Wednesday, October 21, 2020

Yanga achana nao

Must Read

Director Kenny: Harmonize alinipeleka WCB nikafanya video ya Lavalava

MWONGOZAJI bora wa video nchini, Kenned Sanga a.k.a Derector Kenny kutoka Zoom Extra, ametua   hapa Jiachie na...

Rogers mwanamuziki anayevutiwa na Marijani

NA JEREMIA ERNEST BONGO Star Search (BSS), ni shindano lililofanikiwa kuibua vipaji vingi vya...

Ihefu, Azam patachimbika Sokoine, Katwila ndani

NA ASHA KIGUNDULATIMU ya Ihefu inatarajia kushuka uwanjani kucheza na Azam ukiwa ni mchezo wa Ligi Kuu...

NA WINFRIDA MTOI

UONGOZI wa Yanga umekuja na mkakati maalum wa kuhakikisha wanakusanya pointi tatu kila mchezo, wakianzia mechi dhidi ya Mtibwa Sugar, Jumapili hii.

Yanga inatarajia kushuka dimbani katika mchezo wake nne wa Ligi Kuu Tanzania Bara ikikutana na Mtibwa Sugar kwenye Uwanja wa Jamhuri, Morogoro.

Makamu Mwenyekiti wa klabu hiyo, Frederick Mwakalebela, ameliambia BINGWA kuwa baada ya kufanikiwa kuondoka na pointi tatu Bukoba, hawatarudi nyuma bali wanaongeza nguvu katika kukabiliana na michezo hiyo.

Alisema kama uongozi umewaweka bayana wachezaji na benchi la ufundi kuwa waseme chochote wanachotaka wao watatekeleza, muhimu ushindi upatikane.

Mwakalebela alisema mikakati hiyo ilianzia katika kuweka kambi eneo bora na tulivu na baada ya mchezo wa Kagera, benchi la ufundi limeulizwa nini kiongezeke.

“Kwa upande wetu uongozi, tumejiandaa kujitoa kwa kila jambo, iwe kwa mchezaji au benchi la ufundi, tunachohitaji ni ushindi wa kutuwezesha kuchukua ubingwa msimu huu,” alisema Mwakalebela.

Alifafanua kuwa kila timu ilipo na wao wapo kuhakikisha wanafanikiwa malengo yao msimu huu na hakuna atakayewazuia ubingwa.

Alieleza kuwa baada ya timu kuwasili juzi wachezaji walipewa mapumziko ya siku moja na jana jioni walirejea kambini kuendelea na mazoezi hadi pale wakataoelekea Morogoro.

Alisema Kocha Mkuu wa kikosi hicho, Zlatko Krmpotic, amewatoa hofu na kuwaambia kikosi baada ya muda mchache kitakuwa tishio kwani anaelekea kupata kikosi cha kwanza (first 11) cha uhakika.

“Kocha ametuthibitishia kuwa kikosi kinaekea kukaa sawa kwa sababu kilichokuwa kinasumbua ni kupata ‘first 11’ ya uhakika, baada ya mechi na Kagera, ametuambia kuna mabadiliko makubwa.

“Tunaamini katika muda uliobaki kabla ya kukutana na Mtibwa Sugar atakuwa ameboresha  zaidi na wachezaji wanaonekana wana morali nzuri kwa sababu mara nyingi tunakuwa nao kuwasapoti kambini,” alisema Mwakalebela.

Kuhusu ushindi waliopata watani wao Simba, Mwakalebela alisema kwa sababu wamekutana na timu ya kawaida, hauwezi kuwaumiza kichwa, wanachoangalia ni alama tatu tu.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Director Kenny: Harmonize alinipeleka WCB nikafanya video ya Lavalava

MWONGOZAJI bora wa video nchini, Kenned Sanga a.k.a Derector Kenny kutoka Zoom Extra, ametua   hapa Jiachie na...

Rogers mwanamuziki anayevutiwa na Marijani

NA JEREMIA ERNEST BONGO Star Search (BSS), ni shindano lililofanikiwa kuibua vipaji vingi vya wanamuziki wa Tanzania ambao miongoni...

Ihefu, Azam patachimbika Sokoine, Katwila ndani

NA ASHA KIGUNDULATIMU ya Ihefu inatarajia kushuka uwanjani kucheza na Azam ukiwa ni mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara  (VPL), utakaochezwa leo...

Mugalu atema cheche Simba

NA ASHA KIGUNDULA MSHAMBULIAJI wa Simba, Chris Mugalu, amesema wanakwenda mkoani Rukwa kupambana na kupata ushindi katika mchezo wao...

Malale aitisha Yanga

NA ZAINAB IDDY KOCHA Mkuu wa timu ya Polisi Tanzania, Malale Hamsini, amezisikia sifa za kocha mpya wa Yanga,...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -