Thursday, October 22, 2020

WEWE NI MWANAMKE WA NAMNA GANI KWA MWENZAKO

Must Read

Director Kenny: Harmonize alinipeleka WCB nikafanya video ya Lavalava

MWONGOZAJI bora wa video nchini, Kenned Sanga a.k.a Derector Kenny kutoka Zoom Extra, ametua   hapa Jiachie na...

Rogers mwanamuziki anayevutiwa na Marijani

NA JEREMIA ERNEST BONGO Star Search (BSS), ni shindano lililofanikiwa kuibua vipaji vingi vya...

Ihefu, Azam patachimbika Sokoine, Katwila ndani

NA ASHA KIGUNDULATIMU ya Ihefu inatarajia kushuka uwanjani kucheza na Azam ukiwa ni mchezo wa Ligi Kuu...

KUNA tofauti kati ya mwanamke na mwanamke makini linapokuja suala la uamuzi katika mambo ya mahusiano. Mwanamke tu, kwa maana  ya jinsia, yeye anaweza kutaka mwanaume mtanashati ama mwenye pesa ili awe mwandani wake.

Ila Mwanamke makini yeye huwa na vigezo tofauti. Kwake linapokuja suala la mahusiano akili na hisia zake humuongoza kumpata mtu sahihi wa maisha yake.

Mara nyingi nimewahi kusikia wanaume wakilalamika juu ya aina ya wanawake waliokuwa nao. Wanasema wanawake wao hata kabla ya ndoa wamegeuka kuwa mizigo mizito katika maisha yao kwa sababu ya mahitaji ya hovyo na tabia zao.

Mwanamke unakuta kila fasheni ya nguo anataka awe nayo, kila onesho la muziki anataka kuhudhuria. Huyu ni mwanamke mzigo kwa mawanaume makini.

Ikumbukwe, linapokuja suala la uhusiano wanaume hutofautiana sana. Mwanaume ambaye yupo kwa ajili ya kustarehe tu na mwanamke bila kuhitaji kuishi naye katika maisha makini ya ndoa, huenda asipende mwanamke mtulivu na mwenye kukwepa starehe.

Wao wanapenda sana wanawake micharuko kidogo, wenye kujua viwanja na pombe zote za mjini. Mwanaume mpenda starehe asiye na mpango mirefu na mwanamke, kuwa na binti wa aina hii kwake huwa ni furaha na raha sana.

Ila kuna kundi la wanaume wengine. Wao muda mwingi wanapokuwa na wapenzi wao huzungumzia namna ya kutengeneza nao familia ya furaha, heshima na maadili. Mara nyingi hutumia muda wao kukanyana na kutakiana kila la kheri katika matendo na maamuzi yao. Kwa mwanamke mjinga, mwenye pupa ya maamuzi, mwanaume huyu anaweza kumuita mkoloni kisa tu anamkataza kwenda club ama kujumuika na kundi la marafiki wa hovyo.

Nimeona wanawake wengi wakiachana na watu wa aina hii na kukimbilia kwa wanaume ambao watawapa nafasi ya kufanya chochote wanachojisikia kufanya. Kitu wasichojua ni kuwa wale wenye kujidai kutoa uhuru mpana huwa sio watu makini katika maisha yao ndiyo maana hawajali hata wakiona wahusika wakipotea. Wewe binti,  mwanaume wako yuko vipi? Umemsoma na kugundua ana malengo gani na wewe?

Sio vema mwanaume kumbana sana mpenzi wake katika mahusiano, ila ni vema mwanaume akamwelekeza mpenzi wake mipaka ya matendo, marafiki na hata maneno yake. Kufanya hivi maana yake muhusika anataka kumfanya mwanamke wake atoshe katika vigezo vyake na asitamani mwanamke mwingine.

Wanawake wengi wanakosea kuwa viburi kwa watu wao pindi wanaporekebishwa. Kitendo hiki kinakuja kuwagharimu baadaye kwa sababu wahusika baada ya kuona wanawarekebisha wakina fulani na wao hawaelekei basi huamua kupeleka macho kwa wengine wenye kuonekana  kukubaliana na misimamo yao ya kimaisha. Baadaye unakuta mwanamke kutoka katika mahusinao haya anasema wanaume wabaya,  eti alimuahidi kumuoa na sasa kamkimbia?

Ndiyo alikupenda na hata kukuahidi kukuoa. Ila atakuoa vipi ikiwa alisema hataki uwe na kundi la marafiki wa hovyo na wewe hukusikia? Atakuoa vipi ikiwa alikwambia aina ya mavazi unayovaa

yanamvunjia heshima na ni kinyume na msimamo wake wa kiimani ila wewe hukusikia? Mara nyingi wanawake wanalalamika bila kujua chanzo cha mateso yao katika mahusiano yamezalishwa na wao.

Ili mwanamke umfanye mwanaume wako akufikirie kila muda  na kutamani kukuoa inabidi umfanye ajihisi maalum kwa matendo na maneno yako. Inabidi utekeleze mengi ya matakwa yake ili asipatwe na tamaa ya kwenda nje.

Kuna binti mmoja alikuwa na mpenzi ambaye anapenda sana wanawake wenye kujisitiri. Mpenzi wake huyo alipomwambia kuwa na yeye abadilike kimavazi, kutoka katika mavazi ya ‘kimjini mjini’ mpaka katika mavazi ya staha na heshima alikataa kwa kusema kuwa yeye amezoea hivyo na amekulia katika mavazi hayo.

Mwaka mmoja baadaye, mwanaume wake akabadilika tabia. Badala ya kuwa anamsisitizia avae mavazi ya kujisiti akawa anamwamcha tu.

Mara akawa pia hamtafuti tena kwenye simu. Mwezi uliopita yule binti alipatwa na mshtuko na kuzimia baada ya kusikia yule mwanaume wake ameoa kimya kimya binti fulani mpole kutoka Tabora, mwenye kujisitiri na Mcha Mungu. Kuw amakini.

ramadhanimasenga@yahoo

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Director Kenny: Harmonize alinipeleka WCB nikafanya video ya Lavalava

MWONGOZAJI bora wa video nchini, Kenned Sanga a.k.a Derector Kenny kutoka Zoom Extra, ametua   hapa Jiachie na...

Rogers mwanamuziki anayevutiwa na Marijani

NA JEREMIA ERNEST BONGO Star Search (BSS), ni shindano lililofanikiwa kuibua vipaji vingi vya wanamuziki wa Tanzania ambao miongoni...

Ihefu, Azam patachimbika Sokoine, Katwila ndani

NA ASHA KIGUNDULATIMU ya Ihefu inatarajia kushuka uwanjani kucheza na Azam ukiwa ni mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara  (VPL), utakaochezwa leo...

Mugalu atema cheche Simba

NA ASHA KIGUNDULA MSHAMBULIAJI wa Simba, Chris Mugalu, amesema wanakwenda mkoani Rukwa kupambana na kupata ushindi katika mchezo wao...

Malale aitisha Yanga

NA ZAINAB IDDY KOCHA Mkuu wa timu ya Polisi Tanzania, Malale Hamsini, amezisikia sifa za kocha mpya wa Yanga,...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -