Wednesday, September 30, 2020

Yanga: Hatuna mpango na wasugua benchi Msimbazi

Must Read

KISA KONA YA CARLINHOS… ...

NA ZAINAB IDDY BAO la Yanga lililofungwa na Lamine Moro juzi katika mchezo dhidi...

HUYU MUGALU ATAWALAZA WATU NA VIATU TU!

NA ONESMO KAPINGA HAKIKA sijapata utamu wa mshambuliaji mpya wa Simba, raia wa DR...

Wachezaji Gwambina wapewa muda

NA ZAINAB IDDY KOCHA wa timu wa  Gwambina, Fulgence Novatus, amesema amewapa muda wachezaji wake ...

NA ZAINAB IDDY

UONGOZI wa Yanga, umesema hauna mpango wa kusajili wachezaji wanasugua benchi katika klabu ya Simba kwa ajili ya msimu ujao wa Ligi Kuu Tanzania Bara na michuano mingine.

Kauli ya uongozi wa Yanga, imekuja baada ya kuwapo kwa taarifa kuwa wanapango wa kumrejesha beki wao wa zamani Gadiel Michael anayekipiga Simba.

Gadiel alijiunga na Simba msimu uliopita kwa mkataba wa miaka miwili akitokea Yanga, lakini tangu atue Msimbazi amekuwa akipata ushindani wa namba kutoka kwa Mohamed Hussein ‘Tshabalala’.

Kutokana na sababu hiyo, imeelezwa Gadiel ameomba kuondoka klabu ya Simba kwa lengo la kutaka kurejea Yanga.

Akizungumza na BINGWA jana, Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano wa Yanga, Hassan Bumbuli, alisema hawana mpango wa kumsajili mchezaji yeyote kutoka Simba ambaye anasugua benchi katika timu hiyo.

“Yanga tunaonekana masikini sawa,lakini hatujafikia umaskini wa kuchukua makapu ya Simba, ni bora tukachukua wachezaji kutoka timu nyingine na kuwajenga upya.

“Kama tutahitaji kuchukua mchezaji kutoka Simba, basi jua atakuwa yule mwenye kiwango kizuri kwa maana yupo kikosi cha kwanza ambaye atawaumiza roho, lakini sio mtu asiye na namba ndiye aje kwetu,” Bumbuli

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

KISA KONA YA CARLINHOS… ...

NA ZAINAB IDDY BAO la Yanga lililofungwa na Lamine Moro juzi katika mchezo dhidi...

HUYU MUGALU ATAWALAZA WATU NA VIATU TU!

NA ONESMO KAPINGA HAKIKA sijapata utamu wa mshambuliaji mpya wa Simba, raia wa DR Congo, Chris Mugalu,kutokana na jinsi...

Wachezaji Gwambina wapewa muda

NA ZAINAB IDDY KOCHA wa timu wa  Gwambina, Fulgence Novatus, amesema amewapa muda wachezaji wake  ili aweze kutathimini kiwango cha...

Kisu amfunika vibaya Manula

NA ZAINAB IDDY KIPA  wa timu ya Azam, David Kisu, amemfunika Aishi Manula  wa Simba kutokana na kutoruhusu...

Zahera awapa Simba taji mapema

NA ZAINAB IDDY BAADA ya Gwambina kufungwa mabao 3-0 na Simba  katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -