Wednesday, October 28, 2020

YANGA ‘BAMPA TO BAMPA’

Must Read

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya...

NA ZAITUNI KIBWANA

SASA Yanga watakuwa na kazi kubwa ya kuhakikisha wanakaza buti (bampa to bampa) ili kubaki kileleni mwa msimamo, baada ya ushindi wa mabao 2-0 dhidi Mwadui katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara uliochewa jana kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Kwa mabao hayo mawili yaliyofungwa na mshambuliaji Obren Chirwa, yameifanya Yanga kukaa kileleni ikiwa na pointi 46 wakiwazidi mahasimu wao Simba ambao sasa wanashika nafasi ya pili kwa pointi moja.

Azam wanashika nafasi ya tatu wakiwa na pointi 34, baada ya kuichapa Simba bao 1-0 katika mchezo wa Jumamosi ya wiki iliyopita, huku Mtibwa ambao leo watakuwa na kazi ngumu kwa Kagera kwenye Uwanja wa Kaitaba, wanashika nafasi ya tatu wakiwa na pointi 31 sawa na Kagera.

Katika mchezo huo wa Yanga na Mwadui, ulianza kwa kasi ambapo dakika ya tano ya mchezo huo, Haruna Niyonzima alitoa pasi nzuri kwa Simon Msuva ambaye alipiga shuti lililotoka nje ya lango.

Dakika chache baadaye, krosi ya Msuva ilitua kichwani mwa mshambuliaji Amisi Tambwe, lakini mpira wake ulipita umbali kidogo mwa lango la Mwadui.

Katika dakika ya 10 na 18, mshambuliaji wa Mwadui, Paul Nonga, angeweza kuifungia timu yake, lakini mabeki na mlinda mlango wa Yanga, Deogratius Munishi ‘Dida’ walikuwa makini na kuokoa hatari zote.

Mwadui wanaonolewa na kocha Ally Bushiri, walionekana kucheza vizuri kwa mipango hasa kwenye safu yao ya ulinzi na wapinzani wao kushindwa kutumia nafasi zao vizuri, baada ya kiungo wa  Yanga, Justine Zulu ‘Mkata Umeme’, kushindwa kuunganisha vizuri krosi ya Msuva dakika ya 29 kutokana na kubanwa.

Dakika chache kabla ya mapumziko, beki wa Mwadui, Malika Ndeule, alifanya kazi nzuri kuokoa krosi ya Tambwe na kumaliza kipindi hicho cha kwanza bila ya kufungana.

Kipindi cha pili nacho kiliaanza kwa kasi, huku Yanga wakipambana kuhakikisha wanazoa pointi zote tatu kwa kutengeneza nafasi nyingi za mabao, ambapo dakika ya 56, Msuva alitoa pasi nzuri kwa Tambwe lakini kabla hajaifikia beki wa kulia na nahodha wa Mwadui, Said Nassor ‘Cholo’, akauokoa mpira huo.

Dakika ya 69, Chirwa aliyeingia kipindi cha pili kuchukua nafasi ya Niyonzima, aliifungia Yanga bao la kwanza akiunganisha mpira uliotemwa na mlinda mlango, Shaban Kado, baada ya shuti kali la Msuva.

Chirwa alikamilisha idaidi ya mabao yake mawili, baada ya kuifungia Yanga bao la pili dakika ya 82, akimalizia krosi ya kiungo Thaban Kamusoko.

Kikosi cha Yanga kilikuwa: Dida, Juma Abdul, Mwinyi Haji, Kelvin Yondani, Nadir Haroub, Zulu, Msuva, Kamusoko, Tambwe/Said Juma, Niyonzima/ Chirwa, Deus Kaseke/ Emmanuel Martine.

Mwadui ilikuwa: Kado, Cholo, Yassin Mustapha/David Luhende, Malika Ndeule, Iddy Mobby, Kabunda, Razack Khalphani, Awadhi Juma, Nonga, Salim Khamis/Joseph Kimwaga, Abdallah Seseme.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika ujumbe kupitia ukurasa wake wa...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya kinda wa zamani wa timu...

Afua Suleiman afunguka ‘Utalijua Jiji’ ilivyompa ustaa mjini

NA JEREMIA ERNEST JINA alilopewa na wazazi wake ni Afua Suleiman na hata alipojitupa kwenye ulimwengu wa muziki wa...

Keche: Kundi maarufu Ghana linalowatamani Diamond, Kiba, Harmonize

JIACHIE na Staa Wako, wiki hii tumetua mpaka Accra, Ghana kwa kundi maarufu la muziki nchini humo, Keche linofanya vizuri na ngoma...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -