Saturday, November 28, 2020

YANGA KUWAMALIZA WAARABU KWA MIL 600/-

Must Read

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali...

NA HUSSEIN OMAR,

WAKATI kikosi cha timu ya MC Alger ya Algeria kilitarajiwa kuwasili jana usiku tayari kwa mchezo wao dhidi Yanga kuwania Kombe la Shirikisho barani Afrika, nyota wa Wanajangwani hao wameapa kufia uwanjani ili kupata ushindi kuhakikisha wananyakua kitita cha zaidi ya Sh milioni 600.

Mchezo huo utakaochezwa kesho kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, utazikutanisha timu hizo ambazo zinawania kufuzu hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika.

Wakizungumza na BINGWA wachezaji, Haruna Niyonzima na Kelvin Yondani, walisema wameamua kuyasahau kwa muda matatizo yao na kufanya kweli na kuwatoa Waarabu hao.

“Ni kweli tuna matatizo ya kifedha, lakini hayo hatuyapi nafasi tumepiga hesabu na tumeona kwamba kufuzu hatua inayofuata ni ni muhimu sana, tumekubaliana kufanya kazi, unajua ukishaifanya kazi yako vizuri hata bosi atakuwa na moyo wa kukulipa au kukupa chochote kitu,” alisema Niyonzima.

Aliongeza kuwa Yanga ni klabu kubwa ambayo ina matajiri wengi wanaopenda kuona timu ikifanya vizuri na kusisitiza watacheza kufa, kupona kuhakikisha wanaingia hatua ya makundi.

Alisema endapo watashinda mchezo huo na kuingia hatua ya makundi wanaamini matajiri wengi watajitokeza kuwatunza fedha lakini pia kumbuka ukiingia hatua ya makundi kuna mzigo watapata kutoka CAF.

Kwa upande wake straika wa timu hiyo, Malimi Busungu, alisema wapo tayari kwa mpambano huo kutokana na wao kuendelea na mazoezi makali katika Uwanja wa Chuo cha Polisi Kurasini jijini Dar es Salaam, kujiandaa na mchezo huo.

“Tupo vizuri kama walivyokufa Azam juzi ndivyo watakavyokufa Waarabu siku hiyo, tumewaona na tutajitahidi sana, akili zetu sasa ni kwenye hizo dola za CAF na hizo ndizo tunazitumia kama silaha yetu kuwaua Waarabu,” alisema Busungu.

Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Yanga, Boniface Mkwasa, aliliambia BINGWA maandalizi yote kuelekea katika mchezo huo wa kesho yamekamilika kwa asilimia 90 na kuwapongeza wachezaji wake kwa umoja walionao.

“Sisi kama viongozi tumemaliza majukumu yetu ya ushindi kwa zaidi ya asilimia 90, kazi kubwa imebaki kwao wachezaji nawaomba wacheze, wajitoe tushinde mwisho wa siku kuna mambo mazuri zaidi yanakuja kama walivyosema wao wenyewe,” aliongeza Mkwasa.

Katika hatua nyingine Mwenyekiti wa Kamati ya Mashindano ya timu hiyo, Paulo Malume, alisema wao kwa upande wao wamekamilisha maandalizi yote ya ushindi katika mchezo huo na kuwataka wachezaji kujitoa kwa ajili ya kushinda kwa mabao mengi hapa nyumbani ili iwe rahisi kuvuka.

“Tumekamilisha mipango yote ya ushindi, kimsingi pia tumewaahidi wachezaji japo kifuta jasho kidogo endapo wataibuka na ushindi,” alisema Malume.

Kikosi cha wachezaji 20 na viongozi 10 cha MC Alger ya Algeria kilitarajiwa kuwasili nchini jana tayari kwa pambano hilo la raundi ya kwanza ya michuano ya Kombe la Shirikisho barani Afrika.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...

Sarpong ‘aua’ shabiki Simba

Na MWANDISHI WETU, MWANZA BAO la dakika ya 29 lililofungwa na Michael Sarpong wa Yanga juzi, limesababisha kifo cha...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -