Friday, October 30, 2020

Yanga, Azam mjiandae kuanzia sasa kimataifa

Must Read

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya...

NA EZEKIEL TENDWA

MABINGWA watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Yanga pamoja na Azam FC, ndizo timu ambazo zitaiwakilisha nchi katika michuano ya kimataifa mwakani kutokana na kufanya vizuri msimu uliopita.

Yanga kama mabingwa wataiwakilisha nchi michuano ya Klabu Bingwa Afrika wakati Azam FC wataiwakilisha  michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika baada ya kumaliza ligi nafasi ya pili.

Timu hizi kwa miaka minne mfululizo ndizo ambazo zimekuwa zikiiwakilisha nchi kwenye michuano hiyo, kutokana na kumaliza nafasi za juu lakini hazikufanya vizuri katika mashindano hayo kama ilivyokuwa imetarajiwa.

Yanga msimu uliopita walishiriki michuano ya Klabu Bingwa lakini walishindwa kupiga hatua kubwa na wakajikuta wakisukumwa mpaka kwenye michuano ya Kombe la Shirikisho nako huko wakaangukia kundi la timu vigogo wakatolewa.

Wanajangwani hao waliangukia kundi lililokuwa na timu za Medeama ya Ghana, Mo Bejaia ya Lgeria pamoja na waliokuwa mabingwa watetezi wa Klabu Bingwa, TP Mazembe na mwisho wa siku Yanga wakaangukia pua na kurudi nyumbani mikono mitupu.

Kwa upande wao, Azam FC ndiyo kabisa hawakufika mbali kwani waliondolewa mapema na kurudi kuendelea na Ligi Kuu Tanzania Bara ambayo Yanga ndio mabingwa watetezi.

Timu hizi kwa sasa zinatakiwa zijitafakari upya kabla ya kuanza kwa mikikimikiki hiyo, kwani macho na masikio ya Watanzania wote yatakuwa kwao na kama watafanya vizuri ni kwa faida ya wote na wakifanya vibaya ni aibu kwa wote.

Bahati mbaya iliyopo kwa timu hizi kwa sasa ni kwamba, kila moja ipo na benchi jipya la ufundi kitu ambacho kinaleta wasiwasi mkubwa wadau wa soka wakijiuliza nini kitatokea mbele ya safari yao hiyo.

Yanga ambao wamekuwa na kocha wao mkuu Hans van der Pluijm ambaye amewajua vizuri wachezaji wake, tayari ameshashushwa ngazi na cheo hicho akipewa kocha mpya George Lwandamina, huku Azam nao wakisuasua na Zebensul Hernandez raia wa nchini Hispania.

Sifa ya Lwandamina ni kubwa sana kwani timu alizopitia zilifanya vizuri ikiwamo Zesco ya nchini Zambia pamoja na timu ya Taifa hilo, lakini hapa anakuja kukutana na wachezaji wapya ambao hajazoeana nao hivyo ataanza kuingiza falsafa zake mpya ambazo kama wachezaji watashindwa kuzidaka mapema inaweza ikawa hasara kwao.

Kwa upande wa Azam FC nao kocha wao huyo bado hajafanya kile ambacho wengi walitegemea, ikizingatiwa kuwa anatokea Hispania ambapo soka la kule ni la kitabuni ndiyo maana waliianza ligi kwa kusuasua.

Kikubwa ambacho Yanga na Azam wanatakiwa kukifanya mapema ni kuanza maandalizi kuanzia sasa ili makocha wapate muda wa kutosha wa kukaa na wachezaji wao na kuwajua ndani na nje vinginevyo hali inaweza ikawa ya wasiwasi.

Ni kweli kwamba Lwandamina ni kocha mzuri na Uafrika wake ni faida kubwa sana kwa Yanga, lakini hilo halina maana kwamba anaweza kufanikiwa kirahisi kama maandalizi yatakuwa ya kusuasua. Wasipompa muda wa kutosha watamuona mbaya haraka sana.

Timu zetu zimekuwa zikishindwa kupata matokeo mazuri linapokuja suala la michuano ya kimataifa na mchawi mkubwa ambaye yupo ni maandalizi duni yanayofanywa na timu hizo.

Ndiyo maana hata timu yetu ya Taifa ‘Taifa Stars’ imekuwa ikisuasua kila mara kwa sababu kocha hapewi muda wa kutosha wa kukaa na wachezaji wake na kuwaandaa vizuri.

Muda huu ndiyo sahihi kwa Yanga na Azam kuanza kupanga mipango ya kufanya vizuri michuano hiyo ya kimataifa kuliko kuelekeza akili kwenye ligi kuu peke yake, kwani kuiangalia ligi peke yake na kuangalia namna ya kuifunga Ruvu Shooting au Simba wakasahau kwamba wanaweza kukutana na timu kama Etoile Du Sahel ni hatari kubwa.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika ujumbe kupitia ukurasa wake wa...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya kinda wa zamani wa timu...

Afua Suleiman afunguka ‘Utalijua Jiji’ ilivyompa ustaa mjini

NA JEREMIA ERNEST JINA alilopewa na wazazi wake ni Afua Suleiman na hata alipojitupa kwenye ulimwengu wa muziki wa...

Keche: Kundi maarufu Ghana linalowatamani Diamond, Kiba, Harmonize

JIACHIE na Staa Wako, wiki hii tumetua mpaka Accra, Ghana kwa kundi maarufu la muziki nchini humo, Keche linofanya vizuri na ngoma...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -