Friday, November 27, 2020

YANGA HAKUNA KUREMBA LEO

Must Read

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali...

YANGA leo wanashuka katika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, kumenyana na MC Alger ya Algeria, katika mchezo muhimu mno wa kuwania kutinga hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika, ambapo watatakiwa kufanya kila wawezalo ili watoke uwanjani na ushindi mnono.

Wawakilishi hao pekee wa Tanzania katika michuano ya kimataifa watatakiwa kupata ushindi mnono ili watakaporudiana na MC Alger ugenini siku chache zijazo, wasijikute wakiwa na kibarua kigumu cha kuwatoa wapinzani wao hao.

Yanga wamejikuta wakiangukia katika michuano ya Kombe la Shirikisho baada ya kutolewa na Zanaco ya Zambia kwenye kipute cha Ligi ya Mabingwa Afrika raundi ya pili, kutokana na sare ya bao 1-1 kwenye Uwanja wa Taifa, kabla ya suluhu ya ugenini na hivyo wapinzani wao hao kusonga mbele kwa faida ya bao la ugenini.

BINGWA tunaamini kwamba, kwa ubora wa wachezaji wa Yanga, lakini pia morali uliopo ndani ya timu, hasa baada ya kufanikiwa kurejea kileleni mwa Ligi Kuu Tanzania Bara, hatuna shaka kuwa wakali hao wa Jangwani lazima watashinda leo.

Hata hivyo, ushindi utakuja iwapo tu wachezaji wake watakuwa makini kufuata maelekezo ya makocha wao, zaidi ikiwa ni kutumia kila nafasi watakazozipata, ikiwamo kuepuka kufanya kosa lolote linaloweza kuwagharimu.

Wachezaji wa Yanga wanaposhuka dimbani kuwavaa MC Alger, wafahamu kuwa wamebeba matumaini ya Watanzania, ambao wamekuwa na shauku ya siku moja kuiona timu yao ikifanya kweli kwenye michuano hiyo.

Kwa miaka mingi, timu zetu zimekuwa wasindikizaji kwenye michuano hiyo, mara nyingi zikiishia hatua za awali, huku zikizikodolea macho timu za Afrika Kaskazini na Magharibi pamoja na TP Mazembe zikiendelea kufunika.

Hata hivyo, Yanga wasitarajie mteremko leo kutoka kwa wapinzani wao hao, kwani timu hiyo inaonekana kuwa si ya kubeza kiasi kwamba iwapo vijana wa George Lwandamina hawatakuwa makini, wanaweza kujikuta wakipoteza mchezo huo na kuzidi kuwasononesha Watanzania.

Yanga wanatakiwa kuwa makini mno kwa dakika zote 90 na ikiwezekana kushambulia kwa mipango kuepuka kutumia nguvu nyingi katika kusaka mabao na mwisho wa siku kujikuta wakiishia kupoteza nafasi lukuki, kama ilivyojitokeza katika mechi dhidi ya Zanaco na nyinginezo za kimataifa zilizopita.

Iwapo Yanga wataichapa MC Alger leo kwa idadi kubwa ya mabao, watakuwa na uhakika wa kutinga hatua ya makundi, kwani uzoefu unaonyesha kuwa Wanajangwani hao wanapocheza ugenini huwa ni moto wa kuotea mbali, kama ilivyokuwa dhidi ya Zanaco, ambayo walifanikiwa kuibana kwao, lakini ikiponzwa na bao waliloruhusu Uwanja wa Taifa na kupata sare ya 1-1.

Kwa upande wetu, tunaamini uwezekano wa Yanga kupata ushindi wa mabao mengi upo, lakini iwapo kila mmoja ndani ya klabu hiyo, kuanzia viongozi, wachezaji hadi wanachama, atatekeleza wajibu wake ipasavyo.

Zaidi ya hapo, tuitakie kila la heri Yanga kuelekea mchezo wao huo, tukiwa na matumaini kuwa MC Alger lazima watapigwa.

Mungu ibariki Yanga, Mungu ibariki Afrika.

 

 

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...

Sarpong ‘aua’ shabiki Simba

Na MWANDISHI WETU, MWANZA BAO la dakika ya 29 lililofungwa na Michael Sarpong wa Yanga juzi, limesababisha kifo cha...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -