Thursday, December 3, 2020

YALIYOSISIMUA EPL WIKIENDI HII

Must Read

HUJUMA NZITO YANGA

NA WINFRIDA MTOI UONGOZI wa Yanga upo katika harakati za kuhamishia mechi zao zilizobaki...

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

MANCHESTER, England

WAKATI Jose Mourinho akitambulishwa Old Trafford, kila mtu aliamini ungekuwa mwisho wa Juan Mata katika jezi ya Manchester United.

Lakini mambo yamekuwa tofauti na wawili hawa wameonekana kufanya kazi kwa ushirikiano mkubwa licha ya tofauti iliyotokea awali.

Akiwa Chelsea, Mourinho alimuuza Mata kwa United lakini siku zote za maisha yake, Jose amekuwa akiheshimu ubora wa kiungo huyo wa Kihispania.

Ubongo wa Mata kwenye kuuelewa mpira ni wa kiwango cha juu sana. Hana kasi ya kukimbizana na mabeki kama alivyo Anthony Martial, lakini amekuwa hatari anapotokea wingi ya kulia.

Kiwango alichokionyesha dhidi ya Watford, ni matunda ya uvumilivu aliouonyesha Jose Mourinho kwa kuendelea kumpa nafasi kwenye kikosi cha kwanza.

Kwanini Alex Oxlade-Chamberlain anapangwa kiungo wa kati?

Mwanzoni mwa msimu, Alex Oxlade-Chamberlain, alishauriwa kuondoka Arsenal na kutafuta sehemu nyingine atakapocheza na kulinda kiwango chake.

Lakini uwezo aliouonyesha kwenye pambano dhidi ya Hull, tena akicheza kama kiungo wa kati, umefanya wengi kubadili mawazo na kuamini pengine hii ni nafasi sahihi kwake kwenye kikosi cha kwanza.

Mara nyingi Oxlade-Chamberlain anacheza nafasi za pembeni, lakini kasi yake, nguvu na uwezo mkubwa wa kupandisha timu ikawa faida kubwa kwa Arsenal, kwenye eneo la katikati ya uwanja.

Oxlade-Chamberlain ni mchezaji anayejiamini na kitu pekee anachokihitaji kwa sasa ni kuungwa mkono na mashabiki wake.

Bila shaka mchezo wa Ligi ya Mabingwa dhidi ya Bayern Munich, utakuwa kipimo sahihi kwake kuonyesha namna anavyostahili kuaminiwa katika eneo la kiungo.

Mane alivyowaonyesha Spurs umuhimu wa Rose

Kichapo walichokipata Tottenham katika dimba la Anfield, kilitosha kabisa kuonyesha umuhimu wa beki Danny Rose kwenye kikosi chao.

Ben Davies aliyechukua nafasi ya Rose, hakuwa na uwezo wa kupambana na straika hatari wa Liverpool, Sadio Mane. Alizidiwa kasi kwa kiasi kikubwa.

Mchezo wa kwanza uliopigwa White Hart Lake, Agosti mwaka jana, Rose aliweza kumbana vyema Mane na kumlazimisha akimbie wingi ya pembeni na kuingia katikati.

Kwa ushindi wa Liverpool, mtu pekee anayetakiwa kupongezwa ni kocha Jurgen Klopp, ambaye alitambua udhaifu wa Tottenham na kuufanyia kazi.

Spurs bila Rose ni kitu kingine tofauti na kama kungekuwa na uwezekano, kocha Mauricio Pochettino, angetumia nafasi hii kumpa mkataba mpya beki huyo wa kimataifa wa England.

Lucas ni shujaa asiyeimbwa Liverpool

Sifa nyingi zinaweza kwenda kwa Sadio Mane kutokana na mabao yake lakini Mbrazil, Lucas anastahili kupongezwa kwa kiwango alichokionyesha dhidi ya Tottenham.

Kwa kiwango chake, wengi waliamini angepata shida sana mbele ya washambuliaji walio kwenye ubora kipindi hiki, Harry Kane na Dele Alli, lakini Lucas alitulia na kuwazima wawili hawa.

Alisimama imara kwenye safu ya ulinzi, hakuwa na kazi kubwa zaidi ya kuhakikisha mastraika hawa wa Tottenham wanavurugika na kukosa muunganiko kati yao.

Wakati huu Liverpool wanapowakosa, Dejan Lovren na Joel Matip, walio majeruhi ni muda mzuri wa Klopp kumwamini Lucas kwenye nafasi ya ulinzi.

Manolo ni wa kipekee EPL

Manolo Gabbiadini ni straika halisi wa kizamani.

Ni tofauti na mastraika wengi wa kisasa wanaoweza kushuka na kucheza kama namba 10, yeye kazi yake ni moja tu, kukaa kwenye nafasi na kuzitumia zinapopatikana.

Ni msimu wake wa kwanza EPL akiwa na Southampton, hivyo kuna mengi ya kusubiri kutoka kwake.

Turf Moor si pa mchezo mchezo

Unajua kwanini Turf Moor umekuwa uwanja mgumu sana kwa vigogo wa Premier League? Burnley wanapiga kazi si ya kitoto pale.

Sean Dyche amekitengeneza kikosi chake kuwa hatari wanapokuwa kwenye uwanja wao wa nyumbani, wanakaba mpaka kivuli. Haikuwa rahisi hata kidogo kwa vinara wa ligi, Chelsea kung’aa kwenye dimba la Turf Moor.

Kuna tatizo moja tu Swansea

Ushindi dhidi ya Leicester ulionyesha ni namna gani Swansea wameimarika kwenye safu yao ya ulinzi.

Shida pekee inayowakabili ni kwamba hawana uwezo wa kushinda mechi tatu mfululizo, wakishinda leo, tarajia watapoteza mchezo unaofuata, hii inaweza kuwagharimu wasipolifanyia kazi.

Dhidi ya Leicester, walinzi wa Swansea waliweza kuwaweka mfukoni mastraika Vardy na Riyad Mahrez, hali iliyowapa nafasi ya kutawala mchezo kwa kiwango kikubwa.

Wanavutia kutazama kwa soka lao lakini ni wakati sasa wa wao kutafuta namna nzuri ya kucheza kwa kujilinda ili wasiruhusu mabao.

Kazi nzito kwa Bilic 

Hakika Slaven Bilic alikuwa kwenye wakati mgumu sana pale alipoiona timu yake ikiruhusu bao dakika ya mwisho ya mchezo.

West Ham waliruhusu bao dakika za mwisho dhidi ya Wesr Brom na kufanya mchezo kumalizika kwa sare ya bao 2-2 na hivi sasa wamepoteza pointi 6 kwa kuruhusu bao dakika za mwisho.

 

 

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

HUJUMA NZITO YANGA

NA WINFRIDA MTOI UONGOZI wa Yanga upo katika harakati za kuhamishia mechi zao zilizobaki...

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul 'Ben Pol' ameshukuru mashabiki kwa...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -