Sunday, November 29, 2020

YANGA KICHEKO

Must Read

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali...

EZEKIEL TENDWA NA MAREGES  NYAMAKA

KAMA unacheza na Yanga halafu ukawapeleka kwenye uwanja mzuri ‘kapeti’, wewe andika maumivu, kwani watakujeruhi tu na hivyo ndivyo Zanaco walivyojimaliza katika mchezo wao wa leo wa marudiano Ligi ya Mabingwa Afrika.

Kama huamini rudisha picha nyuma uangalie kiwango cha hali ya juu Yanga walichokionyesha dhidi ya Al Ahly msimu uliopita, ambapo Ligi ya Mabingwa Afrika  kama si bao la jioni sana lililofungwa na wenyeji wao hao mambo yangekuwa mengine.

Sasa sikia hii. Wakati Yanga wakishuka uwanjani leo kutafuta ushindi wa aina yoyote ili kuvuka hatua inayofuata, wenyeji wao Zanaco FC ni kama wamejiroga baada ya kuamua mchezo huo uchezwe Uwanja wa Taifa wa Mashujaa mjini Lusaka.

Mara kadhaa kwa asilimia kubwa Yanga wanapokuwa uwanja wa ugenini huwa wanapambana mpaka dakika za mwisho, hivyo Zanaco kuchagua kuutumia uwanja huo mzuri unaokadiriwa kuingiza watazamaji 60,000, ni sawa na kuwatengenezea njia Wanajangwani hao.

Uzuri wa uwanja huo wa Mashujaa ndio uliolifanya Shirikisho la Soka barani Afrika (CAF) kuruhusu kutumika kwa michuano ya Vijana wenye umri chini ya miaka 20, iliyomalizika hivi karibuni kwa wenyeji Zambia kuibuka kidedea walipowafunga Senegal mabao 2-0.

Mbali na uwanja huo, pia Yanga walipata mapokezi mazuri kutoka kwa wenyeji wao hao tofauti na sehemu nyingine, ambapo mara kadhaa wamekuwa wakifanyiwa figisufigisu hiyo ikiashiria kuwa wachezaji wa Wanajangwani hao hawatakuwa na  chembe ya mawazo hasi ya kuwatoa mchezoni.

Mabingwa hao watetezi wa  Ligi Kuu Tanzania Bara waliwasili mapema jana na kupata mapokezi mazuri, ambapo jioni yake walitarajiwa kujifua kwa ajili ya kujiweka fiti kwa mpambano wa leo huku wachezaji wakiwa na morali ya hali ya juu.

Faida kubwa ambayo Yanga wanayo ni kwamba kikosi hicho kinaongozwa na Mzambia George Lwandamina ambaye anaijua Zanaco nje ndani, wakati huo alipokuwa akiinoa Zesco walipokutana katika mchezo wa mwisho kabla ya kutua Tanzania aliwatoa nishai akiwabamiza bao 1-0.

Zanaco wanapokuwa katika uwanja wao wa nyumbani wanaonekana si wa kutisha sana, kwani katika michezo minne waliyocheza walifanikiwa kushinda miwili dhidi ya Forest Rangers mabao 3-0 na dhidi ya Lumwana Radiants, bao 1-0 mingine wakitoka sare.

Katika mchezo huo wa leo licha ya kwamba Yanga watakosa huduma ya mshambuliaji wao Donald Ngoma, lakini hilo halitakuwa tatizo kwani kikosi chao ni kipana ambapo kwa vyovyote wanaweza kuibuka na ushindi utakaowafanya kusonga mbele.

Yanga watatakiwa kuhakikisha wanashinda leo ushindi wa aina yoyote au sare ya zaidi ya mabao 2-2, ili kusonga mbele hatua inayofuata kwani katika mchezo wa kwanza uliochezwa Uwanja wa Taifa, Wanajangwani hao walilazimishwa sare ya kufungana bao 1-1.

Hata hivyo, kocha wa zamani wa kikosi hicho, Hans van der Pluijm ambaye kwa sasa ameanguka saini ya miaka miwili na Singida United ambayo msimu ujao itashiriki ligi kuu, alisema Yanga wanao uwezo mkubwa wa kushinda kama wakiamua kupambana kisawasawa.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...

Sarpong ‘aua’ shabiki Simba

Na MWANDISHI WETU, MWANZA BAO la dakika ya 29 lililofungwa na Michael Sarpong wa Yanga juzi, limesababisha kifo cha...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -