Sunday, November 29, 2020

YANGA IJIANDAE VYEMA KIMATAIFA

Must Read

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali...

YANGA imepangwa na MC Algers ya Algeria katika hatua ya mtoano ya timu 32 za Kombe la Shirikisho barani Afrika, kufuatia kutolewa kwenye michuano ya Klabu Bingwa Afrika na Zanaco ya Zambia.

Ili kusonga mbele kwenye hatua ya makundi, Yanga wanahitaji kuitoa timu hiyo ya Algeria baada ya mechi zake zote mbili za ugenini na nyumbani zitakazochezwa baadaye mwezi ujao.

Ni wazi kwamba, Yanga kupata ushindi dhidi ya timu hiyo si kazi rahisi hata kidogo hasa kutokana na ukweli kwamba klabu hiyo ya Jangwani ya jijini Dar es Salaam imekuwa haina historia nzuri ya kuzitoa timu za Uarabuni au timu kutoka Kaskazini mwa Afrika.

Ni kutokana na hali hiyo ndiyo maana BINGWA tunautaka uongozi wa Yanga kuhakikisha unafanya maandalizi ya kutosha kwa timu yao ili kupata ushindi mzuri hasa katika mechi ya nyumbani ambayo itawawezesha kuvuka katika hatua hiyo na kuendeleza rekodi yake ya kushiriki hatua ya makundi kwa msimu wa pili mfululizo.

BINGWA tunaamini kwamba, soka limebadilika sana hivi sasa ndiyo maana leo hii tunashuhudia timu kubwa zikigaragazwa na timu ndogo na kuondoshwa kwenye michuano ya Afrika, hivyo Yanga nayo inaweza kufuta uteja kwa timu za Waarabu kwa kuanza kuiondosha timu hiyo.

Kwa kufahamu kwamba hiyo si kazi rahisi kutokana na hali ya kikosi cha Yanga na matatizo yao ya kiufundi ya ndani ya uwanja ambayo yamekuwa yakionekana, ndiyo maana BINGWA tunautaka uongozi na benchi la ufundi la timu hiyo kuhakikisha wanapata muda mzuri wa kuyafanyia kazi mapungufu ya muda mrefu ambayo yamekuwa yakiitafuna timu hiyo.

Ni vyema maandalizi ya mchezo huo yakaanza mara moja tena kwa umakini mkubwa, tunaamini kwamba kocha Lwandamina amekuwa na uzoefu mzuri wa kucheza mechi na timu za Waarabu hivyo atakuwa na dozi maalumu itakayowawezesha wachezaji wake kupata ushindi na kujenga historia nyingine kwa klabu hiyo kwenye mashindano ya kimataifa.

Kila la kheri Yanga katika maandalizi hayo.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...

Sarpong ‘aua’ shabiki Simba

Na MWANDISHI WETU, MWANZA BAO la dakika ya 29 lililofungwa na Michael Sarpong wa Yanga juzi, limesababisha kifo cha...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -