Wednesday, October 28, 2020

WILLIAN: NITACHEZA CHELSEA MSIMU UJAO

Must Read

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya...

LONDON, England


 

WINGA wa timu ya Chelsea, Willian, amethibitisha kwamba, ataendelea kucheza soka katika viunga vya Stamford Bridge, akisema amekuwa na furaha wakati wote ndani ya klabu hiyo.

Willian mwenye umri wa miaka 29, ametikisa miamba kadhaa ya soka Ulaya katika dirisha la usajili wa majira haya ya kiangazi, zikiwemo Barcelona na Manchester United.

Inakumbukwa kuwa Barca ilipeleka ofa tatu kwa Chelsea kwa ajili ya kumsajili Willian, lakini zote ziliwekwa kapuni na pia ni mchezaji anayetakiwa na kocha wa Man Utd, Jose Mourinho.

Tetesi za Willian ziliibuka baada ya uhusiano na kocha wake wa zamani wa Chelsea, Antonio Conte, kuvurugika lakini alithibitisha kwamba, ameshazungumza na kocha mpya, Maurizio Sarri na kumwambia anataka kumtumikia msimu ujao.

“Nimeshaliweka wazi hili mara kadhaa kwamba kuichezea Chelsea ni jambo zuri kwangu, najisikia furaha wakati wote.

“Sijawahi kusema nataka niondoke hapa,” alisema Willian mara baada ya mchezo wa Ngao ya Jamii ambao Chelsea walichapwa mabao 2-0 na Man City.

“Nimezungumza vizuri sana na Sarri, nina imani tutafanya kazi nzuri msimu ujao. Mwanzo ni mgumu ila kikubwa ni kushirikiana ili kuimarika zaidi,” alisema.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika ujumbe kupitia ukurasa wake wa...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya kinda wa zamani wa timu...

Afua Suleiman afunguka ‘Utalijua Jiji’ ilivyompa ustaa mjini

NA JEREMIA ERNEST JINA alilopewa na wazazi wake ni Afua Suleiman na hata alipojitupa kwenye ulimwengu wa muziki wa...

Keche: Kundi maarufu Ghana linalowatamani Diamond, Kiba, Harmonize

JIACHIE na Staa Wako, wiki hii tumetua mpaka Accra, Ghana kwa kundi maarufu la muziki nchini humo, Keche linofanya vizuri na ngoma...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -