Wednesday, October 28, 2020

YANGA, MWANJALI WAMALIZANA FASTA

Must Read

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya...

HUSSEIN OMAR NA EZEKIEL TENDWA

YANGA wajanja sana asikwambie mtu, kwani wamegundua kuwa ukuta wa Simba unaoongozwa na Method Mwanjali, ndio ambao hadi sasa haujaruhusu mabao mengi katika mechi za Ligi Kuu Tanzania Bara hivyo kuamua kumalizana mapema na   Mzimbabwe huyo.

Japo Yanga wamekuwa wakidai kutoifikiria mechi yao ya ligi dhidi ya watani wao wa jadi Simba itakayopigwa Februari 25, mwaka huu na badala yake kuelekeza nguvu zao zote katika mchezo wao wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Ngaya de Mbe ya Comoro, imebainika kuwa Wanajangwani hao wanazuga tu.

Kinachoonekana ni kwamba, Yanga wana hasira mno na Simba na  wanachokifikiria kwa sasa ni jinsi ya kuwasambaratisha watani wao hao watakapokutana nao siku hiyo kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam na hivyo kuwa na nafasi kubwa ya kutetea ubingwa wao wa Bara.

Kwa kufahamu kuwa Mwanjali ndiye mchezaji pekee katika safu ya ulinzi anayeweza kuwapa wakati mgumu washambuliaji wao kupata mabao, benchi la ufundi la Yanga lilikaa na kuumiza vichwa kuona ni vipi wanaweza kuvuna mabao dhidi ya wapinzani wao hao na kupata jibu.

Unajua wamepania nini Wanajangwani hao? Ni hivi, kocha mkuu wa Yanga, George Lwandamina pamoja na wenzake, wamewatengenezea dawa maalumu washambuliaji wao kuhakikisha wanamtesa Mwanjali na wenzake na hivyo kufunga mabao kadiri watakavyopata nafasi Februari 25.

Katika mazoezi ya Yanga yaliyokuwa yakifanywa Uwanja wa Taifa kwa takribani siku nne kabla ya kukwea pipa kwenda nchini Comoro leo kupepetana na Ngaya de Mbe, Lwandamina alionekana kusuka zaidi safu yake ya ushambuliaji ambayo inaongozwa na Amis Tambwe.

Katika mazoezi hayo, Lwandamina alikuwa akiwaonyesha washambuliaji wake namna ya kuwatoka mabeki wakorofi na wenye nguvu kama ilivyo kwa Mwanjali, lakini pia namna ya kuwazidi ujanja mabeki wenye tabia ya kupaki basi.

Mzambia huyo alikuwa akigawa timu yake katika makundi matatu, akiwapanga wachezaji wanne kwa watatu na kuanza kucheza ambapo wale watatu walitakiwa kuanza mashambulizi na kukabwa na wale wanne.

Zoezi hilo ambalo lilifanyika katika utulivu mkubwa, lilidumu kwa zaidi ya saa moja ambapo lililenga kuwawezesha washambuliaji kupata mbinu za kuwatoka mabeki wanne ambao ni wengi zaidi yao.

Baada ya kumaliza zoezi hilo, Lwandamina aliwafundisha wachezaji wake namna ya kufunga mabao pale inapotokea wamebaki na beki mmoja au wawili wa timu pinzani.

Katika zoezi hilo, Obrey Chirwa, Tambwe na Simon Msuva, walionekana kumkuna vilivyo  kocha huyo na wenzake kutokana na jinsi walivyomudu kuwapita mabeki Kelvin Yondani, Nadir Haroub ‘Cannavaro’ na Pato Ngonyani na kuwafunga makipa Ali Mustapha ‘Barthez’ na Deogratius Munish ‘Dida’.

Na kwa jinsi ilivyoonekana, iwapo Tambwe, Msuva na Chirwa watazingatia maelekezo waliyopewa, Mwanjali na wenzake wanaounda safu ya ulinzi ya Simba, watakuwa na wakati mgumu Februari 25 iwapo watapoteza umakini wao.

Hata hivyo, ifahamike kuwa Simba ambao wapo nafasi ya pili katika msimamo wa ligi, ndiyo yenye safu imara zaidi ya ulinzi kwani imeruhusu mabao saba tu ambayo ni machache kuliko timu yoyote inayoshiriki Ligi Kuu Bara.

Kwa upande wao, Yanga imefungwa mabao tisa lakini ikicheka na nyavu mara 46 dhidi ya 35 kwa Simba.

Katika hatua nyingine, wanachama na wapenzi wa Tawi la Yanga la Msasani, Dar es Salaam, wanatarajiwa kukutana kesho katika ukumbi wa Sisi Club Msasani uliopo Mtaa wa Mikoroshini.

Msemaji wa tawi hilo, Lincoln Tumbo, alisema: “Tunawaomba wapenzi na wanachama wa Yanga wa tawi letu kujitokeza kwa wingi katika mkutano huo ili kujadili mambo mbalimbali kuhusiana na klabu yao, yakiwamo maandalizi ya mchezo wetu wa Februari 25, mwaka huu dhidi ya Simba kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.”

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika ujumbe kupitia ukurasa wake wa...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya kinda wa zamani wa timu...

Afua Suleiman afunguka ‘Utalijua Jiji’ ilivyompa ustaa mjini

NA JEREMIA ERNEST JINA alilopewa na wazazi wake ni Afua Suleiman na hata alipojitupa kwenye ulimwengu wa muziki wa...

Keche: Kundi maarufu Ghana linalowatamani Diamond, Kiba, Harmonize

JIACHIE na Staa Wako, wiki hii tumetua mpaka Accra, Ghana kwa kundi maarufu la muziki nchini humo, Keche linofanya vizuri na ngoma...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -