Friday, November 27, 2020

YAFAA MUISHI HIVI ILI MUWE HIVI KUPUNGUZA MIGOGORO

Must Read

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali...

HAKUNA uhusiano usiokumbwa na misukosuko, hata kidogo. Kila aliye katika mahusiano na mwenzake kuna kipindi ni lazima tu atajikuta akiingia katika mifarakano, iwe kwa kujua ama kutokujua. Mbali na ukweli huo ila, mifarakano ama matatizo mengi yanapoingia katika mahusiano huwa kuna hati hati ya mahusiano husika kufika tamati.

Wengi hujikuta wakiachana baada ya matatizo kutokea baina yao, japo kwa wengi huweza kuwa tofauti kabisa. Hii hutokana na namna wahusika wanavyoamua kuhusika na tatizo lenyewe. Ikiwa muhusika akiwa na mawazo ya haraka na uamuzi wa kukurupuka ni wazi asilimia za mahusiano yao kudumu ni chache sana. ukilingalisha  na yule anayeamua kuchunguza tatizo kwa umakini na kuamua kujiuliza kwanza kabla hajafikia katika kutoa maamuzi.

Wengi wanaoachana ama ambao matatizo huleta dhoruba kubwa katika mahusiano yao huwa na vitu viwili. Eidha huwa nakawaida ya kudharau tatizo, ama kulikuza kuliko uhalisia wake. Wengi utakuta baada kuona kuna tatizo linaanza kujichomoza katika mahusiano yao badala ya kuanza kulishughulikia hulidharau na kuona kama si tatizo.

Mtu wa aina hii huwa anasahau kuwa tatizo ni kama mimba, ambayo hukua taratibu na mwisho wake kuja kujidhihiri kwa kila mmoja. Unapodharau tatizo unatoa mwanya wa tatizo hilo kuja kukuumiza baada ya kuja kuwa kubwa.

We unamuona mwenzako leo siku ya pili hayuko katika hali yake ya kawaida badala ya kumuuliza ujue tatizo eti na wewe unakaa kimya tu mpaka akwambie mwenyewe. Kweli kwa mtindo huo mtafika? Katika hali hiyo hata kama ulimkera kidogo tu ila ukimya wako unaongeza tatizo lingine.

Anakuona kama usiyemjali na mtu usiyekuwa na hisia naye. Sasa kama tiba ya tatizo ilikuwa ni dakika tano umesababisha iwe ya masaa kadhaa sasa, maana kesi haitokuwa moja tu. Ile ya kumkera. Sasa atalalamika kwa kumkera na hili la kuwa kimya muda mrefu japo ulimuona katika hali isiyo ya kawaida.

Huo ni mfano tu juu ya kudharau tatizo ambalo linaonekana kama ni dogo. Ukiachana na watu wa aina hiyo, unakuta wengine ni mafundi wa kukuza mambo.

Mwenzake anaweza kufanya kosa kidogo badala ya kulihukumu kutokana na udogo wake yeye sasa anataka kumfanya mwenzake aonekane kama ndiye mkosaji zaidi kuwahi kuishi duniani. Kosa huenda ni kuchelewa kupokea simu tu tena kwa sababu iliyowazi, kama labda simu ilikuwa kwenye chaji, sasa hapo ataongea weweee. Atasema weee..! na mwisho kabisa bila kutarajia anaweza kujikuta akianzisha balaa lingine baina yao.

Kosa mwanzo lilikuwa kuchelewa kupokea simu ila sasa baada ya maneno kuwa mengi linazuka jingine. Sasa yule mkosaji unaweza kukuta akihisi kuonewa ama kunyanyasika kutokana na maneno anayoambiwa. Katika aina hii wengi wameharibu amani na utulivu wa ndoa zao.

Unapokosa umakini katika kutatua tatizo ndani ya mahusiano yako jua una uwezekano wa kuwa unatengeneza tatizo kubwa zaidi kati yako na mwenzako.

Lichukulie tatizo kama lilivyo na lipe kile linachostahili. Kama unaona linatakiwa kutafutiwa ufumbuzi basi mara moja inabidi ifanyike hivyo. Usijaribu kuendelea kusubiri kwa kile kinachoitwa kutafuta muda muafaka. Hakuna muda muafaka.

Tatizo kila linapochomoza yafaa kulighulikia mara moja ili mambo mengine yaweze kwenda vizuri. Hakuna muda muafaka wa kutatua tatizo. Usipoteze muda kwa kuusubiria. Kila muda ni muafaka tu. Suala ni uamuzi tu. Amua sasa!

ramadhanimasenga@yahoo.com

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...

Sarpong ‘aua’ shabiki Simba

Na MWANDISHI WETU, MWANZA BAO la dakika ya 29 lililofungwa na Michael Sarpong wa Yanga juzi, limesababisha kifo cha...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -