Saturday, November 28, 2020

YANGA KUIVAA KIUGUMU MC ALGER

Must Read

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali...

NA WINFRIDA MTOI

KOCHA msaidizi wa Yanga, Juma Mwambusi, amesema kuongezeka kwa majeruhi katika kikosi chao ni pigo na wataivaa kiugumu MC Alger ya Algeria katika mchezo wa Kombe la barani Afrika utakaochezwa wiki hii kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Kikosi cha Yanga kinakabiliwa na majeruhi wengi baada ya Mzambia Justine Zullu kuumia katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Azam uliochezwa juzi, Uwanja wa Taifa na wao kushinda bao 1-0.

Wachezaji wengine majeruhi ni  washambuliaji Amis Tambwe, Donald Ngoma, kiungo Thabani Kamusoko na  beki Pato Ngonyani.

Akizungumza na BINGWA juzi, Mwambusi alisema majeruhi walionao wamezidi kupunguza idadi ya wachezaji muhimu wa kikosi chao cha  kwanza.

Mwambusi alisema hali hiyo imekuwa ikiwagharimu mara nyingi ukizingatia wameanza vibaya katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika na kutolewa mapema.

“Inasikitisha sana kuongezeka kwa majeruhi katika kikosi chetu, tunazidi kuwapunguza watu na tunakwenda kwenye michuano muhimu ambayo lengo letu ni kufanya vizuri baada ya kuanza vibaya,” alisema Mwambusi.

Mwambusi alisema malengo yao ni kutaka kufika mbali katika michuano hiyo, lakini wamekuwa wakiandamwa na majeraha na ni pigo.

Alisema wachezaji watano majeruhi ambao wanacheza kikosi cha kwanza, hivyo wanahitaji kufanya kazi kubwa  kurudi katika hali ya kawaida.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...

Sarpong ‘aua’ shabiki Simba

Na MWANDISHI WETU, MWANZA BAO la dakika ya 29 lililofungwa na Michael Sarpong wa Yanga juzi, limesababisha kifo cha...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -