Tuesday, November 24, 2020

WORLD CUP 2018… VIGOGO WALIVYOTUMBUANA KUSAKA NAFASI KWENDA URUSI

Must Read

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali...

AMSTERDAM, Uholanzi

MATUMAINI ya Uholanzi kupata nafasi ya kushiriki fainali za Kombe Dunia nchini Urusi mwakani, yameingia dosari wakati vigogo hao waliowahi kushika nafasi ya tatu fainali zilizopita kuchapwa mabao 2-0 dhidi ya Bulgaria.

Mabao hayo ya Bulgaria yaliyoiua Uholanzi kwa kuichapa mabao mawili ndani ya dakika 20, yote yakifungwa na Spas Delev.

Delev alitumia makosa ya chipukizi wa miaka 17, Matthijs De Ligt, ambaye ni mchezaji mdogo kuwahi kuanza kwenye kikosi hicho tangu mwaka 1931 ambaye alikosea pasi na kusababisha mshambuliaji huyo kupachika bao kiulaini na mpira kumshinda mlinda mlango Jeroen Zoet. Delev alifanya matokeo kuwa mabao 2-0 kwa shuti la mguu wa kulia.

Uholanzi walitawala mchezo huo kwa asilimia kubwa, lakini waliangushwa na safu ya ulinzi ya Bulgarian na mlinda mlango Nikolay Mihaylov, aliokoa bao la wazi la Davy Klaassen na kichwa na Bas Dost katika kipindi cha pili.

Kipigo hicho kimeiacha Uholanzi ikiwa na pointi sita nyuma ya vinara wa Kundi A, Ufaransa, ambao waliichapa Luxembourg mabao 3-1 na kushika nafasi ya nne, pointi tatu nyuma ya Sweden na pointi mbili mbele ya Bulgaria wakati mshindi wa kundi anajihakikishia nafasi ya kwenda Urusi mwaka 2018.

Ufaransa ambao ni mabingwa wa fainali hizo za dunia mwaka 1998 na michuano ya Euro 2016, walishika nafasi ya pili, walimshuhudia mshambuliaji Olivier Giroud akifunga bao la kwanza mjini Luxembourg dakika chache kabla ya mapumziko.

Luxembourg walisawazisha dakika ya 34 kwa penalti ya Aurelien Joachim, likiwa ni bao la kwanza dhidi ya Ufransa tangu miaka 39 iliyopita.

Lakini furaha yao haikudumu baada ya mshambuliaji wa Atletico Madrid, Antoine Griezmann, kuifungia Ufaransa bao la kuongoza, naye pia alifunga kwa penalti dakika nne baadaye.

Nyota wa Arsenal, Giroud, aliongeza bao la tatu dakika ya 77 baada ya kupigiwa krosi nzuri na Benjamin Mendy na kuunganisha kwa kichwa.

“Akiwa na sisi, Olivier mara zote anafunga hata kama akiwa anashindwa kwenye klabu yake. Tumempigia krosi za kutosha na yeye ameonyesha uwezo wake,” alisema kocha wa Ufaransa, Didier Deschamps.

Mechi nyingine, ilikuwa ni Ureno dhidi ya Hungary, ambapo Cristiano Ronaldo alitingisha nyavu mara mbili na kufikisha mabao 70 aliyoifungia timu yake ya taifa, wakati mabingwa hao wa mataifa ya Ulaya, Ureno wakiichapa Hungary 3-0 na kukaa nafasi ya pili nyuma ya Uswisi wanaongoza Kundi B.

Katika mchezo huo mjini Lisbon, Ureno waliichapa Hungary, timu ambayo kwenye michuano ya Euro 2016 walitoka sare ya 3-3.

Ushindi huo unaifanya Ureno kushika nafasi ya pili kwenye Kundi B, pointi tatu nyuma ya Uswisi, ambao walijiwekea rekodi ya kushinda mechi tano kati ya tano ukiwamo ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Latvia.

Mshambuliaji wa Porto, Andre Silva, alifunga bao la kuongoza dakika ya 30, akiunganisha pasi kutoka kwa Raphael Guerreiro likiwa ni bao lake la tano katika mechi sita akichezea Ureno.

Dakika sita baadaye, nahodha wa Ureno, Ronaldo alifunga mabao mawili moja kwa mguu wa kushoto, baadaye aliongeza bao la tatu dakika ya 65 kwa mpira wa adhabu na kufikisha bao hizo 70.

Ubelgiji walihitaji bao la dakika za mwisho la Romelu Lukaku kuambulia sare ya bao 1-1 dhidi ya wachezaji tisa wa Ugiriki na kukaa kileleni mwa Kundi H wakiwa na pointi mbili.

Wakicheza bila ya Eden Hazard ambaye alikuwa na majeraha, Ubelgiji walikosa mtengenezaji nafasi za mabao mjini Brussels, ambapo Ugiriki walipata bao la kuongoza sekunde ya 20 lililofungwa na mshambuliaji wa Benfica, Kostas Mitroglou akipiga shuti la mbali, likiwa ni bao lake la tatu kwenye mechi hizo za kufuzu.

Ugiriki walipungua na kuwa wachezaji 10 baada ya 65, Panagiotis Tachtsidis kuonyeshwa kadi nyekundu kwa kumchezea vibaya beki Toby Alderweireld.

Nyota wa Everton, Lukaku aliisawazishia Ubelgiji dakika ya 89, kabla ya Georgios Tzavelas kutolewa kwa kadi nyekundu.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...

Sarpong ‘aua’ shabiki Simba

Na MWANDISHI WETU, MWANZA BAO la dakika ya 29 lililofungwa na Michael Sarpong wa Yanga juzi, limesababisha kifo cha...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -