Wednesday, September 30, 2020

Yanga anasa mrithi wa Abdul

Must Read

KISA KONA YA CARLINHOS… ...

NA ZAINAB IDDY BAO la Yanga lililofungwa na Lamine Moro juzi katika mchezo dhidi...

HUYU MUGALU ATAWALAZA WATU NA VIATU TU!

NA ONESMO KAPINGA HAKIKA sijapata utamu wa mshambuliaji mpya wa Simba, raia wa DR...

Wachezaji Gwambina wapewa muda

NA ZAINAB IDDY KOCHA wa timu wa  Gwambina, Fulgence Novatus, amesema amewapa muda wachezaji wake ...

NA ZAINAB IDDY

UONGOZI wa Yanga jana umweingia mkataba wa miaka miwili na beki wa kulia wa timu ya Mtibwa Sugar, Kibwana Shomari.

Yanga imemsajili Shomari akitajwa kuwa mrithi wa beki wao wa zamani wa kulia, Juma Abdul aliyeachana na Wanajangwani hao baada ya kushindwa kufikia muafaka juu kuingia kandarasi mpya.

Shimaro alikuwa katika mazungumzo na Simba waliomuhitaji ili kumsaidia Shomari Kapombe baada ya kuwa na tatizo la kupata majeraha ya mara kwa mara.

Usajili wa Kibwana Yanga unakuwa ni wa tano tangu kufunguliwa kwa dirisha la usajili wa msimu wa 2020/21, huku likitaraji kufungwa mwishoni mwa mwezi huu.

Wachezaji wengine waliosajiliwa Yanga ni mabeki Bakari Mwamnyeto kutoka Coastal Union, Yassin Mustaph (Polisi Tanzania) na Abdalah Shaibu (huru), huku wengine wakiwa ni mshambuliji Wazir Junior (Mbao FC) na kiungo Zawad Mauya (Kagera Sugar).

Akizungumza na BINGWA baada ya kusaini mkataba, Shomari alisema amefurahi kujiunga na Yanga kwani ni sehemu ya ndoto zake za kucheza katika timu kubwa ndani ya Tanzania.

“Ukicheza timu kubwa ni rahisi kuonekana, iwe katika timu ya taifa au nje ya mipaka ya Tanzani. Kujiunga na Yanga ni fursa kubwa sana ambayo natakiwa kuitumia vizuri ili nitimize malengo niliyojiwekea.

“Naomba mashabiki wa Yanga wanipokee, wanipe ushirikiano na viongozi kunielekeza pale nitakapoonekana naenda kinyume kwa sababu umri wangu bado mdogo, nahitaji kulelewa na walionitangulia.

“Kama watanielekeza njia sahihi, nina uhakika nitafanya kazi iliyonileta Yanga kwa ufanisi na kuwapa furaha ile wanayoihitaji,” alisema.

Kwa upande wake, Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano Yanga, Hassan Bumbuli, alisema: “Usajili huu umelenga kuimarisha safu ya ulinzi ukiwa ni mwendelezo wa wachezaji wa ndani, kabla ya kuhamia kwa wa kimataifa ambako ndiko tutakapohitimisha suala zima la usajili.” 

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

KISA KONA YA CARLINHOS… ...

NA ZAINAB IDDY BAO la Yanga lililofungwa na Lamine Moro juzi katika mchezo dhidi...

HUYU MUGALU ATAWALAZA WATU NA VIATU TU!

NA ONESMO KAPINGA HAKIKA sijapata utamu wa mshambuliaji mpya wa Simba, raia wa DR Congo, Chris Mugalu,kutokana na jinsi...

Wachezaji Gwambina wapewa muda

NA ZAINAB IDDY KOCHA wa timu wa  Gwambina, Fulgence Novatus, amesema amewapa muda wachezaji wake  ili aweze kutathimini kiwango cha...

Kisu amfunika vibaya Manula

NA ZAINAB IDDY KIPA  wa timu ya Azam, David Kisu, amemfunika Aishi Manula  wa Simba kutokana na kutoruhusu...

Zahera awapa Simba taji mapema

NA ZAINAB IDDY BAADA ya Gwambina kufungwa mabao 3-0 na Simba  katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -