Saturday, October 31, 2020

Wozniacki aibuka mbabe Pan Pacific Open

Must Read

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya...

TOKYO, Japan

MKALI wa tenisi aliyewahi kuongoza kwa viwango vya dunia, Caroline Wozniacki, aliibuka mbabe kwenye mashindano ya wazi ya tenisi ya Pan Pacific dhidi ya mwenyeji wake, Naomi Osaka, ukiwa ni ubingwa wake wa kwanza tangu Februari 2015.

Wozniacki raia wa Denmark, ambaye amekumbwa na mfululizo wa majeraha mwaka huu, alianza kwa kasi mno kwenye pambano hilo dhidi ya mpinzani wake huyo kinda na kumshinda kwa seti 7-5 na 6-3.

“Ni mchezo wa mwisho katika michuano na nilitaka niufurahie,” alisema Wozniacki, ambaye alinyakua taji hilo la pili la Tokyo na la 24 katika muda wake wote wa kucheza tenisi.

“Ulikuwa ni mchezo wa fainali uliotukuta katika hali nzuri. Wote tulitaka kucheza vizuri. Nilifurahia mchezo kwa wakati huo.

“Majeraha hutokea na huwezi kujua ni muda gani utakaokaa nje ya uwanja bila kucheza, hivyo nafurahia kila wakati ninaoupata uwanjani,” alisema.

Wozniacki, kwa sasa anakamata nafasi ya 74, baada ya kupata majeraha ya mkono na kifundo cha mguu yaliyomfanya akose michezo mingi.

Kwa ushindi huo dhidi ya Osaka, Mdenmark huyo ameendeleza rekodi yake ya kunyakua ubingwa katika mashindano anayoshiriki tangu mwaka 2008 na anajiandaa kupanda hadi nafasi ya 22 au 23 kwenye viwango vya dunia.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika ujumbe kupitia ukurasa wake wa...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya kinda wa zamani wa timu...

Afua Suleiman afunguka ‘Utalijua Jiji’ ilivyompa ustaa mjini

NA JEREMIA ERNEST JINA alilopewa na wazazi wake ni Afua Suleiman na hata alipojitupa kwenye ulimwengu wa muziki wa...

Keche: Kundi maarufu Ghana linalowatamani Diamond, Kiba, Harmonize

JIACHIE na Staa Wako, wiki hii tumetua mpaka Accra, Ghana kwa kundi maarufu la muziki nchini humo, Keche linofanya vizuri na ngoma...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -