Sunday, November 29, 2020

YANGA NA AZAM BADO ZINA NAFASI ZA MICHUANO YA AFRIKA

Must Read

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali...

NA MWANDISHI WETU

MICHUANO ya kimataifa kwa timu za Tanzania Bara inaoekana kuwa migumu sana msimu huu. Wawakilishi wa Tanzania Bara kwenye michuano hiyo klabu za Yanga na Azam, zimekuwa katika sintofahamu ya kusonga mbele kwenye michuano hiyo kutokana na hali ya matokeo ya michezo ya awali waliyocheza nyumbani.

Licha ya kwamba Azam FC waliibuka na ushindi wa bao 1-0 kwenye uwanja wao wa Azam Complex uliopo Chamazi, lakini ushindi huo waliousubiri hadi dakika ya 81 bado hautoi matumaini makubwa ya timu hiyo kuwatoa wapinzani wao Mbambane Swallows kutoka Swaziland. Hali hii inatokana na kiwango kizuri na kikubwa walichoonesha wapinzani hao wa Azam katika mechi yao ya ugenini, kwa mantiki ya kwamba mechi yao ya nyumbani watafanya kila wawezalo kupata ushindi mbele ya mashabiki wao.

Yanga ambayo ililazimishwa sare ya bao 1-1 na Zanaco FC ya Zambia, nayo pia ina wakati mgumu sana, inahitaji kupata ushindi au sare ya kuanzia mabao 2-2 ili kufuzu kwa hatua ya 16 ya michuano ya Klabu Bingwa Afrika msimu huu.

Tuziangalie timu zote mbili na safari yao kuelekea katika mechi zao za marudiano ambazo zitachezwa mwishoni mwa wiki hii huko Swaziland na Zambia.

Yanga SC

Imani waliyonayo mashabiki wengi wa klabu hiyo ni ile hali ya mazoea ambayo wamekuwa nayo katika kipindi cha miaka ya hivi karibuni, kwamba timu yao inacheza soka zuri ikiwa ugenini na kucheza vibaya ikiwa nyumbani.

Tangu timu alipoichukua Hans van der Pluijm, Yanga wamekuwa na kawaida ya kucheza kwa kujituma zaidi wanapokuwa ugenini, mechi mbili za ugenini dhidi ya Al Ahly ya Misri licha ya kupoteza zote lakini walicheza soka la uhakika. Wakiwa ugenini pia wakacheza soka safi dhidi ya Etiole du Sahel ya Tunisia na hivi juzi tu wameshinda mabao 5-1 ugenini huko Shelisheli kabla ya kutoa sare ya bao 1-1 kwenye Uwanja wa Taifa.

Kumbukumbu ya mashabiki wa Yanga inaikumbuka pia mechi dhidi ya APR ya Rwanda ambayo Yanga ilishinda 2-1 jijini Kigali na kuja kulazimishwa sare ya bao 1-1 Uwanja wa Taifa, pengine hii ndiyo silaha pekee inayowapa matumaini mashabiki wa Yanga ambao kwa sasa ukiwasikia, wanasema Zanaco anakwenda kufia kwao.

Kiufundi Yanga ilionekana kuzidiwa kila kitu la Zanaco, ilikuwa timu dhaifu sana kwenye eneo la kiungo na timu masikini eneo ya ushambuliaji. Japo Zanaco wameonekana kumaliza kikosi cha kwanza, lakini Yanga pia ilibakisha nje wachezaji wawili tu kwenye kikosi cha kwanza ambao ni Haruna Niyonzima eneo la kiungo mshambuliaji na Amissi Tambwe eneo la ushambuliaji.

Je, Tambwe na Niyonzima wakiwa sawa wanaweza kuibeba Yanga? Jibu la swali hili ni gumu hasa kutokana na aina ya upangaji kikosi cha Yanga ulivyo hivi sasa, kocha Geoge Lwandamina anapanga viungo wengi lakini wote wanye akili ya ukabaji. Bado hajamwamini Deusi Kaseke ndiyo maana katika mechi ya kwanza alimweka benchi na kuamua kumwanzisha Mzambia mwenzake Obrey Chirwa pembeni, jambo ambalo liliigharimu Yanga katika suala zima la ushambuliaji.

Kwa hali ilivyo Yanga wanaweza kupata bao zaidi ya moja kwenye mechi ya marudiano, lakini ili mabao hayo yapatikane benchi la ufundi linapaswa kukaa na wachezaji wake kuzungumza nao bila kupindisha maneno. Kwamba Emmanuel Martin sasa aache kutafuta sifa zake binafsi na badala yake atafute matokeo ya timu, hivyo aache uroho wa kutaka kufunga yeye mwenyewe hata anapokuwa katika mazingira magumu.

Wamfunde vilivyo mshambuliaji huyo anayechipukia ambaye kwenye mchezo wa kwanza baada ya kuingia kuchukua nafasi ya Donald Ngoma, alipoteza nafasi tatu ambapo aling’ang’ana mwenyewe kupiga mashuti yaliyokwenda nje ya lango wakati wenzake walikuwa kwenye nafasi nzuri za kufunga kama angewachukulia na kuwawekea mpira katikati.

Lazima Martin aambiwe kwamba kutoa pasi ya goli ‘Assist’ kuna maana na heshima kubwa sana pengine hata kuliko kuuweka mpira wavuni. Lakini wakati Martin akiambiwa hivyo, Lwandamina na benchi lake la ufundi nao watolewe uvivu waambiwe wazi masuala ya kufanya majaribio kwenye mechi muhimu ambayo timu inahitaji matokeo waache.

Wakati msaidizi wake Juma Mwambusi akijinasibu kwamba alikuwa na uhakika wa kumpanga Kelvin Yondan kiungo mkabaji, lakini Yanga walionekana wazi kwamba wanacheza kamari kwani Yondani hakuwa na mchezo mzuri hata alipocheza na Mtibwa, kwani mara kadhaa alijikuta yuko nyuma ya mabeki jambo ambalo lilimfanya Vicent Bossou kumhimiza kupanda mbele.

Kwa ujumla ndhani yote haya Yanga waliyaona, lakini jambo jingine kubwa na la msingi zaidi ni nidhamu ya mchezo, wachezaji wa Yanga wamekuwa na udhaifu mkubwa wa kuridhika hasa kama wanaongoza.

Kwa kuiangalia mechi ya kwanza dhidi ya Zanaco, Yanga walijua wazi kwamba wameshashinda mchezo huo hivyo wakaanza kucheza ilimradi muda uishe  ndiyo maana Chirwa alipopoteza mpira akalala chini kama vile ameulia na mpira huo alioupoteza ukaenda hadi kuingia langoni kwake Wazambia wenzake wakasawazisha.

Mambo wanayotakiwa kufanya

Jambo la kwanza ambalo Yanga wanatakiwa kufanya kwenye mechi ya marudiano, ni kuacha masihara kando ili kusaka ushindi. Washambuliaji wanatakiwa kuongeza umakini ili nafasi zinazotengenezwa zitumike ipasavyo, kwani kuna kila dalili kwenye mchezo huo Zanaco wakabana nafasi ya Yanga kutengeneza mashambulizi mengi.

Wapate bao, lazima Yanga wajitahidi kulazimisha kupata bao, kwani kuna uwezekano mkubwa Zanaco wasihitaji kupata bao hivyo wakicheza mchezo utakaowaruhusu Yanga kufarijika na kujikuta wakipata sare tasa ambayo inakuwa imewafungashia virago kwenye mashindano hayo.

Safu ya kuingo lazima iimarishwe, viungo wa Yanga wahakikishe wanatawala dimba ili kuwazuia Zanaco kucheza sana eneo la katikati. Kwa akili ya kawaida Zanaco watacheza mechi hiyo kwa lengo la kushambulia zaidi hivyo ni wazi kwamba watajaza viungo wengi na wenye kasi eneo la katikati, hivyo basi viungo wa Yanga lazima wakumbuke mechi yao ya marudiano dhidi ya Al Ahly aina ile ya mchezo ndiyo inatakiwa watakaporudiana na Zanaco, watumie viungo wa pembeni wenye kazi kama vile Kaseke na Simon Msuva.

Safu ya ulinzi ya Yanga haipaswi kufanya makosa ya kizembe kama ambayo yalifanyika kwenye mchezo wa kwanza ambayo wakati mwingine yalifutwa na umahiri wa kipa Deogratius Munish ‘Dida’, wanapaswa kuwa makini zaidi na winga wa kushoto na kulia ambao ndiyo wameonekana kuwa injini ya mashambulizi ya Zanaco. Makosa kidogo tu yatawapa nafasi Zanaco ambao bila shaka sasa watakuwa watulivu zaidi kwa kuwa watakuwa wanacheza nyumbani.

Azam FC

Ushindi wa bao 1-0 ni kama hautoshi, Azam haikutengeneza nafasi nyingi za kupata mabao katika mechi ya kwanza. Mbambane Swallows walionekana wazuri zaidi eneo la kiungo na ni kama vile waliilazimisha Azam kucheza walivyotaka wao muda wote wa mchezo.

Kama Agrey Morris hatakuwa fiti kwa ajili ya mchezo huo, basi benchi la ufundi la Azam liangalie namna ya kumtumia beki mwingine wa kati kama Erasto Nyoni au David Mwantika kama yuko vyema, ambao wanaweza kucheza kwa kujiamini na kwa kutumia akili zaidi kuliko yule Mghana Daniel Amoah   ambaye tangu alipoingia hakuwa na utulivu na hivyo kufanya makosa mengi yaliyomweka kipa wake Aishi Manula kwenye misukosuko kila wakati.

Safu ya kuingia ilipwaya, Salum Abubakar, Frank Domayo na Hamid Mao wote walilazimishwa kucheza nyuma ya mstari kuelekea langoni kwao, hivyo kutoa nafasi ya viungo wa Mbambane Swallows kutawala aneo la katikati na hivyo kucheza mipira yote iliyotoka Azam na ile iliyokaa langoni kwao. Viungo hawa wanaoheshimika sana kwenye soka Tanzania walionekana kukosa mipango mizuri kwenye mchezo huo, hivyo wanatakiwa kuwa makini mno kwenye mchezo ujao ambao Azam inahitaji pia matokeo ya ushindi ingawa sare tu inatosha kuwavusha.

Wanachotakiwa kufanya Azam

Kwanza kubadili safu ya ushambuliaji ili iwe na makali zaidi, kama John Bocco bado hayuko fiti, basi ni vyema kocha akaamua kumchezesha Shaban Idd  moja kwa moja badala ya kuanza na Yahaya Mohammed ambaye kwenye mchezo wa kwanza hakuonekana kufanya chochote chenye madhara kwa mabeki wa Mbambane.

Azam wanapaswa kushambulia kupata bao la mapema ili kujiweka salama zaidi. Kocha anapaswa kufikiria mfumo wa kulenga ukuta mkali wa viungo mbele ya ukuta wa mabeki watatu, ili kutoruhusu ule mchezo wa Mbambane wa kuchezesha mawinga wao.

Pengine mfumo sahihi zaidi kwa Azam kwenye mechi ya marudiano unapaswa kuwa 3-5-2, kwani nguvu kubwa ya wapinzani wao iko eneo la katikati ambalo kama likifa tena basi Azam itakuwa matatizoni.

Pamoja na yote umakini unatakiwa zaidi kwa kila mchezaji, bahati nzuri Azam si wapotezaji sana wa mipira inapokuwa miguuni mwa wachezaji, lakini wana udhaifu mkubwa katika kugombania mpira ambapo katika mechi kwanza kati ya tashtiti 13 zilizotokea baina ya wachezaji wa Azam na Mbambane, mbambali waliongoza kwa kuchukua mipira mara tisa (9) Azam wakipata mara tatu na mara moja mwamuzi akiamua  kwa kuwapa mpira Azam.

Makosa ya mabeki yanapaswa kuwa yameishia Chamazi, kama ambavyo imeelezwa hapo juu, ni bora kocha akamwangalia Erasto Nyoni kama Morris hatakuwa fiti kuliko kucheza kamati ya Amoah.

Watanzania bado wanahitaji kuona mafanikio ya timu zao kwenye michuano ya kimataifa, japo msimu huu unaoenakana kama utakuwa mchungu pengine hata kuingia robo fainali, lakini Azam inaweza kuvuka raundi hii na Yanga nao kwa nidhamu ya hali ya juu wakicheza ugenini wanaweza kusonga mbele ingawa kwa viwango vilivyoonekana kwenye mechi za awali, kuna viashiria kwamba kunahitajika kazi ya ziada na mambo ili timu zetu zote kusonga mbele.

Kila la heri Azam FC, kila la heri Yanga SC

Mungu ibariki Tanzania.

0682300935

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...

Sarpong ‘aua’ shabiki Simba

Na MWANDISHI WETU, MWANZA BAO la dakika ya 29 lililofungwa na Michael Sarpong wa Yanga juzi, limesababisha kifo cha...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -