Saturday, November 28, 2020

YANGA, AZAM MKIZINGATIA USHAURI WA PLUIJM MTAVUKA SALAMA

Must Read

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali...

NA EZEKIEL TENDWA

LEO Yanga watashuka katika Uwanja wa Taifa nchini Zambia kupepetana na wenyeji wao Zanaco FC, mchezo wa marudiano wa Ligi ya Mabingwa Afrika, huku Azam FC wao wakisubiri hadi kesho kuwakabili Mbabane Swallows ya nchini Swazland, Kombe la Shirikisho.

Wakati Yanga wakitakiwa kufanya kila linalowezekana ili kuibuka na ushindi au kutoka sare ya kufungana zaidi ya mabao 2-2 ili kuvuka hatua inayofuata, Azam wao watatakiwa kuhakikisha wanatoka sare yoyote au kuibuka na ushindi wowote.

Yanga wanatakiwa kuhakikisha wanashinda au kupata sare isiyopungua mabao 2-2 ili kuvuka kutokana na kukubali kulazimishwa sare ya kufungana bao 1-1 mchezo wa kwanza Uwanja wa Taifa, huku Azam wao angalau wakiwa na kitu kidogo mkononi kwani waliibuka na ushindi mwembamba wa bao 1-0 nyumbani.

Ukweli ni kwamba, timu zetu hazitakuwa na kazi rahisi ya kupenya kutokana na kwamba wenyeji wao nao watataka kuhakikisha wanatumia vizuri viwanja vyao vya nyumbani kushinda na kusonga mbele, lakini pia kama waswahili wanavyosema ‘hakuna lisilowezekana chini ya mbingu’ ndivyo wawakilishi wetu hawa wanavyoweza kupenya.

Nimesema Yanga na Azam hawatakuwa na kazi rahisi kwa sababu niliuona uchezaji wa Zanaco na nikaona pia jinsi Mbabane wanavyocheza, nikagundua kuwa timu zetu zinatakiwa kupambana kisawasawa na kama wakiweka masihara pembeni wanaweza wakavuka salama.

Juu ya uwakilishi huo wa timu zetu hizi mbili, mwanzoni mwa wiki hii nilipata fursa ya kuzungumza na kocha wa zamani wa Yanga, Hans van der Pluijm, kuhusu maoni yake ambapo alisema kuwa wawakilishi wetu hawa wanaweza wakavuka kirahisi kama wataamua kupambana.

Pluijm aliniambia moja ya mambo ambayo yanaweza kuwarahisishia kazi wawakilishi wetu hawa ni kama wataelewa matokeo ya ushindi yanapatikana popote, iwe uwanja wa nyumbani ama ugenini na kudai kuwa Yanga wanaweza wakawafunga Zanaco na Azam wakaendelea kulinda ushindi wao ugenini.

Kocha huyo ambaye wana-Yanga wenyewe wanakubali kazi yake kutokana na mambo makubwa aliyowafanyia kabla ya kumwondoa bila sababu za msingi, amesema wachezaji lazima wajue kuwa wanalo jukumu kubwa la kuwafurahisha mashabiki wao hivyo lazima wapambane ndani ya uwanja.

Katika ushauri wake, Pluijm amewaambia mashabiki nao lazima wasimame kidete kuzisapoti timu zao na wala wasikate tamaa kwani mpira wa siku hizi upo wazi sana, ambapo timu inaweza ikapata matokeo popote tofauti na zamani ambapo timu mwenyeji ndiyo iliyokuwa ikipewa nafasi kubwa ya kushinda.

Binafsi nimemwelewa sana Pluijm, ni ukweli usiokuwa na shaka kwamba Yanga na Azam FC wanaweza wakapenya kama wataamua kupambana. Kama wachezaji wataamua kuweka shida zao pembeni na kuamua kupigana kiume ni wazi kuanzia leo jioni mpaka kesho na wiki nzima inayokuja Tanzania itatawaliwa na furaha ya timu zetu kusonga mbele.

Nilikuwa mmoja wa wadau wa soka niliyefuatilia kwa ukaribu mechi za kwanza za Yanga na Azam FC dhidi ya wapinzani wao hao na kitu kimoja kikubwa nilichokigundua ni kwamba, tunachokikosa hasa kwa wachezaji wetu ni kupambana ndani ya uwanja.

Yanga walicheza vizuri lakini Zanaco walicheza vizuri sana ndiyo maana hata baada ya mpira kumalizika mashabiki walionekana kutofurahi kabisa tofauti na kipindi cha nyuma, ambapo mabingwa hao watetezi walikuwa wakicheza kandanda la kuvutia na hata wakipata matokeo mabaya mashabiki wao angalau walikuwa wakisifu kiwango. Na hata Mbabane kwani licha ya kushindwa na Azam FC, lakini tuliona utofauti kati ya wachezaji wetu na wao.

Yote kwa yote Yanga na Azam FC wakisikiliza ushauri wa Pluijm bila shaka watavuka salama. Mungu ibariki Yanga, Mungu ibariki Azam FC, Mungu ibariki Tanzania.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...

Sarpong ‘aua’ shabiki Simba

Na MWANDISHI WETU, MWANZA BAO la dakika ya 29 lililofungwa na Michael Sarpong wa Yanga juzi, limesababisha kifo cha...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -