Saturday, November 28, 2020

YANGA HAITAKI MAZOEA AISEE!

Must Read

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali...

HUSSEIN OMAR NA ZAINAB IDDY

KIKOSI cha Yanga kilichokusudiwa kuivaa Stand United leo katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam kwenye mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara, kimeonyesha kwamba klabu hiyo ya Jangwani haitaki mazoea.

Kulikuwa na hofu kubwa kwa mashabiki wa klabu hiyo kutokana na wachezaji wake muhimu wanne kuwa na kadi za njano, wakihofia kupata kadi nyingine kwenye mchezo wa leo na kuikosa mechi ya mahasimu wao Simba itakayochezwa Februari 25, mwaka huu.

Hivyo huenda ikageuza kibao na kuwapumzisha nyota hao wanne wenye kadi mbili za njano kila mmoja, ambao ni Haruna Niyonzima, Deus Kaseke, Said Juma ‘Makapu’ na Kelvin Yondani, huku Amissi Tambwe akiukosa mchezo huo kwa kuwa na adhabu ya kadi tatu za njano.

Kwenye mazoezi ya maandalizi ya mechi hiyo dhidi ya Stand yaliyofanyika wiki hii katika Uwanja wa Chuo cha Polisi, Kurasini jijini Dar es Salaam, benchi la ufundi lilionekana kutumia kikosi tofauti na kile kilichozoeleka kwa lengo la kuwapumzisha wachezaji hao wenye kadi.

Katika mazoezi hayo kocha George Lwandamina, alionekana akiwachezesha mabeki wa kati, Nadir Haroud ‘Cannavaro’ na Andrew Vicent ‘Dante’, huku pembeni akianza Juma Abdul na Mwinyi Haji.

Kwa upande wa safu ya kiungo, Lwandamina alionekana kumtumia Justine Zulu na Thaban Kamusoko, wakisaidiana na Simon Msuva winga ya kulia, kushoto anaweza kucheza Emanuel Martine ama Juma Mahadhi, ikiwa Donald Ngoma ataanza kwenye kikosi hicho sambamba na Obrey Chirwa.

Kama Ngoma hatakuwa fiti, basi huenda Martine akaanza na Mahadhi kucheza nyuma ya Chirwa.

Huenda kikosi hicho kipya cha mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara, kikavuruga mipango ya Stand, ambao walitarajia kukutana na wachezaji tofauti na wale ambao waliwachapa bao 1-0 katika mchezo wa mzunguko wa kwanza uliochezwa Shinganya.

Awali Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kupitia Bodi ya Ligi Kuu ilisogeza mbele mchezo huo hadi Februari 5 mwaka huu, ili kupisha mechi ya kirafiki ya kati ya Yanga na Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini.

Lakini kocha wa mabingwa hao wa Tanzania, Lwandamina aligomea mchezo huo, akisema utaingilia programu zake, hivyo bodi kuamua kuurudisha mchezo huo leo.

Akizungumzia mchezo huo kocha msaidizi wa  Yanga, Juma Mwambusi, ameliambia BINGWA: “Mchezo wetu ni muhimu sana kwetu kwa kuwa tunahitaji pointi tatu ambazo zitatuhakikishia kuendelea kubaki kileleni.”

Stand wataingia kwenye mchezo huo bila ya kocha wao, Hemed Moroco, ambaye alitolewa kwenye mechi dhidi ya JKT Ruvu, akidaiwa kutofautiana na mwamuzi, Alex Mahagi.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...

Sarpong ‘aua’ shabiki Simba

Na MWANDISHI WETU, MWANZA BAO la dakika ya 29 lililofungwa na Michael Sarpong wa Yanga juzi, limesababisha kifo cha...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -