ngumu sana kuziba nafasi ya mtu mwenye akili, wote tunajua kwamba ni mtu mwenye akili sana na bado yuko vizuri. Kwa yale aliyofanya kwenye klabu, nafikiri anastahili kubaki na si kuondoka kwenye kipindi cha matokeo mabaya.”

Naye beki aliyekuwamo kwenye kikosi hicho cha ‘Invincibles’, Sol Campbell, alimwelezea Wenger kama mtu mwenye maono anayestahili miaka mingine miwili kwenye klabu ambayo amefanya kazi kubwa kuibadilisha.

“Nafikiri atatafakari juu ya hilo, ana mkataba wa miaka miwili mezani kwake. Nafikiri mwisho wa siku atasaini,” alisema beki huyo wa zamani wa England mwanzoni mwa mwezi huu.

“Kile alichofanya kwenye klabu, jinsi alivyoiongoza klabu hiyo kutoka Highbury kwenda kwenye uwanja mpya wa Emirates, pamoja na uwanja wa mazoezi. Ni wazi kwamba kwa sasa kuna klabu zina viwanja bab kubwa, lakini ana maono sana kwani uwanja ulijengwa kwa mawazo yake, yeye ndio aliubuni.”

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...

Sarpong ‘aua’ shabiki Simba

Na MWANDISHI WETU, MWANZA BAO la dakika ya 29 lililofungwa na Michael Sarpong wa Yanga juzi, limesababisha kifo cha...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -