Wednesday, October 21, 2020

YANGA MECHI MOJA FAIDA MBILI

Must Read

Director Kenny: Harmonize alinipeleka WCB nikafanya video ya Lavalava

MWONGOZAJI bora wa video nchini, Kenned Sanga a.k.a Derector Kenny kutoka Zoom Extra, ametua   hapa Jiachie na...

Rogers mwanamuziki anayevutiwa na Marijani

NA JEREMIA ERNEST BONGO Star Search (BSS), ni shindano lililofanikiwa kuibua vipaji vingi vya...

Ihefu, Azam patachimbika Sokoine, Katwila ndani

NA ASHA KIGUNDULATIMU ya Ihefu inatarajia kushuka uwanjani kucheza na Azam ukiwa ni mchezo wa Ligi Kuu...

HUSSEIN OMAR NA ZAINAB IDDY

UNAIKUMBUKA mechi ya kirafiki waliyocheza Yanga dhidi ya JKU ya Zanzibar mwanzoni mwa mwezi uliopita kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam? Kama hufahamu, mchezo ule umekuwa muhimu mno kwa mabingwa hao wa Tanzania Bara.

Unajua kwanini? Kuna sababu mbili; kwanza Yanga walifanikiwa kupata mchezaji ambaye aliwasumbua mno akiwafunga mabao mawili, Emmanuel Martin na mwisho wa siku, walifikia uamuzi wa kumsajili.

Mshambuliaji huyo amekuwa mchezaji muhimu mno ndani ya kikosi cha Yanga, akifanikiwa kuingia kwenye ‘first eleven’ ya kocha George Lwandamina.

Lakini ukiachana na faida hiyo, usajili wa Martin unaonekana kuwapa faida nyingine Yanga visiwani Zanzibar inakoendelea michuano ya Kombe la Mapinduzi kutokana na kupata sapoti ya mashabiki wengi zaidi ya timu yoyote ya Tanzania Bara.

Japo Martin ni mwenyeji wa Bara, lakini kwa kuwa ametoka katika ‘mikono’ ya JKU, Wazanzibari wanamwona kama mwenzao ukizingatia kuwa Yanga imeonekana kuwa timu ambayo kikosi chao cha kwanza kina wachezaji watano kutoka Zanzibar, wengine wakiwa ni Haji Mwinyi, Said Juma Makapu, Nadir Haroub ‘Cannavaro’ na Matheo Anthony.

Na kwa hali inavyoonekana huko Zanzibar, mashabiki wengi wa soka wa visiwani humo wamekuwa wakitamani kuiona Yanga ikicheza kila siku ili wawaone vijana wao wanavyokinukisha ndani ya kikosi hicho na mwisho wa siku kubeba ubingwa kutuma ujumbe kwa klabu nyingine kuwa visiwani humo kumesheheni vipaji vya soka.

Wakati Yanga wakiwa na idadi hiyo ya wachezaji kutoka Zanzibar, Azam wanao watatu ambao ni Aggrey Morris, Mcha Hamisi na Mwadini Ally, wakati Simba wakikosa hata mmoja.

Na leo wakati Yanga ikishuka dimbani kuvaana na Azam katika mchezo wa michuano hiyo ya Kombe la Mapinduzi, mashabiki wa soka visiwani humo watamiminika kwa wingi kwenye Uwanja wa Amaan, kuona ‘ndugu’ zao waliopo katika kikosi cha Lwandamina watafanya nini.

Hata hivyo, mchezo huo ni wa kukamilisha ratiba kwa Yanga kwani tayari imetinga nusu fainali baada ya kufikisha pointi sita kutokana na kushinda mechi zao zote mbili za kwanza.

Kwa upande wao, Azam watalazimika kushinda ili kutinga nusu fainali na kwamba iwapo watapoteza mchezo, wanaweza kujikuta wakiiaga michuano hiyo kwani hadi sasa wana pointi nne tu.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Director Kenny: Harmonize alinipeleka WCB nikafanya video ya Lavalava

MWONGOZAJI bora wa video nchini, Kenned Sanga a.k.a Derector Kenny kutoka Zoom Extra, ametua   hapa Jiachie na...

Rogers mwanamuziki anayevutiwa na Marijani

NA JEREMIA ERNEST BONGO Star Search (BSS), ni shindano lililofanikiwa kuibua vipaji vingi vya wanamuziki wa Tanzania ambao miongoni...

Ihefu, Azam patachimbika Sokoine, Katwila ndani

NA ASHA KIGUNDULATIMU ya Ihefu inatarajia kushuka uwanjani kucheza na Azam ukiwa ni mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara  (VPL), utakaochezwa leo...

Mugalu atema cheche Simba

NA ASHA KIGUNDULA MSHAMBULIAJI wa Simba, Chris Mugalu, amesema wanakwenda mkoani Rukwa kupambana na kupata ushindi katika mchezo wao...

Malale aitisha Yanga

NA ZAINAB IDDY KOCHA Mkuu wa timu ya Polisi Tanzania, Malale Hamsini, amezisikia sifa za kocha mpya wa Yanga,...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -