Sunday, October 25, 2020

YANGA ‘IMENAJISI’ MAFANIKIO YA CANNAVARO

Must Read

Fati aweka rekodi Barcelona

CATALUNYA, Hispania ANSU Fati ameweka rekodi ya mchezaji kinda wa kwanza kufunga mabao...

Lampard amshika mkono Silva

MANCHESTER, England KOCHA wa Chelsea, Frank Lampard, amesema atamtumia, Thiago Silva, katika mechi nyingi msimu huu licha ya...

Tuchel awatolea uvivu Mbappe, Neymar

PARIS, Ufaransa KOCHA wa PSG, Thomas Tuchel, amechukizwa na kiwango kibovu walichoonyesha mastaa wa timu hiyo, Kylian...

NA HUSSEIN OMAR


MWISHONI mwa wiki iliyopita, Klabu ya Yanga iliandaa tamasha maalumu la kumuaga aliyekuwa nahodha wa kikosi hicho, Nadir Haroub ‘Cannavaro,’ ambaye amedumu ndani ya kikosi cha timu hiyo kwa miaka 12.

Amecheza soka zaidi ya miaka 20, akizitumikia klabu mbili tu za hapa hapa nchini Tanzania, ambazo ni Malindi FC ya Zanzibar na Klabu ya Yanga, ambayo kaitumikia kwa muda mrefu zaidi.

Akiwa Malindi, Cannavaro alifanikiwa kuitumikia kwa kipindi cha miaka miwili kuanzia mwaka 2003-2005, akicheza michezo 36.

Baadaye Yanga waliamua kumrejesha Cannavaro mwaka 2006, ambapo alidumu  mpaka alipoamua kustaafu akifanikiwa kucheza michezo zaidi ya 250 na kuifungia mabao saba timu yake hiyo.

Licha ya kuwa mzaliwa wa Zanzibar, Cannavaro aliitumikia timu ya taifa ya Tanzania kuanzia mwaka 2006, akicheza zaidi ya michezo 51, lakini pia wakati huo huo alikuwa akiitumikia timu ya Zanzibar Heroes.

Kwa muda wote huo, Cannavaro akiwa Yanga alifanikiwa kuwasaidia Wanajangwani hao kutwaa mataji 8 ya Ligi Kuu kuanzia mwaka 2006, 2008, 2009, 2011, 2013, 2015, 2016 na 2017.

Pia akiisaidia kutwaa taji la Ngao ya Jamii kwa nyakati nne tofauti, kuanzia mwaka 2010, 2013, 2014 na 2015. Kagame Cup mara mbili, mwaka 2011 na 2012, Super Cup mara mbili, mwaka 2007 na 2009 na Kombe la Azam Sports Federation mara moja mwaka 2016/17.

Katika mchezo huo maalumu wa kirafiki wa kumuaga mchezaji huyo, uliochezwa kwenye Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro, Yanga waliibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Mawenzi FC.

Cannavaro ameweka rekodi ya kuwa Mzanzibari wa kwanza kupata mafanikio makubwa zaidi, lakini pia kudumu katika kikosi cha Yanga kwa muda mrefu zaidi.

Beki huyo alijiunga na Yanga akitokea katika timu ya KMKM ya Visiwani Zanzibar, ameweka rekodi ya kuwa mchezaji aliyedumu kwa muda mrefu zaidi katika timu hiyo yenye maskani yake mitaa ya Twiga na Jangwani.

Cannavaro alicheza mechi yake ya mwisho Jumapili wiki iliyopita kwa dakika chache na uongozi wake ulipanga kuistaafisha jezi yake, lakini mwenyewe ameamua kumkabidhi beki mwenzake, Abdallah Shaibu ‘Ninja’.

Akiwa Yanga, Cannavaro alikuwa akitumia jezi namba 23, aliyoivaa kuanzia anatua klabuni hapo mpaka anastaafu kucheza soka na kupewa cheo cha umeneja.

Cannavaro ni nembo ya Klabu ya Yanga kutokana na utiifu wake, ambapo ameweza kuvumilia mengi katika kipindi chote alichoitumikia timu hiyo yenye maskani yake Mtaa wa Twiga na Jangwani, jijini Dar es Salaam.

Mchezaji wa aina hii ambaye ameisaidia timu kubeba mataji lukuki hakupaswa kuagwa katika mchezo mdogo dhidi ya Mawenzi, ambayo haina jina kubwa kama ilivyo Yanga, ambayo ameitumikia kwa mafanikio makubwa.

Cannavaro alipaswa kuandaliwa mechi maalumu yenye mashiko ya kumuaga na si kumuaga ‘kihuni’ kama walivyofanya juzi katika Uwanja wa Jamhuri, mjini Morogoro, kwa kucheza mechi na timu ya daraja la chini kumuaga nahodha huyo.

Sote tunajua kwamba Cannavaro amevumilia mengi katika vipindi vyote vya raha na shida, lakini hajatendewa haki, ilipaswa itafutwe mechi moja kubwa ambayo ingechezwa katika Uwanja wa Taifa, ili mashabiki wamiminike kwa wingi kumuaga shujaa wao ambaye aliyatoa maisha yake kwa Yanga.

Yanga imefanya makosa makubwa kumuaga nahodha huyo mwenye heshima kihuni kupitia mchezo huo dhidi ya Mawenzi. Naiheshimu timu hiyo, lakini ukweli utabaki haikustahili kuwa ya kumuagia Cannavaro, ambaye ni nahodha wa zamani wa timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’.

Kitendo cha kumuaga nahodha huyo kihuni ni kama kumdharau na kupuuza mafanikio yake yote aliyoipa timu hiyo kwa nyakati tofauti. Yanga ilipaswa kuiga mfano wa Simba, ambayo imekuwa ikiwaaga manahodha wao kwa heshima.

Ikumbukwe Yanga hata baadhi ya manahodha wake wawili, Fred Mbuna na Shedrack Nsajigwa haikuwa kuwaaga kabisa. Nini kinawasibu Yanga katika hili.

Rejea namna walivyomuaga straika na nahodha wao wa zamani, Mussa Hassani ‘Mgosi’ kwa heshima kubwa kupitia mchezo wa kimataifa dhidi ya URA ya Uganda.

Mchezo huo uliopigwa Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam, ulimalizika kwa sare ya bao 1-1.

Yanga hawakupaswa kuwa na haraka ya kumuaga nguli huyo, bado walikuwa na muda mwingi wa kufanya hivyo hata kama hawako vizuri kiuchumi wangeweza kulitumia jina la Cannavaro kwa ajili ya kujipatia kipato.

Lakini haya yote yanashindikana kutokana na timu hiyo kutokuwa na viongozi wabunifu wenye uwezo mkubwa wa kubuni mipango ya kuiingizia mapato klabu hiyo.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Fati aweka rekodi Barcelona

CATALUNYA, Hispania ANSU Fati ameweka rekodi ya mchezaji kinda wa kwanza kufunga mabao...

Lampard amshika mkono Silva

MANCHESTER, England KOCHA wa Chelsea, Frank Lampard, amesema atamtumia, Thiago Silva, katika mechi nyingi msimu huu licha ya kuwa na umri wa miaka...

Tuchel awatolea uvivu Mbappe, Neymar

PARIS, Ufaransa KOCHA wa PSG, Thomas Tuchel, amechukizwa na kiwango kibovu walichoonyesha mastaa wa timu hiyo, Kylian Mbappe na Neymar, kwenye mechi...

IBRA:Kifaa kipya Konde Gang aliyetembea kwa mguu kumwinda Harmonize

NA BRIGHITER MASAKI UKITAJA vijana wanaofanya vizuri katika mziki wa bongo fleva, huwezi kukosa kumtaja msanii chipukizi anayefahamika zaidi...

Jay-Z: Mama aliingilia bifu langu na Nas

-Z: Mama aliingilia bifu langu na Nas New York, Marekani HAKUNA shabiki wa Hip hop asiyelifahamu...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -