Monday, January 18, 2021

WINNIE CUTE Mrembo wa Singida aliyetekwa na Diamond

Must Read

Usiyoyajua sare ya Leicester, United

NI katika mechi ya Ligi Kuu ya England iliyomalizika kwa sare ya mabaon 2-2.-Man United wamemiliki mpira...

Eti Zidane anapangiwa kikosi!

IMEFICHUKA kuwa wachezaji waandamizi wa Real Madrid walikaa kikao na Zinedine Zidane kumwambia wachezaji anaopaswa kuwapanga na...

DIDA ASAINI IHEFU FC

Golikipa wa zamani wa Yanga na Simba, Deogratius Munishi ‘Dida’ amejiunga na Timu ya Ihefu inayoshiliki Ligi...

NA MICHAEL MAURUS,

UKIKUTANA naye kwa mara ya kwanza, unaweza kudhani ni mmoja wa washiriki wa mashindano ya urembo nchini ya Miss Tanzania kutokana na umbo lake.

Ni binti mwenye mvuto wa aina yake, akiwa na tabasamu la hali ya juu, mcheshi na mzungumzaji pale inapobidi kufanya hivyo.

Kwa mara ya kwanza kuonana naye, ni pale alipofika katika ofisi za gazeti hili la BINGWA pamoja na magazeti dada, Dimba, Mtanzania na Rai, zilizopo Sinza Kijiweni, Dar es Salaam.

Mara baada ya kumwona nikiwa kama mmoja wa wadau wa mashindano ya urembo, nilidhani ni mshiriki wa mashindano ya Miss Tanzania mwaka huu ambayo fainali zake zinatarajiwa kufanyika jijini Mwanza mwishoni mwa wiki hii.

Lakini nilipomsogelea na kumsabahi, nilibaini haikuwa hivyo bali ni msanii wa muziki wa kizazi kipya ambaye ndio kwanza amejitosa katika fani hiyo inayotajwa kuwa ngumu mno kwa sasa.

Huyo si mwingine bali ni binti kutoka mkoani Singida anayefahamika kwa jina la Winfrida Joseph, ambaye anapenda kujitambulisha kwa jina la usanii la Winnie Cute.

Kutokana na mwonekano wake, nilivutika kufanya naye mahojiano juu ya uamuzi wake wa kujitosa katika muziki ambapo anasema kuwa hilo limetokana na mambo mbalimbali, zaidi ikiwa ni kwa kuwa na kipaji na fani hiyo.

Anasema amekuwa akipenda muziki tangu akiwa mdogo ambapo akiwa shule, alikuwa akiimba nyimbo za wanamuziki mbalimbali, kuanzia wa hapa nchini na kwingineko.

“Nikiwa mdogo nilikuwa nikipenda sana muziki, nilikuwa nikiimba nyimbo za wasanii mbalimbali, huku nikicheza… nilipoanza shule nilizidi kuvutika katika muziki baada ya kujiunga na kwaya ya shule na kuimba katika matukio mbalimbali,” anasema binti huyo mrefu kiasi na mwenye vigezo vya kuwa mmoja wa washiriki waliopo katika kambi ya Miss Tanzania 2016 huko Mwanza.

Winnie Cute anasema pamoja na kuwa na kipaji, kuna wasanii waliochangia kwa kiasi kikubwa kujitosa katika muziki, zaidi akiwa ni mwanadada, Hellen George ‘Rubby’.

Lakini mbali ya Rubby, Winnie Cute, anasema amekuwa akipagawishwa mno na Naseeb Abdul ‘Diamond Platnumz’ kutokana na umahiri wake katika muziki, zaidi ikiwa ni jinsi alivyopambana hadi kufikia mafanikio aliyonayo kwa sasa.

“Hakuna msanii wa muziki anayenivutia zaidi kama Diamond, yule kaka ninamhusudu sana, hana maringo, ana upendo na ni mwenye huruma kwa wengine,” anasema Winnie Cute.

Binti huyo anasema pamoja na Diamond kupitia katika wakati mgumu tangu akiwa mdogo hadi alipoanza maisha ya muziki, bado hajaona shida kusaidia wengine kutimiza ndoto zao.

“Ingekuwa ni msanii mwingine, asingethubutu kusaidia wengine, kwani amepitia katika mazingira magumu na ya kukatisha tama, fikiria mtu anahaha kutafuta fedha za kurekodia hadi anauza kitu chake cha thamani, hali mara baada ya kutoka, anakumbuka kuwasaidia wengine, ni wachache sana wanaoweza kufanya hivyo.

“Ndio maana nampenda sana Diamond, Mungu azidi kumwongezea afike mbali zaidi ili aweze kuwasaidia wengine kama anavyofanya kwa sasa japo yeye hakupata msaada wakati anajitosa katika muziki,” anasisitiza.

Alipoulizwa iwapo angetamani kufanya kazi na Diamond, Winnie Cute anasema: “Siku hiyo ikitokea, sitapata hata usingizi, nitatamani kukuche haraka siku ifike kwani ninampenda sana Diamond na ninatamani kufikia mafanikio yake.”

Katika kuonyesha jinsi alivyopania kufika mbali katika muziki, hasa kutokana na kuvutwa na mafanikio ya Diamond, lakini pia Rubby, tayari Winnie Cute ameingia studio na kutoka na wimbo unaokwenda kwa jina la Nina Hofu ya Pendo Lako.

Juu ya wimbo huo, mrembo huyo aliyezaliwa katika Mji wa Unyankindi, Singida, anasema wimbo huo amemshirikisha msanii wa muda mrefu, Sam wa Ukweli.

Wimbo huo umeelezea jinsi mtu fulani alivyo na hofu juu ya penzi la mwenza wake hivyo kutaka kuwekwa wazi iwapo anapendwa au la.

Sehemu ya mashairi ya wimbo huo, yanakwenda hivi: “Nina hofu ya upendo wako, unasema mimi ni wako lakini mbona hutumi picha zangu kwenye kurasa zako za twitter na instagram?”

“Huo ndio wimbo wangu wa kwanza na ninaamini utanitambulisha vizuri tu kwani tayari umeshaanza kuchezwa katika vituo mbalimbali vya redio na ninashukuru kila redio ninayokwenda ninapewa ushirikiano na sibaniwi kama baadhi ya wasanii wanavyolalamika,” anasema.

Winnie Cute anasema kwa sasa ameingia msituni ili kutoa wimbo mwingine ambao anaamini utakuwa bomba zaidi kwani amejifunza mengi kupitia kazi yake ya kwanza.

“Ninawaomba mashabiki wanipokee nami ninawaahidi kutowaangusha, nitafanya kazi kwa uwezo wangu na kipaji changu chote,” anasema.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Usiyoyajua sare ya Leicester, United

NI katika mechi ya Ligi Kuu ya England iliyomalizika kwa sare ya mabaon 2-2.-Man United wamemiliki mpira...

Eti Zidane anapangiwa kikosi!

IMEFICHUKA kuwa wachezaji waandamizi wa Real Madrid walikaa kikao na Zinedine Zidane kumwambia wachezaji anaopaswa kuwapanga na ndiyo maana timu hiyo imeshinda...

DIDA ASAINI IHEFU FC

Golikipa wa zamani wa Yanga na Simba, Deogratius Munishi ‘Dida’ amejiunga na Timu ya Ihefu inayoshiliki Ligi Kuu Tanzania Bara katika kipindi...

JDart Nation wapanga kutawala Africa

CHRISTOPHER MSEKENA MWANAMUZIKI na bosi wa JDart Nation, JDart, amesema miongoni mwa mipango yake kwa mwaka 2021 ni kuhakikisha...

HUJUMA NZITO YANGA

NA WINFRIDA MTOI UONGOZI wa Yanga upo katika harakati za kuhamishia mechi zao zilizobaki za Ligi Kuu Tanzania Bara...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -