Saturday, October 31, 2020

YANGA HAOOO UNGUJA KULIPA FADHILA KWA MALINDI

Must Read

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya...

Lulu Ringo, Dar es Salaam


Mabingwa wa kihistoria Yanga sc wanatarajiwa kushuka dimbani visiwani Unguja kesho Oktoba, 13 kucheza mchezo wa kirafiki na timu ya malindi ya Zanzibar mchezo utakaochezwa saa kumi kamili katika uwanja wa Amaan.

mchezo huo utakuwa ni mahususi kwaajili ya kumuaga meneja wa timu hiyo Narid Haroub ‘Cannavaro’ ambaye aliwahi kuichezea timu hiyo mwaka 2003-2005 kabla ya kusajiliwa na Yanga ya jijini Dar es Salaam mwaka 2006.

Meneja huyo mpya wa Yanga aliyeichezea timu hiyo kwa mafanikio takribani miaka 13 amesema licha ya kutamani kucheza na timu ya taifa ya zanzibar amefurahishwa na uongozi wa timu yake kukubali kwenda kucheza mechi hiyo visiwani zanzibar.

“Awali nilitamani ningeagwa Zanzibar kwa kucheza na timu ya Taifa ya huko lakini ratiba zake zimebana, nikaomba kucheza na Malindi wakakubali nashukuru uongozi wa Yanga kukubali kucheza mechi hii Zanzibar, niwasihi mashabiki waje kwa wingi kwani nami nitacheza kwenye mechi hiyo,” amefafanua Canavaro

Kabla ya msimu huu 2018/19 kuanza Cannavaro alitangaza kustaafu soka akiwa ndie nahodha mkuu wa Yanga, akiva jezi nambari 23 mgongoni. Yanga iliandaa mchezo dhidi ya Mawenzi Market ya Morogoro kwa ajili ya kumuaga lejendari huyo ambao ulimalizika kwa Yanga kushinda bao moja Kwa bila, beki huyo aliutumia mchezo huo kumkabidhi Kelvin Yondani kitambaa cha unahodha mkuu wa Yanga na Abdallah Shaibu ‘Ninja’ alimkabidhiwa jezi nambari 23 aliyokua akiitumia, Cannavaro aliwaamini mabeki hao wanaweza kuendeleza kile alichokianza katika klabu hiyo.

Licha ya Yanga kwenda Unguja kucheza mchezo huo kwaajili ya kumuaga Cannavaro baada ya kustaafu kucheza Soka, hapo awali klabu ya Yanga ilikua na taratibu ya kujiwekea kambi Pemba wanapokaribia kuanza Ligi Kuu Bara au timu inapokabiliwa ma mechi kubwa kama Simba na Yanga au zile za kimataifa ambapo visiwa hivyo vyote ninapatikana Zanzibar.

Tangu msimu huu kuanza mambo yamekua tofauti kwani kambi kubwa ya Yanga imekua ikiwekwa Morogoro hata katika mechi yao dhidi ya Simba kambi ilikua Morogoro jambo ambalo halikua lakawaidamn kwa vilabu hivi, ambapo Simba nao walijikita jijini Dar es salaam na mwisho wa mchezo hakuna aliefanikiwa kuliona lango la mwingine.

Yanga ikiwa chini ya Meneja Cannavaro imeshacheza michezo sita ya Ligi kuu ikifanikiwa kushinda michezo mitano na kutoa sare mchezo mmoja na kujikusanyia alama 16. Yanga itacheza na Alliance ya jijini Mwanza Octoba 20 katika uwanja wa Taifa.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika ujumbe kupitia ukurasa wake wa...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya kinda wa zamani wa timu...

Afua Suleiman afunguka ‘Utalijua Jiji’ ilivyompa ustaa mjini

NA JEREMIA ERNEST JINA alilopewa na wazazi wake ni Afua Suleiman na hata alipojitupa kwenye ulimwengu wa muziki wa...

Keche: Kundi maarufu Ghana linalowatamani Diamond, Kiba, Harmonize

JIACHIE na Staa Wako, wiki hii tumetua mpaka Accra, Ghana kwa kundi maarufu la muziki nchini humo, Keche linofanya vizuri na ngoma...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -