Wednesday, October 28, 2020

YANGA HAPONI MTU

Must Read

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya...

 

 

  • Takukuru ‘wafukua makaburi’ mkataba wa Quality Group, nembo ya Yanga
  • Mwalusako, Tiboroha waanika kila kitu; Baraka ang’aka, Madega mmh!

NA HUSSEIN OMAR


KITENDO cha Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), kuanza kuchimba mikataba iliyohusisha mambo ya fedha ndani ya Yanga tangu kuondoka madarakani kwa aliyekuwa Mwenyekiti wa klabu hiyo, Lloyd Nchunga mwaka 2008, hakitawaacha salama baadhi ya viongozi wa Wanajangwani hao.

Maofisa wa Takukuru walipiga hodi katika makao makuu ya Yanga yaliyopo makutano ya mitaa ya Twiga na Jangwani, Dar es Salaam na kudaiwa kufanya mahojiano na Mhasibu wa klabu hiyo, Jestina Ezekiel pamoja na viongozi wengine.

Pamoja na hayo, taasisi hiyo iliagiza kupewa namba za wachezaji wote wa Yanga na baadhi ya nyaraka za klabu hiyo ili kuzifanyia kazi kuona iwapo kuna vitendo vyovyote vya rushwa vilivyofanyika au ukwepaji kodi ya serikali.

Mmoja wa maofisa wa Takukuru ambaye hakupenda jina lake kutajwa gazetini, ameliambia gazeti hili kuwa tayari wameanza kufanyia kazi mikataba ya wachezaji waliosajiliwa tangu Nchunga alipoondoka madarakani mwaka 2008.

“Tunafanyia kazi mikataba ya wachezaji walioingia kipindi cha uongozi wa Yusuf Manji, lakini pia nembo ya Yanga jinsi ilivyokuwa ikitumika na Kampuni ya Quality Group kama kulikuwa na mkataba wowote unaonyesha Yanga walikuwa wanafainikaje nao.

“Lakini pia kuna sehemu inaonyesha Yanga ilikuwa ikilipwa milioni 12 kwa mwezi na Quality Group, je, Mamlaka ya Mapato (TRA) nao walikuwa wanapata kodi au vipi? Kuna mambo mengi bado tunaendelea kufuatilia, ikiwamo nembo ya Yanga ilivyokuwa ikitumiwa,” alisema.

BINGWA tangu juzi lilikuwa likimtafuta Mwenyekiti wa Yanga aliyemrithi Nchunga, lakini hakuweza kupokea simu pamoja na kuita kwa muda mrefu.

Gazeti hili lilipiga hodi kwa aliyewahi kuwa Mwenyekiti wa klabu hiyo, Imani Madega, ambaye pamoja na kutoa ushirikiano wa hali ya juu, lakini hakuweza kuzungumza lolote juu ya suala hilo kutokana na kubanwa na mazingira aliyokuwapo.

Lakini kwa upande wake, aliyekuwa Katibu Mkuu wa Yanga, Lawrence Mwalusako, alisema: “Awali Manji alikuwa akiisaidia Yanga kama mfadhili na baadaye alipokuwa Mwenyekiti, alisaidia sana klabu kama kiongozi, alitoa fedha kwa mapenzi yake mwenyewe kwasababu alitaka timu isikwame chini yake.

“Alisaidia usajili wa wachezaji, mishahara ya wafanyakazi na gharama nyingine nyingi tu. Kiuhalisia ninavyojua mimi, Quality Group imetoa fedha nyingi sana Yanga kuliko hata kile ilichokipata kutoka kwa klabu.

“Mdhamini anatoa hela (fedha) anavyotaka yeye, mnaweza kumuomba akawanyima, mnaweza kumuomba akawapa, (Manji) aliamua kutoa hela kwasababu anaipenda Yanga.”

Juu ya unaodaiwa mkataba baina ya Quality Group na Yanga, Mwalusako alifafanua: “Mkataba wa mwanzo ulikuwa ni wa Quality Group kuilipa Yanga kila mwezi na walifanya hivyo. Baada ya (yeye Mwalusako) kuondoka, sijui kama kulikuwa na makubaliano mengine mapya tofauti na hilo la Yusuf kuisaidia timu kama kiongozi, akiuchukulia huo kama ni wajibu wake kwa kuwa klabu haikuwa na fedha wala vyanzo vya mapato.

“Kuna kipindi (Manji) alisema Yanga nawakopesheni, lakini hakukuwa na mkataba, alisema anaidai Yanga mabilioni, lakini hakuonekana kuweka mkazo katika hilo kwa kuidai klabu.”

BINGWA lilimtafuta Jonas Tiboroha, ambaye naye aliwahi kuwa Katibu Mkuu wa Yanga, ambapo alisema: “Mkataba uliokuwapo ulikuwa ni wa Quality Media, ambao ulihusisha website na social media zote zilizomilikiwa na kampuni hiyo.

“Nilipokuwa Yanga, kuna mambo sikutaka kujihusisha nayo, hasa ya fedha, sijawahi kusaini cheki yoyote, hayo mambo aulizwe …(anamtaja mmoja wa viongozi wa Yanga), likiwamo suala la timu kuvaa jezi za Quality Group.”

Naye aliyewahi kuwa Kaimu Katibu Mkuu wa Yanga, Baraka Deusdedit, alisema: “Kwa sasa mimi si kiongozi wa Yanga, ofisi ina kumbukumbu, waulizeni waliopo ofisini kwa sasa, mimi siwezi kuzungumzia, kwani si kiongozi wa Yanga, sifahamu lolote.”

Habari kutoka ndani ya Yanga zinasema kuwa baadhi ya vigogo wa klabu hiyo wameanza kupatwa na mchecheto wakihofia kuwakuta kama ya viongozi wa Simba wanaotuhumiwa kwa utakatishaji fedha.

“Hali ni mbaya, tangu hizi habari zitoke hakuna tena siri, watu matumbo joto. Unajua tangu Mwenyeikiti atangaze kujiuzulu, hakuna ripoti kamili ya mapato na matumizi, mambo yanakwenda holela holela na kitu kingine ni mikataba ya ovyo waliyoingia wachezaji na klabu pamoja na mkataba wa SportPesa,’’ alisisitiza mtoa habari wetu huyo.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika ujumbe kupitia ukurasa wake wa...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya kinda wa zamani wa timu...

Afua Suleiman afunguka ‘Utalijua Jiji’ ilivyompa ustaa mjini

NA JEREMIA ERNEST JINA alilopewa na wazazi wake ni Afua Suleiman na hata alipojitupa kwenye ulimwengu wa muziki wa...

Keche: Kundi maarufu Ghana linalowatamani Diamond, Kiba, Harmonize

JIACHIE na Staa Wako, wiki hii tumetua mpaka Accra, Ghana kwa kundi maarufu la muziki nchini humo, Keche linofanya vizuri na ngoma...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -