Wednesday, October 28, 2020

Yanga mtafanya kosa kubwa mkimtema Pluijm

Must Read

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya...

 

KATI ya mambo ambayo mara kadhaa yamekuwa yakiwachanganya wachezaji ni leo kuwa na kocha huyu na kesho wanashangaa kubadilishiwa mwingine na kubadilishiwa mifumo, hali inayowaacha njia panda.

Kwa kawaida kila kocha ana mfumo na tabia zake, hivyo anapobadilishwa na kuletewa mwingine maana yake ni kwamba, wanaanza upya na bahati mbaya iwe huyo anayeletwa hajui mazingira ya ligi husika.

Kama unadhani natania, angalia jinsi Simba walivyoteseka kwa misimu minne mfululizo na ujiulize mwenyewe ni makocha wangapi ambao wamepita mpaka sasa katika kikosi hicho ambacho kipo chini ya kocha mkuu wake, Joseph Omog na nini kimefanyika cha maana.

Simba inayo misimu minne mfululizo bila kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara na imekuwa hodari kutimua na kuajiri makocha wapya, jambo ambalo linaweza kuwa sababu ya kushindwa kufanya vizuri, achilia mbali matatizo yao ya migogoro iliyokuwepo.

Baadhi ya makocha ambao walitimuliwa na Simba ni kocha mzawa Abdallah Kibaden, wakati huo akiwa na msaidizi wake, Jamhuri Kihwelu ‘Julio’, akaja Zdravko Logarusic na baadaye tukasikia tena Patrick Phiri ametambulishwa kama kocha mkuu wa klabu hiyo.

Wakati wengi tukiamini kwamba Phiri atapewa muda wa kuiongoza Simba na kuiletea mafanikio, ghafla analetwa Goran Kopunovic, ambaye naye aliondoka baada ya kumaliza mkataba wake na klabu hiyo, wakasema wanampenda ila dau la kumbakisha hawana, akatimka zake.

Yaani kwa ufupi ni kwamba, toka Simba walipochukua ubingwa 2011/12 chini ya kocha Mserbia Milovan Circovic, imepitia mikononi mwa makocha wengi bila kumsahau Mfaransa Patrick Liewig, ambaye kwa sasa anainoa Stand United.

Ni wazi kwamba, kama Simba wangetulia na kocha mmoja kati ya hao huenda wasingemaliza misimu minne bila kutwaa ubingwa. Mfano kocha kama Kopunovic, alikuwa na uwezo mkubwa wa kufundisha soka, ndiyo maana hata alipoondoka wachezaji na mashabiki walichukia sana na hii ni kutokana na uwezo wa ufundishaji aliokuwa nao, lakini viongozi wakamuachia akaondoka zake.

Mafanikio ambayo Yanga wameyapata katika misimu hiyo minne wakati Simba wamekuwa wakihangaika ni kutokana na kuwaamini makocha ambao wamewapa kazi na pia kutokuwaingilia kwenye majukumu yao.

Ni kweli kwamba hata Yanga wamewaacha baadhi ya makocha, akiwamo, Mbrazil Marcio Maximo, lakini wao wamekuwa wavumilivu kidogo, ndiyo maana haya mafanikio waliyoyafikia walistahili.

Lakini wakati hayo yote yakitokea, zipo taarifa kuwa mabingwa hao wa Ligi Kuu Tanzania Bara wanataka kuachana na kocha wao mkuu, Mholanzi Hans van der Pluijm, huku pia taarifa hizo zikitanabahisha kuwa benchi zima la ufundi halitabaki salama.

Yaani Pluijm ataondoka na msaidizi wake, Juma Mwambusi, kocha wa makipa Juma Pondamali na meneja wa kikosi hicho, Hafidh Saleh, licha ya kwamba watu hao wamefanya kazi kubwa sana.

Yanga, ambao wanapigania kutetea ubingwa wao mbele ya Simba, wanaoonekana kujipanga vilivyo msimu huu, wanataka kumchukua Kocha Mkuu wa Zesco ya Zambia, George Lwandamina.

Ni kweli kwamba Lwandamina ni kocha mzuri, kwani CV yake inajulikana, lakini najiuliza Yanga wamekosa nini kwa Pluijm mpaka kutaka kuachana naye? Wamesahau mambo makubwa aliyowafanyia? Au wamechoka tu kumuona na miwani yake?

Msimu uliopita ni kama Yanga wamepata kila kitu kwa Pluijm na wasaidizi wake na wote tumeona ushiriki wao kwenye michuano ya kimataifa, wakitinga hatua ya makundi Kombe la Shirikisho Afrika na kupangwa na timu vigogo, ikiwamo TP Mazembe waliokuwa mabingwa watetezi wa michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Baada ya taarifa kuvuja za Yanga kutaka kumuacha Pluijm, uongozi kupitia kaimu katibu mkuu wao, Baraka Deusdedit, aliibuka na kukanusha kwamba hawana mpango huo, lakini ukweli ni kwamba, jambo hilo lipo.

Nasema jambo hilo lipo kwa sababu licha ya Yanga kukanusha, kocha huyo mwenyewe amethibitisha kufuatwa na Wanajangwani hao na kwamba wapo katika mazungumzo, licha ya kuwa ana ofa nyingine kwenye Klabu ya Free State ya nchini Afrika Kusini.

Hata kipindi kile vyombo vya habari viliporipoti kuwa Yanga wanafanya mazungumzo ya kumleta Marcio Maximo, walitumia nguvu nyingi kukataa, lakini mwisho wa siku Mbrazil huyo alikuja akafundisha siku zake chache pamoja na ndugu zake kama Andrey Coutinho Emerson, pamoja na Jaja, baadaye wakatimka zao.

Suala la msingi hapa ambalo najiuliza na wadau wengi wanajiuliza kwamba, Yanga wanaanzaje kumuacha Pluijm? Binafsi naamini kwamba, Wanajangwani hao watafanya kosa kubwa kumuacha na wanaweza wakapotea kama walivyopotea Simba misimu kadhaa iliyopita.

Nadhani pia hata lile bao la Shiza Kichuya linaweza kuwa sababu ya Pluijm kutaka kutimuliwa, kwani nina uhakika kama wangeifunga Simba mchezo huo haya yote yasingezungumzwa. Hizi timu zetu pasua kichwa aisee.

NA EZEKIEL TENDWA, sirtendwa@gmail.com, 0789291209

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika ujumbe kupitia ukurasa wake wa...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya kinda wa zamani wa timu...

Afua Suleiman afunguka ‘Utalijua Jiji’ ilivyompa ustaa mjini

NA JEREMIA ERNEST JINA alilopewa na wazazi wake ni Afua Suleiman na hata alipojitupa kwenye ulimwengu wa muziki wa...

Keche: Kundi maarufu Ghana linalowatamani Diamond, Kiba, Harmonize

JIACHIE na Staa Wako, wiki hii tumetua mpaka Accra, Ghana kwa kundi maarufu la muziki nchini humo, Keche linofanya vizuri na ngoma...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -