Saturday, October 31, 2020

WHOZU:NILIMWAMBIA GIGY MONEY AKICHANA ATANOGA ZAIDI

Must Read

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya...

NA CHRISTOPHER MSEKENA


KARIBU msomaji wa safu hii ya Jiachie na Staa Wako inayokupa nafasi ya kuwa karibu na watu maarufu uwapendao kwa kuwauliza maswali na wao wanayajibu hapa hapa.

Leo tupo Oscar Lole maarufu kama Whozu ambaye ni msanii wa muziki na ucheshi anayefanya vizuri na nyimbo kama Follow Unfollow, Gonga, Tunavesha na hivi sasa ngoma yake Huendi Mbinguni imekuwa miongoni mwa nyimbo 10 zinazovuma katika mtandao wa YouTube, karibu.

SWALI: Jamal Seif wa Bukoba anauliza ulianza vipi kuchekesha na kufanya muziki kwa wakati mmoja?

Whozu: Komedi ilikuja kama zari tu, mimi nilikuwa siyo mchekeshaji nilianza kama masihara kwenye mtandao wa Instagram, nilifanya video nyingi ila baada ya kuigiza video ya Rockonolo  aliyoshirikishwa Diamond, mastaa wengine wakaanza kunitafuta nichekeshe kwenye video zao.

Na muziki nilianza zamani mpaka nilipoingia Chuo cha Ushirika Moshi, nilikuwa nafanya nyimbo namsikilizisha Nikk wa Pili, ananiambia siwezi, akawa ananiambia nijifunze muziki kwa miaka mitatu, nilichoka ila sasa najua kwanini aliniambia vile, akawa ananipa nyimbo za wasanii ili niwasikilize hatimaye leo ninatoa nyimbo kali.

SWALI: Salehe Muhina wa Njombe anauliza kwanini unajiita Whozu?

Whozu: Kwa sababu mimi ni mtu ambaye sitabiriki, siyo mwoga, naamini katika kile ninachokifanya, nipo sekta zote, naweza kuimba, kuchekesha, kurap nk.

SWALI:Khadija Monge wa Tanzania anasema anapenda wimbo wako Huwendi Mbinguni, anasema wazo na wimbo huo ulilitoa wapi?

Whozu: Mara nyingi nyimbo zangu huwa ni maisha ambayo nnayaishi au niliwahi kuishi, nakumbuka nikiwa mdogo mama alikuwa ananitishia kuwa sitaenda mbinguni  kama nitachelewa kwenda jumuiya, hapo ndiyo aidia ilipokuja mimi nikachukua yale makosa madogo madogo nikayaweka kwenye wimbo.

SWALI: Ernest Kitoze wa Bagamoyo anauliza Whozu ni nani?

Whozu: Mimi ni kijana wa kitanzania, nimezaliwa na kukulia Moshi, masomo pia nimesoma huko na baada ya masomo ndiyo nikaingia kwenye muziki nikianza kama mchekeshaji kupitia video za wasanii wakubwa sasa hivi nipo Dar es Salaam nafanya muziki.

SWALI: Rehema Mustafa wa Vingunguti anauliza kwanini hubadilishi mtindo wako wa nywele?

Whozu: Napenda kuwa tofauti hapa Bongo ni mimi tu nina mabutu, ni staili ambayo inanipendeza kwa hiyo akitokea mtu mwingine mwenye mabuntu atakuwa ananiinga, hii ni ‘brand’ yangu imenitambulisha.

SWALI: Emmanuel Essau wa Bugando Mwanza anauliza warembo ambao huwa wanaonekana kwenye video zako huwa unawalipa bei gani?

Whozu: Mimi nuna watu ambao wamenizunguka ambao naishi nao vizuri, hata mavideo vixen ambao wanaonekana kwenye video zangu huwa nawalipa lakini tunalipana kindugu.

SWALI: Kwanini tasnia ya uchekeshaji haina mvuto sana kipindi hiki?

Whozu: Komedi zimegawanyika mfano Idris Sultan huwezi mfananisha na uchekeshaji wa Mkali Wenu, mimi nilichofanya ni kitu ambacho hakuna mchekeshaji Bongo alikuwa anafanya, mimi nilikuwa nachekesha kupitia nyimbo.

SWALI: Raynhard Msigwa wa Iringa anauliza ilikuwaje ukafanya kazi na Gigy Money?

Whozu: Mara nyingi huwa napenda kufanya vitu tofauti, Gigy Money nilikutana naye studio  akiwa anarekodi nyimbo zake, nikamwambia akichana atanoga zaidi, na yeye mwenyewe akakubali, akanipa aidia ya Kiki ni Gigy mimi nikamwandikia na ninashukuru wimbo umepokewa vizuri.

SWALI: Shaibu Konde wa Mbezi Kimara anauliza malengo yako ni yapi kwenye muziki?

Whozu: Unapofanya kitu lazima uwe na malengo, muziki ni biashara kama biashara zingine, mimi nachukulia kama kazi, nataka mafanikio zaidi na siyo umaarufu bila hela, naomba mashabiki waendelee kunisapoti.

Wiki ijayo tutakuwa na mchoraji wa katuni Noah Yongolo aliyewahi kuvuma na katuni maarufu za Sunche na Kapeto, tuma swali lako kwake kupitia namba hapo juu, meseji tu.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika ujumbe kupitia ukurasa wake wa...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya kinda wa zamani wa timu...

Afua Suleiman afunguka ‘Utalijua Jiji’ ilivyompa ustaa mjini

NA JEREMIA ERNEST JINA alilopewa na wazazi wake ni Afua Suleiman na hata alipojitupa kwenye ulimwengu wa muziki wa...

Keche: Kundi maarufu Ghana linalowatamani Diamond, Kiba, Harmonize

JIACHIE na Staa Wako, wiki hii tumetua mpaka Accra, Ghana kwa kundi maarufu la muziki nchini humo, Keche linofanya vizuri na ngoma...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -