Sunday, November 29, 2020

YANGA ILIKUFA DAR MAZISHI LUSAKA

Must Read

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali...

NA ONESMO KAPINGA

YANGA imefika mwisho kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika, baada ya kutolewa na Zanaco ya Zambia kufuatia matokeo ya sare tasa waliopata katika mchezo wa marudiano uliochezwa juzi kwenye Uwanja wa Mashujaa, Lusaka.

Zanaco ilifanikiwa kusonga mbele kwa faida ya bao la ugenini walilolipata katika mchezo wa kwanza uliochezwa kwenye Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam.

Katika mchezo huo uliopigwa Machi 11, mwaka huu, iliruhusu bao wakati walipotoka sare ya bao 1-1 na kuonekana imekufa Dar es Salaam na mazishi Lusaka.

Yanga ilifanya kosa kubwa la kuruhusu bao kwenye uwanja wao wa nyumbani na ndilo lililoivusha Zanaco katika hatua inayofuata ya ligi hiyo.

Baada ya matokeo hayo, Yanga ilihitaji kupata ushindi katika mchezo wa marudiano, hivyo kushindwa kukabiliana na fitina za soka za ugenini.

Wenyeji Zanaco walikuwa wanahitaji matokeo hayo ili waweze kusonga mbele, baada ya Yanga kuwarahisishia kazi jijini Dar es Salaam.

Historia inaonyesha kwamba kwenye michuano ya kimataifa, Yanga inashindwa kujipanga kuanzia mechi zake zinazochezwa nyumbani.

Katika misimu miwili iliyopita, Yanga ilikuwa na rekodi mbaya kwenye michuano ya kimataifa, licha ya kwamba baadhi ya mechi ilikuwa inapata ushindi mwembamba nyumbani, lakini ilikuwa inafungwa inapokuwa ugenini.

Si mara ya kwanza kwa Yanga kutolewa kwenye michuano wakiwa ugenini na sababu kubwa inashindwa kujipanga na fitina za ugenini.

Ni tofauti kidogo na timu kama Simba  ambayo imewahi kusonga mbele kwenye michuano ya kimataifa ikiwa ugenini.

Simba ilisonga mbele kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika, pale ilipoivua ubingwa Zamalek ya Misri mwaka 2003 nchini kwao na kutinga robo fainali.

Katika mchezo wa kwanza uliochezwa kwenye Uwanja wa Taifa, kwa sasa Uhuru, Simba ilishinda bao 1-0, lakini Zamalek ilipata matokeo kama hayo nchini kwao  na matokeo kuwa sare ya bao 1-1, lakini Simba walisonga mbele kwa changamoto ya penalti.

Lakini iliweza kutoa Setif ya Algeria kwenye michuano ya Kombe la Shirikisho katika msimu wa 2011/12, baada ya kushinda mabao 2-0 katika mchezo wa kwanza uliochezwa kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Timu hizo ziliporudiana ugenini, Simba ilifungwa mabao 3-1, hivyo kusonga mbele kutokana na faida ya bao la ugenini lililofungwa na mshambuliaji Mganda, Emmanuel Okwi dakika za majeruhi.

Ukiangalia ushiriki wa Yanga katika msimu uliopita wa michuano ya kimataifa, haikuwa na matokeo mazuri kwenye uwanja wa nyumbani.

Ilianza kucheza ugenini na Cercile de Joachim ya nchini Mauritius, ambako ilishinda mabao 2-0 lakini ilionyesha kiwango kibovu waliporudiana kwenye Uwanja wa Taifa kwa Yanga kushinda bao 1-0.

 

Baadaye ilicheza na APR ya Rwanda na kuibuka na ushindi wa mabao 2-1  wakiwa ugenini, lakini ilitoka sare ya kufunga bao 1-1 waliporudiana kwenye Uwanja wa Taifa.

Rekodi ya Yanga kutofanya vizuri ilidhihirika hata ilipofanikiwa kuingia hatua ya makundi ya robo fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika msimu uliopita.

Yanga ambao waliingia kwenye Michuano ya Kombe la Shirikisho baada ya kutolewa na Al Ahly ya Misri kwa jumla ya mabao 3-2, iliendeleza rekodi mbaya pale iliposhindwa kupata matokeo mazuri nyumbani.

Katika mechi zao za makundi, ilishinda bao 1-0 dhidi ya Mo Bejaia ya Algeria  ambayo ilikuwa imefungwa bao 1-0 katika mchezo wa kwanza uliochezwa ugenini.

Lakini ilifungwa bao 1-0 na TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) kwenye Uwanja wa Taifa, kabla ya kutoka sare ya bao 1-1 Meadema ya Ghana wakiwa nyumbani.

Kutokana na rekodi yao, Yanga ilifungwa mechi zote iliyocheza ugenini, pale ilipopoteza kwa  mabao 3-1 dhidi ya  Meadema ya Ghana, kisha mabao 3-1 na TP Mazembe.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...

Sarpong ‘aua’ shabiki Simba

Na MWANDISHI WETU, MWANZA BAO la dakika ya 29 lililofungwa na Michael Sarpong wa Yanga juzi, limesababisha kifo cha...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -